Kosea vyote lakini siyo mtu wa kuoa ama kuolewa naye

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
7,105
18,005
WanaJF - wakati mwingine ni vizuri kusema jambo linalokukwaza katika maisha kwa watu wengine - si kwa sababu utapata ufumbuzi, ila kwa sababu ukilisema kwa watu wengine inakupunguzia msongo wa mawazo na kichwa kuuma.

Kuna huyu mwenza wangu. Tuna watoto pamoja na tunakaa pamoja. Ni mume na mke. Mambo ya kawaida sana kama usafi wa nyumbani yanamshinda. Hawezi kabisa kujifunza, akabadilika. Miaka nenda rudi. Akiosha vyombo, ataacha mabaka ya chakula juu yake.

Siyo kwamba kuna tatizo la maji ama sabuni nyumbani - la hasha! Akienda kununua chakula, atanunua vitu kama matunda ya juma zima na yote ukiyaangalia, yako tayari kuliwa siku hiyo hiyo. Kwa sababu yamenunuliwa mengi kwa ajili ya juma zima, baada ya siku 2-3 hivi, yote yanaoza. Yakishaoza, atayakata hivyo hivyo na kuyaweka mezani kwa ajili ya kula. Ukishaweka mdomoni, ndio unapambana na ladha ya kitu kilichooza.

Hata watoto, ambao bado ni wadogo, tayari wanajua na kuepuka kitu kisichostahili kuliwa na binadamu lakini mama yao hawezi kabisa. Nimejaribu kumwelewesha lakini wapi. Kuna wakati ilibidi tuwe tunakwenda wote sokoni ili ajifunze baada ya mwaka mmoja nikamwacha awe anakwenda peke yake. Kwa sababu ya kazi, haiwezekani siku zote kwenda naye. Siku hizi nimemwacha afanye manunuzi mwenyewe. Lakini hakuna mabadiliko kabisa.

Hapa naongelea mwanamke mwenye elimu ya chuo kikuu lakini kwa sababu watoto bado ni wadogo, ni mama wa nyumbani kwa sasa. Hata kama haukwenda shule, je, kweli ni vigumu kujua kuwa haya mananasi/mapapai niliyonunua kwa ajili ya kutumia kwa siku 7 kwa hali yake ya kuiva hayawezi kukaa siku 7? Kama kuna umuhimu wa kununua ya juma zima basi nichanganye yaliyoiva na magumu? Yaliyoiva ya kula leo na kesho na magumu ya kula baadae?

Vijana wa sasa - kosea kitu kingine lakini usikosee kuchagua mwenza wa maisha ambaye unaapa kukaa naye hadi kifo kiwatenganishe. Ukikosea, utakufa kabla ya wakati wako. Tafadhali zingatieni hili. Waingereza wanasema, "to be forewarned is to be forearmed".
 
Samahani kaka.. ukweli sijaoa ila kama makosa ni hayo tu. Sioni sababu ya wewe kulalamika hapa hayo ni makosa ya kawaida tu na yanavumilika sana na ukiamua unaweza mrekebisha...
Nilifikili mkeo anakiburi, Mgomvi, Malaya au tambia zinazogusa hisia moja kwa moja. Ila tutafata ushauri wako
 
To be forewarned is to be forearmed.
 
Yaani sio siri,.kuna vitu ukivisikia hadi masikio yanawasha kwa hasira,.hivi inakuwaje hivyo jamanii ni sifa,ujinga,kudeka,kukomoa,kutojali ama ni nini?? Aisee hapana kuna viumbe vinahitaji msaada tena si wa kimwili bali wa kiroho,.binadamu uliyekamilika kiakili huwezi fanya vitu vya namna hii...kuna shida mahali,.narudia tena shida ya kiroho wala si ya kimwili....
 
Kwakweli c kwa hali hiyoo jmn. Ni uvivu au nikitu gani? Au mtoto wa kishua.
Hawa ndio wale wanaolewa for show off lakin hawataki kuhudumia mume.

D hata kama umezaliwa familia ya kifalme kuna vitu huwezi fanya bwanaa,.ina maana hata kuchambishwa uchambishwe eti kisa wa kishua??hapana nakataa...ni pepo tuu hilo sio bure...shenzi kabisaa
 
Samahani kaka.. ukweli sijaoa ila kama makosa ni hayo tu. Sioni sababu ya wewe kulalamika hapa hayo ni makosa ya kawaida tu na yanavumilika sana na ukiamua unaweza mrekebisha...
Nilifikili mkeo anakiburi, Mgomvi, Malaya au tambia zinazogusa hisia moja kwa moja. Ila tutafata ushauri waambiako
Acha masihara basiii mtu ana kwambia amesha kwenda nae sokoni kwa muda wa mwaka mzee ", dhumuni kuu likiwa nikumbadilisha ..lakini tangu aanze kwenda peke yake (mwanamke), anarejea kufanya yale yale aliyoambiwa kuwa hayafai ... then wewe unadai kuwa amvumilie atabadilika "... Mimi namshauri amvumilie tu ..lakini suala la mabadiliko asahau
 
Kabla ya kufikia hatua ya kua na watoto alikuaje??? Huyo mkeo ana hulka ya ujinga na uchafu, huwez mlisha mumeo kitu kilichooza bwana mpunguzie hela anunue vitu kwa kiasi labda itasaidia
Ndoa ya Kikristo inasema ukishaoa, mpaka kifo - uwe ama usiwe na watoto.
 
Back
Top Bottom