Kosa la ponda ni lipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa la ponda ni lipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabieWana, Oct 26, 2012.

 1. B

  BabieWana Senior Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu inaenda pabaya kwani waislam wanaona kama wanaonewa na serikali hii, lakini wakristo wamekuwa wanashabikia na kua upande wa serikali kufurahia madhila yanayo wapata waislam. hakuna mkristo aliyewahi kuona kuwa hapa serikali haijatenda haki kwa waislam. hiki ndio kitu kibaya kuliko vyote?

  Suala la ponda liko hivi

  1. amehisishwa na kesi ya kuchoma makanisa, kitu ambacho si kweli waliochoma makanisa walikamatwa na kesi yao inaendelea, alichosema ponda waachiwe waliokamatwa kwa hoja alizozitoa kama muislam

  2. Kosa alilokamatiwa ni UVAMIZI wa eneo la mtu hapo chang'ombe hili ndo kosa lake akiwa na watu 36 wengine
  kwanini unakua uonevu? suala la kiwanja kuvamiwa halihitaji waziri wa mambo ya ndani aite wanahabari kuwaambia uovu huo, hili ni suala la mdai (anayedaiwa mwenye kiwanja), polisi na wavamizi kwanini kiwanja hiki kinatetewa kwa nguvu zote? waziri amepewa kitu kidogo au anafurahia kiwanja hicho kuuzwa ili waislam wakose

  3 KIWANJA NI MALI YA WAISLAM walichorithi iliyokua jumuia ya afrika mashariki ya waislam, sasa kinaangaliwa na bakwata. Bakwata wameshindwa kuiendeleza matokeo yake wanataka kukiuza ili wajipatie fedha wale wao kwa manufaa yao na si waislam.
  kiwanja hiki aliuziwa manji miaka ya nyuma, waislam wakishirikiana na imam wa masjid mtoro walipiga kelele manji akashindwa kukichukua, sasa kimeuzwa tena na aliyenunua kiwanja alianza kujenga, walioweza kina ponda walienda kukizuia wakavamia na kujenga msikiti wa muda ndipo alipokamatwa


  Dhulma inaandaliwa ili kuwakandamiza waislam, imeunganishwa na kesi ya UAMSHO ili ionekane nchi iko kwenye hali ya hatari wakati si kweli, Ya mbagala yalipita watu wakachukuliwa hatua leo kuja kumkamata ponda halafu useme wewe kwa sababu fujo ilifanyika mbagala unakosa, ulikataa sensa unakosa, huu ni uhuni.

  nchi imetulia ila yanajengwa mazingira kuonyesha nchi iko kwenye hali ya hatari waislam wakandamizwe mbaya christian your happy, Lakini mambo yakiharibika yataharibika kwa wote

  Waislam tuzidishe dua katika kipindi hiki kigumu na ALLAH(S.W) atadhihirisha haki inshalah
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hujui makosa yake?? kamuulize afande Kova.
   
 3. a

  adolay JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Ukiwa mtenda mabaya kila siku utasema unaonewa

  ukiwa mtenda mabaya huko unakokwenda pia ni wabaya

  Ukiwa na roho mbaya ee kweli tutakuogopa

  kweli walimwengu hawa wema mola awape ninii eee.... (Ramadhani Mtoro Remi ongala)
   
 4. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  1.Umewahi kujiuliza ni kwanini amekuwa akiishi maisha ya kukimbia na kuvipiga chenga vyombo vya dola??

  2.Umewahi kujiuliza kwanini hajawahi kuonyesha hadharani familia yake au hata ndugu zake wa kuzaliwa tumbo moja??

  3. Kama ni mtu safi asiye na hila, kwanini akwepane na polisi??
   
 5. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mbona makosa ya Ponda umeyataja?. Halafu unauliza kosa la Ponda!. Mwenzio Ponda jana pale mahabusu alinyolewa ndevu kwa msumeno wa Afande Kova, hadi akasema yeye ana undugu na Lipumba!. Ndipo walipomsamehe!.
   
 6. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha dhulma wala nini, waislam mnajikandamiza wenyewe kwa kukosa maarifa...wenzenu wanazidi kununa maeno makubwamakubwa nyinyi hata msikiti tu maishia kuugombea mpaka kupelekea watu kukatana masikio na kulipuana mabomu. Dhulma mnajitengenezea wenyewe kwa kukosa maarifa. Period.
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kawaulize wanaomshikiria!
   
 8. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Ponda ana mawakili wanaomtetea...kama una points (maana hapa sijaona points za kisheria zaidi ya kulalamika as usual) wapelekee mawakili wake. Tena kama hana kosa ina maana atashinda kesi, then afungue kesi ya madai dhidi ya serikali.
   
 9. b

  bantulile JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,439
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kesi iko mahakamani, unataka wana JF wawe mahakama! Si usubiri vyombo vyenye mamlaka ya kutafsiri sheria na kutoa haki vifanye kazi yake?
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  dua za waislam tayari zimesikika kwa mola wao: mashehe wawili-tunduru na arusha wako ICU
   
 11. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  ukichunguza kwa ndani zaidi, chanzo cha machafuko ni waislamu kugawanyika. hii inatokana na uongozi FISADI WA BAKWATA. for sure BAKWATA kimekuwa kisiasa zaidi na haitatui matarajio ya waislamu. LAZIMA BAKWATA IVUNJWE KWA MANUFAA YA WAISLAMU NA NCHI!!
   
 12. C

  Chiya Chibi JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umejichanganya kwel ndg yangu..! Tizama mada yako (kosa la Ponda ni lipi) na ulichokieleza ni kipi? Badilisha topic iwe: Hili ndo kosa la Ponda. Achen kulalamika bila hoja, Bakwata chombo chenu, aliyenunua kiwanja (Manji) Muislam mwenzenu, aliyemkamata Ponda (Kova) muislam mwenzenu, kiongoz wa nch ni muislam mwenzenu, Wakristo wanaingiaje hapo.?? Wachochez kama nyie ndo mnavuruga wenzenu misikitin badala ya kuwaelimisha watayamudu vp maisha na kufuata sheria za nchi, mnawachochea kwa hoja kama hzi kichwa chni miguu juu. Tafakarin sana, huu ndo muda wakuwekana sawa, 2015 akiingia mkristo Ikulu si ndo mtaisingizia serikal kila ki2 kibaya??
   
 13. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wewe usiyeona makosa ya baba yako Ponda hata ukielezwa hutaelewa. Kwani huoni wala usikie linapotamkwa jina la Ponda mhuni anayetumia uislam kujineemesha. Hujaona mashehe wanavyoshambuliwa na wahuni wenye mawazo mfu na mgando kama ya Ponda mwanangu? Kweli asiyejua maana haambiwi maana na akiambiwa maana hatajua maana kwa vile hajui kuwa hajui. Ponda na Farid ni viumbe wanaopaswa kuwa kuzimu by all means kwa vile nao wanataka kutuvuruga by all means. Ingawa hutaelewa ujumbe umefika. To hell Ponda and his opium.
   
 14. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Kosa la Kopa ni kwamba ni kafiri asiyejijuwa anachochea makafiri wenzake kufanyia fujo wapenda amani huku akijifanya yeye hausiki.
   
 15. K

  Kulya JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 339
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sheikh Ponda and his followers are accused of
  1. Committing conspiracy;
  2. Trespass;
  3. Criminal possession of property owned by Agritanza Limited at ChangÂ’ombe in Temeke municipality.
  4. Stealing of building materials from Agritanza limited including 1,500 bricks and 36 tonnes of aggregate and iron bars, all worth 59.6m/.
  5. Inciting people to commit offences (only Ponda's).

  Haya ndo makosa aliyopandishwa nayo Kisutu. Hayo manne ni pamoja wa wengine 49, na hilo la 5 ni peke yake.
   
 16. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  BabieWana; Nimependa jinsi ulivyoandika. Katika vitu vinavyoniuma japo si muislam ni jinsi kiwanja kizuri kilivyouzwa na kupeteza lengo kujenga chuo kikuu. Nimependa kwa kuwa unaonekana unaweza kuwa mvumilivu katika mijadala. Pamoja na mie kuumia, nisaidie ndugu yangu, Wakristo wamekosa nini na wanaingia wapi na vipi. Huenda mimi kuna nisichofahamu. Baadhi ya wakristo wamelia sana kuchomewa makanisa. Fedha na mali walizojinyima kwa miaka mingi zimeteketea. Labda hilo tumuachie Mungu kwani zilizochomwa ni Nyumba zake Mola. Atajuana nao yeye Mwenyewe.

  Ninaafiki kuwa huenda kuna tatizo, lakini naona kama njia zinazotumika kutatua siyo sahihi, unaweza kunisahihisha kama sipo sahihi. Ninaifahamu kiasi BAKWATA, Ni taasisi iliyosajiliwa. Nadhani ina wanachama au waasisi. Naona kama inawakilisha waislam sina hakika kama inawakilisha waislam wote. Wakristo pia wapo Katoliki, KKKT, Anglikana, TAG nk.

  Nisaidie wakristo wana makosa gani ili kama inawezekana tutafute njia za kiungwana za kutatua. Nimesoma jinsi ulivyoandika, ninaona kama una kitu unataka kusema, na ninahisia wewe unaweza kuwa mzuri katika kuleta umoja na mshikamano kwa kueleza yanayojiri na huenda tukakubaliana kwani tuna uwezo wa kutatua matatizo kistaarabu bila kuteketeza mali na kuleta maafa. NISAIDIE
   
 17. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Umemaliza mkuu. Asante.
   
 18. T

  Trueman Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  BabieWana@Sikia ww kama wataka kujua kosa la Ponda nenda mahakamani na kama una ushahidi kuwa Ponda hana hatia peleka mahakamani usibwabwaje kam zuzu
   
 19. doup

  doup JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  uongozi wa bakwata upatikanaje?, naamini huko hakuna rushwa kama kwenye siasa; wekeni watu safi.
   
 20. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  si vizuri kuzungumzia jambo ambalo tayari lipo mahakamani,mahakama ndio itaprove whether Ponda is guilt or otherwise.nina imani haki itatendeka na hakuna atakaeonewa
   
Loading...