Kuachiliwa kwa watu waliokuwa mahabusu

Lamkyeku

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
494
661
Wakuu salaam. Watu wetu waliokuwa mahabusu za polisi za Central na OysterBay wameachiliwa kwa dhamana ya Mahakama. The Vwawa Four, yaani waliokamatwa Vwawa, Songwe, walirudishwa Vwawa juzi usiku na jana walifikishwa mahakamani.

Leo wametoka kwa dhamana. The OysterBay Five, waliokuwa wanashikiliwa OysterBay wamesomewa mashtaka mchana huu na kupata dhamana.

Ignasia Mzenga alirudishwa Morogoro na Alex John wa Dodoma pia wote hawa wamesomewa mashtaka yao jana na taratibu za dhamana zinafanyika.

Tumetoka mahakamani muda huu. Watu wetu wako huru. Ni furaha kubwa kwao na kwetu pia. Nawapongezeni wote mlioshiriki katika kupaza sauti zenu hadi watu wamepata dhamana.

Tuendelee na utaratibu huu wa kusaidiana nyakati hizi za giza na mateso. Aluta continua.

Anaandika Tundu Lissu.
 
Ahsante sana mtu mwenye akili nyingi sana uliyazaliwa Tanzania... Ingekuwa ulaya ungekuwa Nuru kubwa sana kwa Tanzania yetu umekuwa Adui na mwiba.. Congrats Mh T. LISU
 
Back
Top Bottom