Kozi za Engineering ziige kozi za Afya

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Barabara zinajengwa na Wachina, Wajapan, Waitaly huku upenuni kwetu, wanafunzi wetu wanajifungia tu vyumbani wakikariri vitu vya kizamani ambavyo katika Ulimwengu wa Engineering havipo tena.

Hivi kwanini huko kwenye ujenzi, viwanda n.k. tusiwe tunawapeleka wanafunzi wetu wakafanya kazi labda miaka miwili au mitatu sawasawa na madaktari au manesi wanavyofanya kwenye fani zao?

Sasa hizi Barabara zetu za wilaya nani atajenga kama engineers wetu wanasomaga theory tu.
 
Mkuu kuna programme inaitwa SEAP (Structured Engineering Apprenticeship Programme) ilikuwa efficient sana ilianzishwa zaidi ya miaka 10 iliyopita . Mimi nilikuwa mmoja wa wanufaika wa programme hiyo enzi hizo. Inasikitisha haikuendelezwa wala kukazaniwa na kuboreshwa kiasi cha kutosha imekuwa ni kama haipo sasa hivi. Ilivyokuwa ni kwamba baada tu ya graduation mnatuma maombi kwenda Engineers Registration Board na baada ya muda yule anayefaa (ambaye credentials hazina shida) anapangiwa kituo cha internship yake,kabla ya kwenda vituoni mnafanyiwa semina ya programme breakdown/scope,report writting na manners na kupewa logbooks ambazo unatakiwa kuwasilisha ERB mara moja kwa miezi mitatu zilizosainiwa na msimamizi wako ambaye anatambulika (Registered Professional Engineer). Serikali ilikuwa ikitoa posho kwa kila mwezi nakumbuka ilikuwa ni 128,000 kwa mwezi. Ila baadaye nilikuja kusikia fedha zilikosekana na serikali ilijitoa kuifadhili kwa hiyo kwa sasa wanafanya wanawake tu kwa ufadhili wa nchi fulani za wazungu katika mpango wa kuongeza idadi ya Engineers wanawake. Japo haikuwa mandatory lakini ilisaidia kwani ilikuwa ukimaliza miaka hiyo mitatu unawasilisha report ya mwisho na kuomba registration kama Registered Professional Engineer (PE)
 
Barabara zinajengwa na Wachina, Wajapan, Waitaly huku upenuni kwetu, wanafunzi wetu wanajifungia tu vyumbani wakikariri vitu vya kizamani ambavyo katika Ulimwengu wa Engineering havipo tena.

Hivi kwanini huko kwenye ujenzi, viwanda n.k. tusiwe tunawapeleka wanafunzi wetu wakafanya kazi labda miaka miwili au mitatu sawasawa na madaktari au manesi wanavyofanya kwenye fani zao?

Sasa hizi Barabara zetu za wilaya nani atajenga kama engineers wetu wanasomaga theory tu.
Unajua tofauti kati ya injinia na contractor?? Unajua hizo barabara wanazojenga wachina nani ame design?
 
Mkuu umeuliza swali zuri sana, wengi wanazungumzia taaluma ya Uhandisi ila hawaelewi uhandisi ni nini? Wanashindwa kutofautisha Mkandarasi na Mhandisi, na hata kujua jinsi inavyofanya kazi.
 
Kweli mkuu yaani nakumbka semister ya kwanza tu nipo hospital nafanya vitendo kwa MLT miaka 3 asee namaliza najua kila kitu kama nina miaka 8 kazini.
Ila so mbaya theory wapo vzuri

Kozi gani hiyo ulienda hospitali ukapractice ukiwa sem 1?
 
Mkuu Unaongea kitu usichokijua kabisa Unajua kuna tofauti kati ya Mkandarasi na Mhandisi hao wajina mostly ni wakandarasi japo wahandisi wapo pia
 
acha siasa nyingi, in short mnakariri madesa tuu
 
Msaada jamani nachukua clinical medicine chuo cha kampala nahitaji kuhamia cha serikali je inawezekana na kama inawezekana naanzaje mchakato?
 
Back
Top Bottom