Kova umebebeshwa mzigo... huna jinsi!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,575
8,595
Kutokana na Taarifa iliyotolewa na Polisi na Kusomwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Ndg,Suleiman Kova,Inaonyesha hiyo taarifa inajitenga na ukweli! kitu hicho kilichomfanya Msomaji kubabaika na kuwa na hali ya sintojua na kutojiamini!, kwakuwa Msomaji alifahamu fika kuwa anachowaeleza wananchi siyo!! na kwakuwa yeye ndiye anapaswa kufanya hivyo basi hana budi!!Kwani ndilo jukumu lake!!!....Kwa taarifa ile hata kama siyo mtaalamu wa maswala ya saiklojia unaweza kumsoma mtu uso wake!, na ukamsoma anawaza nini! kwakuwa anaanza kuongea na sauti ikichelewa kutoka!! hiyo ni dalili dhahiri kuwa hiki nacho kiongea si sahihi!......hii ni kutokuwa na imani kwakitu anachokuwa akifanya kwa wakati ule!!......Ila na sema Watanzania hawajafikia mahali hapo siku hizi watanzania wengi niwajuzi na niwataalamu wakusoma taarifa za kiinterejensia!!!

Ila na kupa pole kwa twishwa zigo zito......!!
 
Yani kwajinsi alivyokuwa akieleza.....ahiitaji msomi kuele kwamba kinachoelezwa ni uongo!!!Kwana mtu anaongea jambo ambalo ni very sensitive unaongea kama upo kwenye mkutano wa Polisi jamii!! zaleo niliandika Huu uzi kuhusiana na kutojiamini kwa kova wakati anaongea...kumbe na wewe uliliona hili ndiyo maana nilisema haiitaji mtu aliye bobea kwenye mambo saiklojia!!
 
Last edited by a moderator:
Kakakiiza, Kova kaumwa tu kuleta cooked story. Watakachokifanya ni kupiga danadana na kisha kumtamkia KIFUNGO CHA MAISHA halafu hadithi inaishia hapo, atatolewa kimyaaaaa na kwenda kuendeleza usanii mitaani. Hawa jamaa na wafanye maigizo yao wapendavyo, lakini watanzania tulishajua tangu mwanzo anayehusika ni serikali ikitumia vyombo vyake vya maguvu. PERIOD! Jifurahisheni tu, ipo siku kila mtu ataanikwa kwa kadiri ya mchango wake. Tanzania is becoming Russia nowadays.
 
Ni jambo la kutia aibu kwa vyombo vyetu vya dola na taifa kwa ujumla kutangaza jambo ambalo hata mtoto mdogo anajua kuwa ni habari iliyopikwa ili kuuhadaa umma. Mtu huyo anayejiita mtesaji wa Dr. Uli alikwenda kanisa la ufufuo kutubu, lakini kwa maelezo yake tu wale wachungaji walitambua kuwa ni mwongo. Na kwa kuwa wanajua kanisani sio mahali pa kuchezea maigizo ya serikali na vyombo vyake vya dola, wakapiga simu polisi waje wachukue uchafu wao. Cha kushangaza Kova anatangaza eti alikuwa anatubu kanisani, hayo ni maigizo takataka!

Polisi kama kweli walikuwa wanataka kumtafuta mtesaji wa Ulimboka, wangeanza na Abeid ajulikane ni nani na alitumwa na nani kumuhoji Dr. Uli? Na baada ya dr kutekwa yeye Abeid ilichukua hatua gani kuokoa maisha ya mdau wake aliyetekwa?

Polisi acheni maigizo. Zama hizi hakuna mtu wa kumdanganya kama mlivyozoe zama hizo! Tutafutieni Abeid kwanza ndipo mlete maigizo yenu hapa!
 
Kakakiiza, Kova kaumwa tu kuleta cooked story. Watakachokifanya ni kupiga danadana na kisha kumtamkia KIFUNGO CHA MAISHA halafu hadithi inaishia hapo, atatolewa kimyaaaaa na kwenda kuendeleza usanii mitaani. Hawa jamaa na wafanye maigizo yao wapendavyo, lakini watanzania tulishajua tangu mwanzo anayehusika ni serikali ikitumia vyombo vyake vya maguvu. PERIOD! Jifurahisheni tu, ipo siku kila mtu ataanikwa kwa kadiri ya mchango wake. Tanzania is becoming Russia nowadays.

Sidhani kama picha itaendelea salama, pona pona yao iwe Gwajima hujishughulisha na biashara mbaya nyuma ya pazia, kinyume chake Gwajima atayakemea hayo mapepo hadharani, hapo ndipo serikali itabaki uchi wa mnyama!
 
Sidhani kama picha itaendelea
salama, pona pona yao iwe Gwajima hujishughulisha na biashara mbaya
nyuma ya pazia, kinyume chake Gwajima atayakemea hayo mapepo hadharani,
hapo ndipo serikali itabaki uchi wa mnyama!

Ya wakamwangukie gwajima, au la wampoteze! La sivyo anawamliza!
 
Mimi mpaka naogopa!!!Kuna kila dalili kuwa siku moja hii nchi itaingia kwenye machafuko na vita vya wenyewe kwa wenye!!Ila na muomba mungu hii apishie mbali!!
 
Tatizo hawa kina Kova, Msangi na wenzao walishafanya issue kama hizo huko nyuma...sasa wakaonekana ndio wataalamu wakapewa hii issue, lakini kwa bahati mbaya Uli kapona.. utata ukaanzia hapo.... utaalamu wa kubumba, wewe unategemea form IV failure wata come up na nini... yaani udwanzi mtupu... eti Nitaunda timu ya wataalamu wa upelelezi na hii issue itakuwa mtihani wao.... jamani yaani mpaka Gwajima saidie?? HATUDANGANYIKI!!!! Zigo la Chawa hilo.... acha limwashe... ona mimacho ilivyotoka.....
 
hivi hivo viapo walivyoapa vya kazi zao hawavikumbuki au walikuwa wanaigiza hata mtoto wa darasa la 5 ukimsomea hiyo tamthilia hataielewa, ee kweli tz imekuwa bongo movie. ndo hawa huwa wanakuwa ndani ya tume zinazoundwa? kichefuchefu tuu
 
gwajima atakuwa anahusika! na huenda akawa kwenye system! huo uchungaji ukawa kivuli tu! si tunayaona hata kwa james bond! na hii sinema wame copy na kupest kutokea hollywood wandugu!
 
shame on kamanda kova,
serikali mbona inajidhalilisha hivyo?
CCM mbona inajimaliza yenyewe!!!!
Kwanini serikali inapenda kuwakasilisha wananchi wake?
Kwa heri kova, kwa heri serikali ya kikwete, kwa heri CCM.
Kwa hili, nani atampenda kova? nani ataipenda serikali ya kikwete? nani ataipenda CCM?
 
Kakakiiza, Kova kaumwa tu kuleta cooked story. Watakachokifanya ni kupiga danadana na kisha kumtamkia KIFUNGO CHA MAISHA halafu hadithi inaishia hapo, atatolewa kimyaaaaa na kwenda kuendeleza usanii mitaani. Hawa jamaa na wafanye maigizo yao wapendavyo, lakini watanzania tulishajua tangu mwanzo anayehusika ni serikali ikitumia vyombo vyake vya maguvu. PERIOD! Jifurahisheni tu, ipo siku kila mtu ataanikwa kwa kadiri ya mchango wake. Tanzania is becoming Russia nowadays.

huko ulikofika siko, kimsingi hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na swala la ulimboka. Hayo ni maneno tu ya kulisafisha jeshi la polisi
 
Kwa nini polisi waamini moja kwa moja kwamba yeye ni mhalifu? Anaweza kuwa kichaa au anatala kutoa habari za uongo. Mtu huyo alitakiwa afanyiwe uchjunguzi wa kina kabla ya polisi kuja kutoa habari za kumkamata mtesaji wa Ulimboka. Je kwa kutoa hii ripoti uchinguzi umekwisha?

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
ni kweli kabisa CHIMUNGURU...kwa jinsi ninavyomjua bwana KOVA anavyokuwa na mbwembwe na tambo za kila aina when it comes to press release kwenye matukio ya uhalifu!!!jana hakuwa vile kabisaaaaaa yani alionekana wazi kabisa kapitishiwa report na kuambiwa kaitoe kwa umma...yani anajikanyaga mwanzo mwisho na kukosea kosea tu.
kama walitaka au kutaka report ya DR.ulimboka iwe true n fair kwanini walikataa kusiwe na Free enquiry commission?ktk akili ya kawaida wewe kama mshukiwa au mtuhumiwa huwezi kujichunguza mwenyewe kisha ukajitolea taarifa kwa umma na ukakuelewa.
na hilo suala la mkenya its just a planted guy and at the end of the day watakuja kumwacha huru kama wale waliouwa wafanyabiashara wa mahenge,au kumsafirisha kwao huyu mkenya na kwendakula raha kenya.
Hizi ni mbinu chafu chafu za intelligence primitive ya bongo.
 
Kova huyo mkenya amesharudisha zile gwanda na bunduki zote? Je mabwepande iko kenya au? Iko siku uongo utajitenga kova utajuta na kusaga meno ......
 
Back
Top Bottom