Kosa la kukata mguu wa mgonjwa

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
[h=3]DAKTARI CHUNYA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKATA MGUU WA MGONJWA NA KUUTOROSHA[/h]


WAZIRI WA WIZARA YA AFYA DR.HAJI MPONDA


HOSPITALI ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imeingia lawamani kwa kumkata mguu mgonjwa na hatimaye kuutowesha mguu huo unaosadikika kupelekwa kwa mfanyabiashara wa madini wilayani humo.


Tukio hilo la kikatili lilitokea January 8, Mwaka huu wilaya humo kwa kumuhusisha Robert Kateni (42) mkazi wa Kijiji cha Mkola katika Mji wa Makongolosi wilayani Chunya ambaye ni mfanyakazi wa mgodi wa madini.


Akizungumzia tukio hilo, Kateni alisema kuwa siku ya tukio alikuwa akifanya kazi katika mgodi huo akitumia mashine ya kupasua miamba na kusaga (Karasha) ndipo mkanda wa mashine hiyo ukafyatuka na kumgonga katika mguu wake.


Anasema baada ya hali hiyo kujitokeza wafanyakazi wenzake walimpigia simu tajiri yao aitwaye Joseph Makulilwa ambaye alifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza katika Hospitali ya wilaya ya Chunya na kumpeleka moja kwa moja katika chumba cha upasuaji bila kuandikisha mahala popote.


‘’Nilishangaa naingizwa Theater na kuchomwa sindano ya usingizi bila kupiga hata Exlay na hatimaye baada ya siku mbili nikazinduka na kukuta mdogo wangu na mke wangu wakiwa na huzuni nilipowauliza kulikoni wakaniambia niwaeleze mguu wangu uko wapi ndipo nikahamaki’’ alisema Kateni huku akitokwa na machozi.


Alisema baada ya kubaini kuwa mguu wake ulikuwa umekatwa wakati yeye hakuumia kiasi cha kushindwa hata kutembea bila kusaidiwa na mtu huku tajiri yake akiwa ametoroka, akawaambia ndugu zake kuwa walipaswa kuondoka Hospitalini hapo ili asije akachomwa sindano ya sumu kuficha ushahidi na wakakubaliana hivyo na kumtafuta mtu baki kwa ajili ya kumuuguza.


Mwananchi huyo anatanabaisha kuwa anakumbuka kuwa Mganga aliyehusika kumkata mguu huo ni Dr. Mgode ambaye anahisi walishirikiana na mwajiri wake ili kiungo hicho kitumike katika shughuli za madini na baada ya kupata nafuu aliruhusiwa na kwenda kuomba msaada wa kisheria katika asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Haki za Binadamu inayojulikana kwa jina la Defence of Human Rights and Citizen Rights ambao wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo.


Mwanasheria wa Asasi hiyo Ally Simanyani alikiri kuwepo kwa suala hilo ofisini kwake na kwamba tayari asasi yake imefanya uchunguzi na kufika Hospitalini na kuonana na uongozi wa Hospitali hiyo ya wilaya ambao hauna vielelezo vya msingi vya kumkata mguu mwananchi huyo.


‘’Suala hili limejaa ubabaishaji kutoka kwa watumishi wa Serikali, maana tulipofika Hospitralini Juni 29, mwaka huu walikiri kuhusika na ukataji wa kiungo cha mlalamikaji na kwamba hawajui walikipeleka wapi, tuliopoomba Xxray na mahala alipokuwa amesaini mgonjwa ili kulidhia kukatwa mguu wake hawakuwa na maelezo kwasababu inaonekana kuwa hili suala lilipangwa’’ alisema Simanyani.


Alisema baada ya kuona uongozi wa Hospitali hiyo kushindwa kujibu tuhuma hizo walipeleka suala hilo Polisi na kufungua jalada la uchunguzi lenye namba 13/2011 chini ya Askari aliyemtaja kwa jina moja la Borniface na kwamba walipofuatilia zaidi Novemba 31 mwaka huu Polisi nao wameshindwa kutoa majibu ya uhakika.


Sanjari na hayo, Mwanasheria huyo alisema kuwa wanatarajia kulifikisha suala hilo mahakamani kwa kumshitaki Daktari huyo kwa kosa la jinai na pili wataifungulia Serikali kesi ya madai kwa kuajiri mtu anayetumia taaluma yake isivyopaswa na kufungua mashitaka ya mtu atakayepatikana na kiungo hicho.


Joseph Makulilwa ambaye anadaiwa kufanya mpango wa kumkata mguu mfanyakazi wake na kusadikika kumiliki kiungo hicho alikiri kuwepo kwa uvumi huo na kwamba yeye alikuwa hausiki na kutupa lawama kwa Daktari aliyetekeleza tendo hilo.


‘’Ni kweli Robert alikatwa mguu lakini mimi sikuhusika na mpaka askari walikuja kupekua kama huo mguu upo kwangu lakini hawakuupata nadhani mtu wa kujibu suala hili ni Daktari maada mimi siyo daktari niyayeweza kujua kuwa ningemtibu vipi na hivi karibuni nilitaka kumnunulia mguu alikataa’’ alisema Makulilwa.


KALULUNGA COMMUNITY MEDIA TANZANIA: DAKTARI CHUNYA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKATA MGUU WA MGONJWA NA KUUTOROSHA
 
Jamhuri Watu wa Mbeya bwana...
Usiliangalie hili tatizo kwa akili ya ujazo wa kizibo cha bia. Kama ni kweli hili tukio limetokea kama lilivyoripotiwa, ni kilelele cha unyama na uzembe. Ni kielelezo jinsi Tanzania ilivyokosa uongozi madhubuti.
 
Usiliangalie hili tatizo kwa akili ya ujazo wa kizibo cha bia. Kama ni kweli hili tukio limetokea kama lilivyoripotiwa, ni kilelele cha unyama na uzembe. Ni kielelezo jinsi Tanzania ilivyokosa uongozi madhubuti.

ndugu yangu, wajenzi wawili hawagombei fito! mimi naijua fika serikali yetu, lakini hili limekuwa powered na ushirikina wa wanajamhuri wa mbeya! unakubaliana na mimi?
 
inamaana wambeya ni washirikina kwa sana???
ndugu yangu, wajenzi wawili hawagombei fito! mimi naijua fika serikali yetu, lakini hili limekuwa powered na ushirikina wa wanajamhuri wa mbeya! unakubaliana na mimi?
 
Back
Top Bottom