Kozi gani umesoma ambayo huwezi kumshauri mtu mwingine aisome?

Mdogo wangu mimi hapa kaka ako ni Procurement Cordinator kwenye shirika flani la Kimataifa(INGO) Nakushauri life is too short. Nimepiga Public Admin, nikaja nikaweka na PGD ya procurement. Salary za kwenye NGOs zinajulikana. Ila kwa mwezi kwenye michakato ya hapa kule hapa kule naweka mpaka 45milion kwenye accounts. Jiongeze.
Kaka naomba intern hapo
 
Nimesomea Masters in Atomic Engineering nje ya nchi kule Pakistani.
Binafsi nina ujuzi wa kutengeneza mpaka mabomu ya atomic na nishati ya atomic ila nipo kitaa nimetulia napiga udalali ,kupata kazi labda niende Marekani au Iran.

Nangoja siku Tanzania tutakapoanza tengeneza umeme wa uranium hapo ndio utaona Magufuli au rais ajaye ananipigia sim moja kwa moja nakula kitengo cha mabomu na umeme.

Wenye ujuzi huu kwa Tanzania tupo wawili tu mm na jamaa yangu na wote tupo kitaa hatuna habari .
Kaz unayo tayar bro tengeneza bomu kipind hichi siku ya kura unaliset sehem alaf una demand kaz unatoa deadline..
 
Hello wana JF .

Unakuta umesoma kozi ambazo either ulijikuta tu comby imebalance au kwa kua zilikua na priority ya mkopo lakini hazikua chaguo lako.

Baada ya kuhitimu ukaingia kitaa ukakuta things on the ground are not as you thought. Kozi uliosoma haina market.

Please share your experience about life after college.

Sent using Jamii Forums mobile app
community health
 
Take Om ni Tshs 587000 mkuu
Alikwambia anadaiwa na Bodi ha mkopo
Bachelor of Science in Mathematics.

Hata chuo kilikua na mpango wakuimodoa hii kozi, sijui kama bado ipo kama ilivokua.

Aliyekuja kunikagua field alikua honest, "nakushauri kama kijana mwenye ndoto, ili usipate shida kwenye career yako, lazima field yako uichanganye na either uchumi, takwimu au finance", alinishauri. Hayo alishauri niyafanye kwa masters maana it was too late kwa bachelor.

Asante Dr. ____, ulinipa A ukanitoa kimasomaso ila huku mtaani mi ni bwege tu kama mabwege wengine. Familia duni sikuweza kusoma masters. Sijawahi ona kazi inamtaka Mathematician.

Nimedandia kazi nyingi sana za watu. Nimeshafundisha mpaka shule ya msingi(teh teh).

Mkuu wa department alisemaga one of the most paying job in America is being Mathematician. Sasa nimejiandaa kumpigia kura Hashim Rungwe kama sio Gwajima(Jimboni), nadhani ule mpango wenye umarekani unaweza badilisha maisha yangu.

Nikimaliza CPA naweza nikadandia kazi za wahasibu. Nikikwama hapo basi 2022 nitafungua kanisa. Samahani ninaexplore option zote, sitaki kufa nikiwa fukara.

Af kuna mtu kanambia nikisoma postgraduate education ntaajiriwa kama mwalimu halmashauri, nitalipwa laki saba na kumi na sita (716,000/=)
Take home 467,000/= Mbona nayo maisha tuu..
 
Biomedical ni Upepo unapita soon, Kwa wanaofatilia trending 2007 watakumbuka upepo wa Computer science na Telecommunications mpaka kufikia Mahali COET ikawa ili uwe enrolled Telecom basi uwe na High Cut off points na Kampuni za Mawasiliano zilikuwa zinaopoa Wanafunzi wa mwaka wa nne chuo na kuwapa kazi kabisa Leo iko wapi telecom? Arusha Technical wenyewe Intake ya kwanza almost wote walipewa offer watachukuliwa ila kwa sasa mfano wa diploma tu wanasota kitaa, Mtu anaetaka kusoma engineering yoyote asome Core courses kama Electrical,Mechanical au Civil, Electrical engineering akienda training anapiga mzigo full wa biomedical na Telecom, Civil same nae anaweza kufanya Highway au irrigation na Mecha nae anaweza kupiga Automotive, Auto electric basi wadogo zangu msiendeshwe na hisia
Umesema kwel kabsa kiongozi
 
Upo sahihi kabisa soma kama unapenda ila usifikilie kuishi maisha bora na kupata maendeleo kwa mshahara wa laki 8 kwa mwezi.
 
Advocates ni social science mkuu?
Kozi karibu zote za social science (angalau advocates kidogo) ni chenga na za Biashara (angalau CPA s)
Kozi nzuri ni hizi
Za afya zote
Uhandisi wote
Land savey, wasanifu majengo,

Veternary
 
Back
Top Bottom