Korogwe: Serikali yafuta mashamba sita ya Mohammed Enterprises

Korogwe: Serikali yafuta mashamba sita ya Mohammed Enterprises

Na uende naye pia huko India kama unampenda sana, Afrika for Afrikans, time is now!
Niliwahi kuijibu hoja yako humu na kukuonya juu ya ubaguzi huu wa wazi uliojaa moyoni mwako! Mo kazaliwa na kukulia singida na dar na hajawahi kuishi India! Kwanini umuite au umtake akaishi India asikokujua? Mbona wewe hurudi kwenu Burundi? Huko ulikofundishwa kuwabagua watu ipo siku yatakugeuka na Mungu anipe uhai nilisimamie hili la kuung'oa ukoo wako wote na kuwarejesha kwenye asili yenu ukaone na kujifunza madhila ya ubaguzi! Siasa unazoshabikia bila kujiuliza hazina afya kabisa kwa zama hizi! Kama vipi kang'oe na viwanda vyake umpelekee India!
 
Serikali yafuta mashamba sita ya Mohammed Enterprises

Serikali imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12, 915.126 ya kampuni ya Mohammed Enterprises yaliyopo korogwe mkoa wa Tanga.

Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya wilaya ya Korogwe kuyafuta mashamba yasiyoendelezwa kwa muda mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa.

Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula, amesema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises Mazinde wilayani Korogwe, na kubainisha kuwa uamuzi huo unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali ili kuzingatia masharti ya uwekezaji.

Alisema, mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohammed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu ya mambo ya halmashauri husika la kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa rais na kuridhiwa.

Alisema, uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohammed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji.

Hata hivyo, Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri.

Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.

Aidha, Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela, kwa kufanya kazi nzuri ya kufuatilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa huo aliwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo.

Alisema, ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi na uwekezaji.


Chanzo: IPP Media
Zimbabwe ya Mugabe ileeee yaja taratiiibu....
 
Nia ni kumfanya aishi kama shetani au kuna sehemu kakosea so sheria imefuata mkondo wake?
Unapoandika "sheria imefuata mkondo wake" umepaswa kuhakikisha (spelling check) kwa umakini mkubwa ama la sivyo all 'O' zikiwa replaced na 'U' itakuwa balaaah!
 
MO ni mtu ambae namuheshimu katika nchi hasa nilipoamua kuifuatilia vizuri historia yake namna alivyoiweka MOHAMED ENTERPRISES pale ilipo leo. Niliapia ipo siku nitakutana na MO na kumuuliza mengi...

LAKIN KATIKA HILI LA KUWA NA MASHAMBA MAKUBWA NA HAYATUMII SIWEZI KUWA UPANDE WAKE INGAWA WENGI HATUJUI NYUMA YA HAYA KUNA NINI..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naipongeza serikali.
Kwa Muda mrefu miji kama Mombo imeshindwa kuwa miji ya kisasa.

Watanzania Wazawa wanakosa ardhi ya kujenga na wengi wamekimbilia kujenga kwenye mawe kama mijusi walati huo huo kuna Mtu anamiliki maelfu ya Hekari za ardhi nzuri kwa ujenzi na yenye Rutuba .

Kuna watu wanaishi mabondeni Maeneo ya Misajini kila mwaka wanakumbwa na mafuriko wakati huo huo maeneo yenye mapori ya mikonge hayapatwi na mafuriko mana wakoloni walijipimia maeneo bora ya kilimo na kuishi.

Afrika itajengwa na waafriaka wenyewe.

ARDHI YETU YENYE RUTUBA WALIKUJA KULIMA MIKONGE WAKATI KWAO ARDHI NZURI WANALIMA MATUNDA NA MBOGA MBOGA NA VYAKULA BORA KWA AJILI YA AFYA ZAO NA KUTUUZIA VYAKULA VITAM KWENYE MASUPER MARKET.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
MO ni mtu ambae namuheshimu katika nchi hasa nilipoamua kuifuatilia vizuri historia yake namna alivyoiweka MOHAMED ENTERPRISES pale ilipo leo. Niliapia ipo siku nitakutana na MO na kumuuliza mengi...

LAKIN KATIKA HILI LA KUWA NA MASHAMBA MAKUBWA NA HAYATUMII SIWEZI KUWA UPANDE WAKE INGAWA WENGI HATUJUI NYUMA YA HAYA KUNA NINI..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana mashamba maeneo ya punga korogwe tanga mashamba ya Chai na yanafanya kazi
Kaajiri vibarua kibao....

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naipongeza serikali.
Kwa Muda mrefu miji kama Mombo imeshindwa kuwa miji ya kisasa.

Watanzania Wazawa wanakosa ardhi ya kujenga na wengi wamekimbilia kujenga kwenye mawe kama mijusi walati huo huo kuna Mtu anamiliki maelfu ya Hekari za ardhi nzuri kwa ujenzi na yenye Rutuba .

Kuna watu wanaishi mabondeni Maeneo ya Misajini kila mwaka wanakumbwa na mafuriko wakati huo huo maeneo yenye mapori ya mikonge hayapatwi na mafuriko mana wakoloni walijipimia maeneo bora ya kilimo na kuishi.

Afrika itajengwa na waafriaka wenyewe.

ARDHI YETU YENYE RUTUBA WALIKUJA KULIMA MIKONGE WAKATI KWAO ARDHI NZURI WANALIMA MATUNDA NA MBOGA MBOGA NA VYAKULA BORA KWA AJILI YA AFYA ZAO NA KUTUUZIA VYAKULA VITAM KWENYE MASUPER MARKET.



Sent using Jamii Forums mobile app
Ardhi ipo mitanzania mivivu ardhi ipo wanaiangalia tu....
Serikali kwanza haijawahi kufikiria kuwa empower raia kwenye kumiliki ardhi na kufanya kilimo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri sana, ardhi haitumii aachiwe ya nini? Wapewe wazawa wajenge majumba au wafanye kilimo kuliko kuachia majitu yenye ubaguzi. Kudadeki Magufuli kura yangu unayo 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kumyang'anya mashamba ndio mnahisi mmemkomoa? Haya tuone serikali iyaendeleze wao bas! Na swala hili linashadadiwa na vijana ambao wameshindwa hata kuwa na vitalu vya mchicha uani kwenye majumba yao!
 
Haha..kwa hiyo hao wananchi wanataka kulima katani au ndo basi kukomoana......baada ya miaka kadhaa tupate mrejesho jinsi hao wananchi nao watakua wameboresha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika wataishi kama mashetani ni mojawapo ya kauli iliyowahi kutolewa na sasa inafanya kazi

Baada aliyekuwa mwenyekiti wa YANGA kukumbwa na misukosuko kutoka serikali ya JPM na kampuni zake kupelekea kufilisika na zingine kufungwa na sasa ni kwa mfanyabiashara Mo Dewji


Serikali yamnyang'anya mashamba 6 mkoani Tanga na huku waziri akitoa onyo Kali

IMG-20190115-WA0017.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom