KOROGWE : Trafiki aliyempiga dereva wa basi matatani

Mambo mengine yanaudhi sana.
Hivi unaanzaje kumpiga mtu mzima mwenzako? Yaani kabisa unatoa mkono unakunja ngumu au unampiga makofi mtu mzima mwenzako?
Kisa wewe ni trafiki?

Mambo mengine watu wanatafutia wenzao kwenda jela bila sababu za msingi, mwisho wa siku mtu anaacha familia inateseka bure.
 
Kuna Traffic mmoja anajulikana kwa ukorofi Mji wa Katoro, Alimpiga kofi Mzee mmoja aliekuwa anaendesha Tax kutoka Katoro kwenda Butengo. Kisa hana Leseni inayoruhusu kubeba Abiria.
Mzee wa watu akili ilihama kwa dakika 5. Alikuwa kama kachanganyikiwa hivi.
Kamwe usibishane na Traffic ukiwa umekaa kwenye gari. Utalambwa kofi akili ihame.
Nazani huwa wanaangalia sura za kupiga,
 
Kile kitendo tu cha kwamba wananchi walimjia juu huyo askari usalama barabarani ni ishara ya ukomavu katika kuelewa haki za msingi za raia ikiwemo haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wako..

Huko nyuma kitendo cha dereva kuhoji kupigwa kofi kingepelekea kusombwa pamoja na abiria wote au baadhi na kuswekwa ndani bila masuali.

Huko Mara kamishna wa ardhi amesimamishwa kazi kwa kushindwa kumsaidia bibi mmoja ambae aliporwa ardhi yake na waziri Lukuvi tayari leo amefika Musoma ku-sort out masuala ya watu kuporwa ardhi zao mchana kweupe.

Pale TAKUKURU mkurugenzi wa mipango alikuwa akikusanya fedha za wafanyakazi na watu wengine wapatao 200 na kudai kuwauzia vwanja huko bagamoyo na wengine wasipate viwanja hivyo hadi leo.

Fikiria watu Zaidi ya 200 uwatoze ada za wiwanja kuanzia milioni 3 hadi 7 kwa kiwanja huko Bagamoyo!

Hivyo bwana Diwani amepelekwa pale ku-sort out matatizo hayo likiwemo la kumfikisha kwenye vyombo vya sheria huyo mwanamke aitwae Kulthum Mansoor ambae bwana Mlowola alikuwa akipata kigugumizi kumshughulikia.

Tanzania imepata raisi ambae anajali wanyonge na matunda ya kumpata raisi anaejali maisha ya wanyonge yanaendelea kupatikana.

Zile zama za dhulma, uonevu , uzandiki zinaelekea kupotea.
 
Kwa wananchi tunaambiwa tufuate sheria bila shuruti. Jee kwa walinda usalama wamepewa kibali cha kufanya lolote lile ambalo wanataka au wanapaswa wafuate standing order?????
Baada ya Askari kumtuhumu dereva kuwa aliendesha basi kwa kasi ya 57kph kwa saa kwenye sehemu ambayo alipaswa kuendesha kwa kasi ya 50Kph ni sawa kabisa lakini pia dereva alikuwa sahihi kumuuliza traffic kuhusu kibao kinachoonyesha hivyo siyo kosa kabisa.
Kwa kawaida ni kosa la jina kwa kupiga sasa tuone itakuwaje kwa askari huyu.
Ni dhambi kuficha magonjwa kama haya na matarajio yetu ni kwamba tutaarifiwa kinachoendelea.
Hiyo ya trafic kukaa maeneo ambayo hayana vibao nimegombana sana na trffic barabara ya Mbeya- Chunya, traffic anaenda kujitega eneo ambalo halina alama hafu anakwambia we huoni kuwa ni makazi na mm namuuliza hii ni highway unazani Tanroad ni wajinga kutokuweka kibao cha 50KM hapa? Anaanza kuwa mkali anataka tu umpe leseni.
 
Ungeweka video wala usingepata shida ya kufanya hiyo narration....
 
Aamekataa kutoa ya kiwi na brush acha apigwe hajui polisi saivi wapo juu ya sheria
 
Ukweli kwa sasa kitengo cha usalama barabarani kinaendekeza faini sana kwenye magari, hasa swala la over speed, waelewe kwamba kwa sasa madereva wengi wameelimika swala la speed, ukimuotea mtu yupo speed kwenye 50 ni bahati mbaya sana kwa sasa.
 
Hakuna kesi hapo
Askari wa Usalama Barabarani wilayani Korogwe mkoani Tanga, ambaye jina lake halijafahamika, anatuhumiwa kumpiga dereva wa basi la Tahmeed Coach baada ya kumkamata kwa mwendokasi.
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Leonce Rwegasira akizungumza kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alisema wanaendelea kulifanyia uchunguzi tukio hilo.

“Ni kweli tukio lipo. Tunaendelea na uchunguzi utakaotuelekeza ni hatua gani za kuchukua dhidi ya mtuhumiwa kama tutabaini kosa.”
Taarifa za kupigwa kwa dereva wa basi hilo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa iliyopita baada ya video zilizokuwa zikionyesha tukio la wafanyakazi wa basi hilo pamoja na abiria, wakimshambulia kwa maneno askari huyo.

Video hiyo pia ilionyesha abiria na wafanyakazi wa basi hilo ambalo lilikuwa likitokea Nairobi, Kenya kuelekea Dar es Salaam wakimlalamikia askari huyo kwa kumpiga dereva wa basi hilo. Video hiyo inaonyesha jinsi mabishano hayo yalivyokuwa yakiendelea huku mfanyakazi mmoja wa basi na abiria wakilalamika kuwa kitendo kilichofanywa na askari huyo si cha kiungwana.

“Kama anakosa si ungemtoza faini baada ya kumuonyesha uthibitisho, kwa nini mnampiga?” anaonekana mfanyakazi wa basi hilo akimhoji mmoja wa askari aliyekuwa akiwataka wanyamaze. Sauti nyingine inasikika ikisema, “Trafiki anampiga dereva, kamwandikia faini lakini bado anaendelea kumpiga dereva kutoka Dar kuelekea Nairobi, kwa kosa la kuzidisha spidi. Je, hii ni haki.”

Sauti nyingine ambazo zinazosikika katika video hiyo ni pamoja na “una-power (nguvu) gani ya kumpiga dereva… aah mwache ampige, mwache ampige…. endelea kumpiga.” Askari mmoja katika video hiyo anaonekana akihoji ushahidi wa dereva huyo kupigwa na hapo sauti nyingine inasikika, “Amempiga...mimi ninao ushahidi. Nimemuona akimpiga, mimi ninao ushahidi.”

Dereva huyo alipotakiwa kueleza ukweli wa tukio hilo, licha ya kuthibitisha kutokea, hakutaka kuingia kwa undani akisema alikuwa barabarani akiendesha gari.
“Nikweli tukio limetokea lakini kwasasa siwezi kuzungumza niko barabarani ninaendesha gari nikifika Dar es Salaam nitakupigia kueleza ukweli wa tukio” alisema.

Alipotafutwa baada ya kufika dereva huyo alisema hawezi kuzungumza mpaka apewe maelekezo na bosi wake juu ya kipi azungumze. Baadaye, Mwananchi lilimtafuta msimamizi wa mabasi hayo upande wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mabasi Ubungo (UBT), Nguzo Abdallah ambaye alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa Ijumaa iliyopita huko Korogwe.

Alisema dereva huyo aliyemtaja kwa jina mojo la Salehe, alisimamishwa na askari akimtuhumu kuendesha gari kwa mwendokasi.
“Ukweli ni kwamba, baada ya askari kumsimamisha dereva, alimweleza amezidisha mwendo wa kilomita 57 kwa saa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani ambayo inamtaka kwenda kilomita 50 kwa saa katika eneo hilo,” alidai Abdallah.

Alisema baada ya kukamatwa, dereva alimtaka askari huyo amtajie eneo kilipo kibao kinachoonyesha 50, lakini askari hakumtajia na badala yake alimwambia ajiongeze la sivyo atapelekwa Mahakamani. Alisema dereva aliendelea kugoma akimwambia kuwa anamuonea kauli iliyosababisha askari huyo kuanza kumshambulia kwa matusi na kipigo.

“Baada ya kuona tukio hilo, abiria walishuka na kuanza kumsaidia dereva asipigwe na askari huyo na wengine wakawa wanarekodi tukio hilo kwa simu zao,” alisema meneja huyo.
Mbali ya Abdallah, meneja wa kampuni ya mabasi hayo, Hassan Singano alisema taarifa za tukio hilo zinashughulikiwa na dereva wao alifika kituo cha usalama barabarani Korogwe kuhojiwa.

“Taarifa nilizonazo hadi sasa, ni kuwa dereva wetu alikuwa akiendesha gari nje ya kilomita ambazo zipo kwenye kibao, askari walimkamata, lakini dereva akadai aonyeshwe hizo picha zinazomuonyesha ameendesha kwa kasi na kibao kinachomtaka atembee kilomita 50 kwa saa, lakini hakuonyeshwa.

“Katika kubishana pale, ikafikia hatua askari kumshambulia kwa matusi na kipigo, lakini suala hilo bado linafuatiliwa na kampuni. Kama kutakuwa na taarifa zozote tutakujulisha,” alisema Singano.
Hakuna kesi hapo sanasana polisi atahamishwa!! Hapo dawa ni dereva aliyepigwa kusubiri muda upite watu wasahau kisha aanze kula sahani moja na huyo ndata uswahili!
 
akamloge au?
 
Hiyo kideo iko wapi mleta uzi nimi nishuhudie kichapo
 
Sasa hiyo matatani iko wapi hapa mkuu ? hiyo kuchunguza "endapo itaonekana kuna kosa " ndio matatani ? Traffic amemaliza shift yupo juu ya stuli ndefu wakati Dereva anaugulia maumivu, kati yao nani yupo matatani ?
 
Polisi angetakiwa aingie ndani awasalimie abiria na kuwaeleza kosa la dereva . Ajue awamu hii rushwa ni sumu .
 
Wapigwe tu wame zidi madharau,ila nyie viongozi wa polisi mbona mnapenda kucheza mbele ya kamera! Hivi jambo dogo kama hili nalo mumelitangaza kwa media,shem on some of the police officers!!
 
Back
Top Bottom