Ku-copy na ku-paste style za member wa JF

Jamaa kafanya plagiarism ya Hali ya juu
Kiukweli sijapenda hata kidogo. Then utakuta ni member wa hapa hapa JF na anajua alichokifanya, na hapa kazi yake kubwa kujisifia ujinga mtupu.
 
Vipi ulishajisajili BASATA tufungue kesi ya madai, tupige pesa[emoji849][emoji849]
 
Duh! Pole sana Da'Vinci. Aisee! Hivi JF huwa hawana mambo ya Copyright?!
 
Pole sana.
 
Tumshauri mwenzetu hatua za kufanya, maana hili swala la kukopiwa limemletea msongo wa mawazo na kumwathiri kisaikolojia.
Halijaniathiri ila sio vizuri. Maana hata gerezani ndani ya Marekani uliwahi kuingia mtindo wa uvaaji kwa wafungwa na watu nje ya gereza wakawa wanaiga mtindo huo huo wa uvaaji bila kujua wale wafungwa walikuwa wanamaanisha nini kuvaa vile! Inatakiwa kwanza ujue mwenzio anamaanisha nini ndipo uige kama ni jema na sio kila kitu unaiga!!
 
Kiukweli sijapenda hata kidogo. Then utakuta ni member wa hapa hapa JF na anajua alichokifanya, na hapa kazi yake kubwa kujisifia ujinga mtupu.
Unajua uhalisia ni uhalisia tu, atapata likes na comments ila moyoni mwake atajua sio yeye ni za jamaa fulani. Japo tabia hiyo inaboa ila inaweza kukuonesha kiasi gani watu wanapenda madini yako.
 
Hata Mimi sijaona tatizo maana kama ni emoj kila mtu anazo kwenye simu na ni haki yake kuzitumia atakavyo
Sawa, ila kuna mtindo mtu huwa anabuni katika huo utumiaji, kama unataka kutumia mtu si na yeye abuni mtindo wake?! Mtu anakopi post kama ilivyo!! What a shame!!
 
Hii imekuwa kawaida sana siku hizi. Mimi kuna post yangu moja ilitoka humu ikapelekwa Facebook. Baada ya muda, kuna mtu akaitoa Facebook na kuirudisha humu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Minmi ninadhani kupeleka mada nje ya JF si dhambi. Lakini ukichukua kazi ya mtu kiri kuwa si yako kwa kumnukuu.
Kama mada ni kubwa ni vizuri kufanya hivyo. Ila kama ni hizi fupi fupi basi walau usikopi kama ilivyo!! Buni mtindo wa kuwasilisha na sio unacopy kama Photocopy bila kuacha hata nukta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…