KTB yatarajia sekyta ya utalii kuendelea kunawiri 2017

GODLOVEME

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,643
494
Halmashauri ya utalii nchini Kenya KTB imesema ina imani kwamba watalii wengi watatembelea kenya licha ya kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi ,

Mkurungezi wa KTB Betty Radier amesema sekyta hiyo inatarajiwa kuendelea kufanya vyema kama mwaka wa 2016.

Alisema wameweka mikakati ya kuitangaza Kenya kwenye masoko ya watalii huku uchaguzi ukitarajiwa baadaye mwezi Agosti.

Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na kufanya kampeni za kuhakikishia watalii usalama wao na pia kupigia debe utalii wa nyumbani.

Mwaka 2016 sekta hiyo ilionekana kufanya vyema baada ya kipindi cha miaka mine cha kupungua kwa watalii huku ikiwa na ongezeko la asilimia 12.

Mwaka jana kulikuwa na watalii 983,876, ikilinganishwa na 874,544 wa mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom