Kosa langu liko wapi, wakati uzembe umafanya mwenyewe?

lazima ukae

JF-Expert Member
May 15, 2013
788
380
Nina mpenzi wangu ambae tuna miezi mitatu toka tuanzishe uhusiano wetu mimi nampenda na yeye nina imani ananipenda ingawa sina uhakika kama na yeye ananipenda kwa kiwango kilekile ninachompenda mimi mana sina uwezo wa kuufungua moyo wake na kungalia ananipenda kwa kiasi gani.

Kwa kipindi chote hicho cha takribani miezi mitatu tumekua na maelewano mazuri na mpenzi wangu ingawa kuna kule kupishana maneno mara chachechache ambapo ni jambo la kawaida kutokea kwenye mahusiano mana hata vikombe tu kabatini hugongana.

Jana mida ya jioni alinipigia simu kwamba anashida na kiasi fulani cha pesa hivyo anaomba nimsaidie, kwakua nilikua safarini toka mkoani nikamwambia asubiri kama lisaa limoja nitakua nishafika mjini na nitamtumia hicho kiasi cha pesa mana kipo ndani ya uwezo wangu.

Nilivyofika mjini haraka sana nikamtumia hiyo pesa kupitia mitandao ya simu na akanijulisha kuwa ameipata na anashukuru sana baaada ya kupita kama lisaa limoja akanipigia simu kwamba ameenda kwa wakala lakini kwa bahati mbaya amekosea namba ya wakala hivyo pesa imeenda kwa wakala mwingnine na hawezi kuipata siku hiyohiyo hivyo anaomba nimtumie pesa nyingine ikibidi nikope hata kwa mtu kitu ambacho sikukubaliana nacho mana yeye ndo amefanya uzembe na siwezi kujiingiza kwenye madeni yasiyokua na ulazima.

Hivi ninavyoongea toka jana kanichunia na mimi nimekaa zangu kimya na nishaamua kama akiendelea kukaa kimya basi na mapenzi yenyewe yafe tu huenda haikua ridhiki mana najua tu atakua amenikasirikia kwa kosa ambalo sio langu.

Je hapa mimi nina kosa waungwana ?
 
Hahahahaha hiyo ilinitokeaaa enzi hizo nina mpenzi wangu yupo Kenya saa akawa kanitumiaa ela si nikawa nimekoseaa namba nikamwambiaa nimekosea namba alichonijibu ni kuwa Ok ur not serious baada yaa hapo nilikulaa block kilaa konaa ili nisimsumbuee alakuja kuongea na mm baada ya kirudi nchini .

Hujakosea huyo msichana wako anakuchoraa tu na am sure hakukoseaaa piaa ila aliplan kufanya hivyo so take care akiona umuhimu wako atakufatuta sisi wasichana ndivyo tulivyo
 
Kaka shituka,hiyo ni chuma ulete.Mapenzi yenu yako mfukoni kwako,mfuko ukikauka hayapo.Kwa mtu anayethamini msaada uliompa hata asingekupa huo mrejesho kuwa pesa imeenda kwingine,Kwa kuwa ingekushitua kuwa anakutumia tu kujinufaisha.
Halafu,hivi wewe hushituki kwa msisitizo alioweka kuwa ukakope umpe tena.?
 
Hamna sehemu ambayo watu hua makini kama kwenye miamala, mkuu uyu mtu anakutumia...
Kama kavunga,nawe vunga...
Tatizo mnawazoesha wenyewe, inaweza hata alivyokuambia ukope, alikukaripia.
Au achana nae tu, asikupelekeshe.
 
Ndo ushakua ATM machine....
Kaz kwako kuchagua uwe ya Benki Gan
CRDB, NMB, STANBIK AU????
 
Hapo unapigwa tu pesa bro hakuna mapenzi na wala hajakosea usikute hela unayomtumia nayeye kuna lijamaa analitumia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom