Kozi ngumu, ajira hakuna

Kozi ngumu, ajira hakuna

Mr Global

Senior Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
150
Reaction score
125
Kwanza nianze na pole wale mliosoma Bsc PHYSICS, MATHEMATICS na BIOLOGY kwa ugumu wa kazi lakini pia niwaambie ukweli hizi kozi hazina hajira kabisa na kama zipo basi mara moja ndani ya miaka miwili.

Hapo mwanzo kozi hizi zilianzishwa kwa ajili ya kupunguza tatizo la walimu wa sayansi,walipomaliza walichukulia chap na baadae waliombwa waingie kwenye ualimu (wasome postgraduate diploma PGDE) Lakini kwa sasa hali in tete kwan hawaitajiki tena
Mwaka Jana 2019, TAMISEMI waliwapangia watu hawa vituo vya kazi ya ualimu lakini UTUMISHI waliwarudisha kwa sababu walikosa sifa ya ualimu. Kwa maana hiyo hawaaitajiki tena, ila cha kushangaza chuo bado kinadahili hawa watu....

Ushauri wangu tu,,hawa watu wasi-dailiwe tena na hao waliosoma basi tufanye tumetoa sadaka. Kwa sababu hata leo ukimuuliza LECTURE wa hiyo kozi kuhusiana na wapi nitafanyia field hii kozi yangi HAJUI

Poleni wahanga wezangu, tuendelee kusaga na lumba jua na mvua kwa mpigo

Never give up!!
 
Kwani watu wa hizo kozi option ni kufundisha tu hakuna nyingine?
 
Kupanga ni kuchagua! Mtu aliyesoma BSc Physics and whatever can not be a teacher, simply b'coz hajasoma kozi yoyote ya elimu/ualimu and so he/she is not prepared to be a teacher!

Kama alitaka kuwa mwalimu alipaswa kusoma BSc. Ed majoring in either chemistry, biology, physics or mathematics.
 
Kila unapoenda watu hawakuelewi, wanakuambia wewe in mwalimu ukija kwenye ualimu wanakuambia we we sio mwalimu
Yaan, full mastress mkuu.
 
Kupanga ni kuchagua! Mtu aliyesoma BSc Physics and whatever can not be a teacher, simply b'coz hajasoma kozi yoyote ya elimu/ualimu and so he/she is not prepared to be a teacher!

Kama alitaka kuwa mwalimu alipaswa kusoma BSc. Ed majoring in either chemistry, biology, physics or mathematics.
Nachojaribu kuzungumzia ni kwamba watu wa kozi hizo wana kazi ya kufanya ili watambulike na waajiri la sivyo watakaa na historia kwamba walipitia chuo na walisoma kozi fulani lakini hakuna watakachoapply kutokana na walichokisoma
 
Poleni sana wakuu, tafuteni fursa sehemu zingine ikibidi
 
Kweli Mkuu..ila sie tupo kwenye nchi zinazoendelea ndio shida
 
Mhh hii mbona balaa, ila maybe afanye kokote tu pale ambapo watahitaji degree
 
Bsc in physics wanaajiriwa Sana TBS na wakala wa vipimo.

Pia wanaajiliwa Sana tume ya mionZi ya atomiki.
 
Kila unapoenda watu hawakuelewi, wanakuambia wewe in mwalimu ukija kwenye ualimu wanakuambia we we sio mwalimu
Yaan, full mastress mkuu.
Shida yetu tuna kariri, yan unasoma kozi baada ya either kukosa sifa au baada ya tcu kukupangia.

Physics ndio msingi wa sayansi na engineering.

Mtu uliyesoma phy natarajia kichwa chako kiwe chepesi kuangalia mambo kwenye jamii!!

Kwenye phy huko mmesoma kozi za programming, yan unashindwa hata kutumia programming kutengeneza mfumo wa kutatua matatizo yetu?

Mkuu acha uzembe miaka inasonga!
 
Back
Top Bottom