Kosa langu liko wapi hapa?

Kosa langu liko wapi hapa?

Achana naye huyo, yupo kimaslahi zaidi. Mambo yake yakinyooka atarudi tu kwa huyo mzazi mwenzake.
 
Yupo na wewe kutimiza mahitaji yake. Akili za kuambiwa unatakiwa uchanganye na zako, si kila anayekwambia anakupenda na akakuvulia pichu basi ujibweteke na kuamini anakupenda. Chukulia hayo mahusiano kama funzo usije fanya makosa mbeleni.

Achana naye, kusema uongo hata kwa Mungu ni kosa kubwa sana. Na kwa msg ya jamaa yake jinsi ilivyo inaonesha anampenda sana na ana wivu sana, ukichelewa unaweza kuweka roho yako rehani. Kutenda kosa sio kosa, kosa.......!
 
Fikiri wamekutana mwezi uliopita leo wanaishi kama mke na mme.... Hii ni shidaaaaaaaaaa, huyu binti alitaka hifadhi kwa malipo ya ngono haya mengine yanatokea bila kukusudiwa.
Na sidhani km walipima
 
Nikiwa mkoa flani hivi kibiashara mwanzoni mwa mwezi uliopita nikakutana na mdada mmoja ambaye alikuja kuanza kazi kama mwalimu wa secondary {hawa walioajiriwa juzijuzi}. Katika kuzoeana tukajikuta tumeanza mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa tuko pamoja na tunaishi pamoja, ukizingatia kipindi hicho ndo anakuja kuanza kazi hakuna mshahara wala pesa ya kujikimu ikabidi nimpe hifadhi.

Kiumri nina 31 yrs yeye ana 25 yrs kwa kipindi hiki kifupi tunaishi vizuri hapa kijijini mpaka watu wanajua ni wanandoa.Jana nikiwa nmetoka kazini yeye yuko nje anafua kuna sms iliingia kwenye simu yake nikatamani nijue ni nani nikaifungua nikakuta ujumbe huu " hellow my wife nimekumiss sana kipenzi changu leo ndo nimerudi toka safari kama nilivyokuahidi kesho naenda kwenu kupeleka nguo za mtoto na matumizi.

Naomba mke wangu ujichunge najua umepangiwa kufundisha mkoa mwingine lakini isiwe sababu ya kuisariti ndoa yetu nakupenda pia nampenda mtoto wetu."Sio siri nlishtuka sana kwani binti huyu hakuwahi kusema kama ameolewa japo alishanieleza ana mtoto. Basi nikamuita na kumwonyesha sms hiyo alikiri kuwa ameolewa na ana mtoto mmoja japo alipokuja kuanza kazi mtoto alimpeleka kwao kwani mmewe anafanya biashara za kusafiri.

Nikamuuliza lengo la kunificha kama ameolewa akaanza kulia na kusema alishindwa kunipa ukweli alijua ningemwacha wakati yeye pia ametokea kunipenda na anaenjoy mapenzi nnayompa! Pia akasema hawakuwahi kufunga ndoa ingawa walioana baada ya binti kupata mimba akiwa chuo na jamaa kujitambulisha kwao na kuanza kumsaidia binti kimasomo. Pia anasema kipindi chote cha ndoa yao hakuna amani kama anayoipata kwangu na akaahidi yuko tayari kuachana na mmewe ili aishi kwa furaha na mimi.

Wadau niko njia panda kwani katika maisha yangu sikuwahi kufikilia kuwa na mke wa mtu achilia mbali kuishi nae! Nampenda sana kwani tunaishi kwa amani na sijaona kasoro yoyote kitabia ananijali na kuniheshimu. Lakini katika hili la mmewe nafsi inanisuta! Nafikiria kumwacha mapema kabla mmewe hajapata taarifa ili nisihatarishe maisha yangu.
Je nitakuwa na kosa katika hili?

Kwa wale wazee wa matusi tafadhali msinichafulie uzi wangu sio lazima ucoment pumba,busara inahitajika zaidi.

hebu soma hapo kwenye red...then uandike upya...no wonder unakurupukia mahusiano
 
Kama wanawake wameisha kiasi kwamba ni lazima uwe na huyo go on
 
Pole sana Mbwa dume

Kuna vitu kadhaa nilivyoviona;

1. Uharaka: Sijui kwa wengine, lakini binafsi uliposema mmekutana mwezi uliopita(Mei) mwanzoni na sasa hivi ni mwezi wa sita mwanzoni, ninadhani hapa umeharakisha mahusiano hata kama unampenda kiasi gani, esp. kwa dunia ya sasa!

2. Uhitaji: Either you are too desperate or too easy going! Sidhani hata kama ndani ya mwezi unaweza kuishi na mwanamke kama me na mke(as you said, hata kijijini wanajua nyie mmeoana.

3.Upofu: 'They say curiosity killed the cat' huko kuchunguza chunguza kwa simu yake ndiyo kumeleta haya. Sasa nashindwa kuelewa unaposema 'hana kasoro' ..Believe me everyone has, tunavumiliana tu! Kama huzioni it was not high time for you kuingia katika mahusiano.

Pili, kasoro ndiyo hizo umetambua uongo(kuficha ukweli), uaminifu haupo pia.

Uamuzi mgumu: Ninadhani binti/mwanamke/dada huyo amefanya out of desperation(Ulimpa hifadhi hukuwa na nia yeyote nyingine), ilibidi akubali, na alijua kuishi pamoja kunaweza kupelekea huko(mahusiano) na ndiyo maana hakukueleza wazi kuhusu baba wa mtoto wake! Pili Baba wa mtoto wake amemueleza amefikia wapi?

Then, kama 'fadhila' ya kumhifadhi ndiyo ikapelekea mahusiano nothing else.

Stand to be corrected,
-Dont rush into things.
-Usimuamini mtu yeyote kirahisi rahisi.
-Mueleze wazi kuwa huhitaji maendeleo yoyote ya mahusiano yenu, ila sishawishiki kumhifadhi mke wa mtu mliyekutana tu huko hata kama ana shida gani aisee.
 
Last edited by a moderator:
Unataka ushauri gani wakati jibu unalo?achana na mke wa MTU..jenga utu ktk moto wako.
 
Nikiwa mkoa flani hivi kibiashara mwanzoni mwa mwezi uliopita nikakutana na mdada mmoja ambaye alikuja kuanza kazi kama mwalimu wa secondary {hawa walioajiriwa juzijuzi}. Katika kuzoeana tukajikuta tumeanza mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa tuko pamoja na tunaishi pamoja, ukizingatia kipindi hicho ndo anakuja kuanza kazi hakuna mshahara wala pesa ya kujikimu ikabidi nimpe hifadhi.

Kiumri nina 31 yrs yeye ana 25 yrs kwa kipindi hiki kifupi tunaishi vizuri hapa kijijini mpaka watu wanajua ni wanandoa.Jana nikiwa nmetoka kazini yeye yuko nje anafua kuna sms iliingia kwenye simu yake nikatamani nijue ni nani nikaifungua nikakuta ujumbe huu " hellow my wife nimekumiss sana kipenzi changu leo ndo nimerudi toka safari kama nilivyokuahidi kesho naenda kwenu kupeleka nguo za mtoto na matumizi.

Naomba mke wangu ujichunge najua umepangiwa kufundisha mkoa mwingine lakini isiwe sababu ya kuisariti ndoa yetu nakupenda pia nampenda mtoto wetu."Sio siri nlishtuka sana kwani binti huyu hakuwahi kusema kama ameolewa japo alishanieleza ana mtoto. Basi nikamuita na kumwonyesha sms hiyo alikiri kuwa ameolewa na ana mtoto mmoja japo alipokuja kuanza kazi mtoto alimpeleka kwao kwani mmewe anafanya biashara za kusafiri.

Nikamuuliza lengo la kunificha kama ameolewa akaanza kulia na kusema alishindwa kunipa ukweli alijua ningemwacha wakati yeye pia ametokea kunipenda na anaenjoy mapenzi nnayompa! Pia akasema hawakuwahi kufunga ndoa ingawa walioana baada ya binti kupata mimba akiwa chuo na jamaa kujitambulisha kwao na kuanza kumsaidia binti kimasomo. Pia anasema kipindi chote cha ndoa yao hakuna amani kama anayoipata kwangu na akaahidi yuko tayari kuachana na mmewe ili aishi kwa furaha na mimi.

Wadau niko njia panda kwani katika maisha yangu sikuwahi kufikilia kuwa na mke wa mtu achilia mbali kuishi nae! Nampenda sana kwani tunaishi kwa amani na sijaona kasoro yoyote kitabia ananijali na kuniheshimu. Lakini katika hili la mmewe nafsi inanisuta! Nafikiria kumwacha mapema kabla mmewe hajapata taarifa ili nisihatarishe maisha yangu.
Je nitakuwa na kosa katika hili?

Kwa wale wazee wa matusi tafadhali msinichafulie uzi wangu sio lazima ucoment pumba,busara inahitajika zaidi.

Kuwa msiri na muongo ni tabia

anyway alifanya hivyo asikukose maana kakupenda.... so kama unampenda pia usimwache hata kama sijui ni mke mtu au ana mtoto tayari maana "LOVE IS ABSENT OF JUDGMENT"
 
Kosa lako ni kudandia mwanamke usiyemjua na kumuweka ndani na kuishi pamoja bila kumchunguza.........hivyo basi jiandae kuliwa 0713 ili liwe fundisho kwako next time usirudie Mkuu.
 
Sasa sijui hata afya zenu mlicheki au la,? Majanga.
 
Soma alama za nyakati si ajabu huyo ndo mauti wako Some tym uwe unafuatilia mambo ya nyota yatakusaidia kujua ukoje kama hujajisoma vizuri
 
Be careful kijana kuishi na mke wa mtu ni risk sana bora uachane nae maana mshikaji akigundua atakufanyia kitu mbaya kwa gharama yoyote ile
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom