Kosa langu liko wapi hapa?

Kosa langu liko wapi hapa?

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
6,286
Reaction score
10,944
Nikiwa mkoa flani hivi kibiashara mwanzoni mwa mwezi uliopita nikakutana na mdada mmoja ambaye alikuja kuanza kazi kama mwalimu wa secondary {hawa walioajiriwa juzijuzi}. Katika kuzoeana tukajikuta tumeanza mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa tuko pamoja na tunaishi pamoja, ukizingatia kipindi hicho ndo anakuja kuanza kazi hakuna mshahara wala pesa ya kujikimu ikabidi nimpe hifadhi.

Kiumri nina 31 yrs yeye ana 25 yrs kwa kipindi hiki kifupi tunaishi vizuri hapa kijijini mpaka watu wanajua ni wanandoa.Jana nikiwa nmetoka kazini yeye yuko nje anafua kuna sms iliingia kwenye simu yake nikatamani nijue ni nani nikaifungua nikakuta ujumbe huu " hellow my wife nimekumiss sana kipenzi changu leo ndo nimerudi toka safari kama nilivyokuahidi kesho naenda kwenu kupeleka nguo za mtoto na matumizi.

Naomba mke wangu ujichunge najua umepangiwa kufundisha mkoa mwingine lakini isiwe sababu ya kuisariti ndoa yetu nakupenda pia nampenda mtoto wetu."Sio siri nlishtuka sana kwani binti huyu hakuwahi kusema kama ameolewa japo alishanieleza ana mtoto. Basi nikamuita na kumwonyesha sms hiyo alikiri kuwa ameolewa na ana mtoto mmoja japo alipokuja kuanza kazi mtoto alimpeleka kwao kwani mmewe anafanya biashara za kusafiri.

Nikamuuliza lengo la kunificha kama ameolewa akaanza kulia na kusema alishindwa kunipa ukweli alijua ningemwacha wakati yeye pia ametokea kunipenda na anaenjoy mapenzi nnayompa! Pia akasema hawakuwahi kufunga ndoa ingawa wanaishi pamoja, baada ya binti kupata mimba akiwa chuo na jamaa kujitambulisha kwao na kuanza kumsaidia binti kimasomo. Pia anasema kipindi chote cha ndoa yao hakuna amani kama anayoipata kwangu na akaahidi yuko tayari kuachana na mmewe ili aishi kwa furaha na mimi.

Wadau niko njia panda kwani katika maisha yangu sikuwahi kufikilia kuwa na mke wa mtu achilia mbali kuishi nae! Nampenda sana kwani tunaishi kwa amani na sijaona kasoro yoyote kitabia ananijali na kuniheshimu. Lakini katika hili la mmewe nafsi inanisuta! Nafikiria kumwacha mapema kabla mmewe hajapata taarifa ili nisihatarishe maisha yangu.
Je nitakuwa na kosa katika hili?

Kwa wale wazee wa matusi tafadhali msinichafulie uzi wangu sio lazima ucoment pumba,busara inahitajika zaidi.
 
Ungekua una nia ya kumuacha usingekuja huku
huku unatafuta baraka au nini ??

hivi unajua matumizi ya ky jelly ??
ngoja mwenyewe agundue
 
Kosa lako wewe ni mbea na tapeli.

swissme
 
Wewe umeona sms ya mr kwa mrs wake. na huyo mwalimu alifanya hayo ili umsaidie maisha maana hakuna na pesa. sasa bado wangangania ngoja waje wakufire ndo utajua!!!!!! mbona unjihami matusi utatukanwa kwa vile umeonesha utaahira kutojua la kufanya mpaka ufumaniwe!!! mpuzi wewe
 
ungekua una nia ya kumuacha usingekuja huku
huku unatafuta baraka au nini ??

hivi unajua matumizi ya ky jelly ??
ngoja mwenyewe agundue

Loh hufai wewe
 
Mke wa mtu sumu mkuu au unataka mpaka uliwe 0713....?
 
Kosa lako ni kutongoza mwanamke siku moja, kukubaliwa siku moja na kuamua kumhamishia kwako siku moja! Yaani ndani ya mwezi mmoja umeshafanya yote hayo, maana hawa walimu wapya hawana hata miezi miwili......UKIMWI unakunyemelea
 
ungekua una nia ya kumuacha usingekuja huku
huku unatafuta baraka au nini ??

hivi unajua matumizi ya ky jelly ??
ngoja mwenyewe agundue

Wazee wenzangu wamatusi leo tupumzke,,,,Kiongozi pole sana,Sasa fikiria kwa undani maumivu ya kuliwa kibogo au kuchinjwa kama IS....ACHANA NAE Tafuta mwingine huu ugomvi mkubwa sana mwenyew akijua mziki utaupata
 
Achana nae jamaa akija ghafla kumtembelea akapata stori zako,hutajua atakachofanya.Tafuta mtu asiye na mme,,,,,,mke wa mutu sumu man,jikaze kiume na umuache, wanawake wanatabia ya kuanza penzi jipya na kujisahaulisha ya familia yake ila ikitokea jamaa kamfuma anakumwaga wewe jumla hatakutetea hata kidogo mkuu.
 
Muache mke wa mwenzio, tena mwambie awe mkweli siku nyingine maana anaweza sababisha mauaji yasiyotarajiwa.
 
Mbona hujishangai hata wewe??????????? mmekutana mwezi jana leo mnaishi pika pakua.... Si ajabu na mwezio nao alifanyiwa hivyo hivyo....... Endelea kulea ili nawe ujiopolee kajitoto.
 
Muache mke wa mwenzio, tena mwambie awe mkweli siku nyingine maana anaweza sababisha mauaji yasiyotarajiwa.
Fikiri wamekutana mwezi uliopita leo wanaishi kama mke na mme.... Hii ni shidaaaaaaaaaa, huyu binti alitaka hifadhi kwa malipo ya ngono haya mengine yanatokea bila kukusudiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom