Kua uone

Kua uone

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,763
Reaction score
57,339
Nakwea Bila ngazi
Maskini huchechemea Bila vazi
Nchi wanaichezea kila dansi
Huku tukitizama wanavyojimegea ardhi
Wamezindikwa na mganga
Hii Siri Ni Kali nagubikwa na utata
Mtanza kajibanza chocho
Huku Akiangaza wanavyosaza Hadi makombo
Pigo la Kwanza takatifu wamekauka jasho wanataka kuichana hanger-chief
Mtawala madarakani
Wapo machokoraa waliolala majalalani
Tiba Bora hatupewi sisi
Nyama iliyonona vipi amegewe fisi
Hawana hotuba za maana
Sisi tukipigika kwao dhoruba mwanana

Kua uone wanaokula nchi
Kua uone wanaotembea nusu uchi
Fungua usome
Kisha paza sauti
Ugua upone
Yasikufike mauti *2

Kua uone unyumba ulivogeuka soko
Utadhania mitumba inavyoanikwa mitoko
Uchumi unayumba viongozi wanakula hongo
Watu wanakula pesa za waliofunikwa udongo
Kua uone penye haki hakuna usawa
Everybody knows now days money power
Yakitokea majanga wanaota mbawa
Tunabakia mihanga
Namna gani watu Hawa
Njoo usome nyaraka za serikali
Uzikomboe haraka rasilimali
Kua utuondoe kwenye hii hali
Kufika nchi ya ahadi ipungue umbali
Kua usome ingawa uchumi umekata kauli
Juzi imepanda nauli
Wapi nitapata ada sijui
Bado asubuhi kubangaiza hainisumbui
Askari wanaonitatiza Sina uadui

Kua uone wanaokula nchi
Kua uone wanaotembea nusu uchi
Fungua usome
Kisha paza sauti
Ugua upone
Yasikufike mauti *2

Kua uone vicheche wa mashavuni
Kua uone vishada vya ughaibuni
Shindua upone achana na sabuni
Zinduka usome usidate na uhuni
Ona mafisadi na madikteta wameshika hatamu Sheria ime vioderater
Haki wameikeketa
Leo uzalendo wameupepeta
Kua uone mkono wa birika na mkono wa Sweta
Uone wanaokula kwa kalamu na wenye kutweta
Zunguka usonge
Tupambane na kimeta
Funguka tulonge na kibonge anayemeremeta
Kua uone wanaong'ata na kupuliza
Vichwani Wana majibu na maswali wanajiuliza
Wachunguzi wameperuzi na upekuzi hawajamaliza
System iko corrupt bongo inatubabatiza
Kua uone jinsi watu wamekata ringi
Kua uone mashuga dadi na mashangingi
Zingua uone utakavyoingizwa kingi
Jipindue usikonde utaidaka shilingi

Kua uone wanaokula nchi
Kua uone wanaotembea nusu uchi
Fungua usome
Kisha paza sauti
Ugua upone
Yasikufike mauti*2

Kua ujue kusoma na kuandika
Kua ujue kuomba na kutambika
Kua ujue kupenda na kuachika
Kua ujue ni noma tz usipochakarika
Ukikua utayaona mengi
Utajua Kuna kuishiwa na kuweka Bondi
Utawaona maskini wakispend
Utajua bila ya ndinga unaweza ukapinga ng'ondi
Utaona kuishi na utaonja kufa
Utapata scholarship utapiga masafa
Utamuona maskini jeuri na fogo masifa
Utaona starehe sherehe na maafa kwenye taifa
Utapata kazi au utakuwa chokoraa
Utakuja underground au utakuwa superstar
Mshukuru MUNGU ukiwa mzima unaweza kuwa kichaa
Ukiugua kifua Ni vema ukiokoa mtaa
Utaona mabitoz na ma gangster
Utawasoma ma gay na wangster
Kama kawa masheikh na ma pastor
Weupe weusi kipara na marasta
Utaona ma HB,bad couples na warembo
Utaona wanyama mfano wa chui na tembo
Utazisikia lugha kiswazi na kimombo
Utacheka ukiziona picha zako za kitambo


Kua uone wanaokula nchi
Kua uone wanaotembea nusu uchi
Fungua usome
Kisha paza sauti
Ugua upone
Yasikufike mauti*2
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom