Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Majimarefu aliyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Vijji vya Kwemshai, Ngulu na Mlungui, katika ziara yake Jimboni mwake
Alisema licha ya kuwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini baada ya afya yake kuimarika amerejea nchini akiwa tayari kutatua kero za umma
Aidha, amewaomba wapiga kura wake kuendelea kushirikiana naye huku wakimpatia muda kumwezesha kuwatatulia kero hizo
"Nawashukuru kwa kuniombea pale nilipokuwa nikiugua, nilikuwa nje ya nchi kwa matibabu Sala zenu zimeniwezesha kuungana nanyi leo "alisema
Aliwaeleza wananchi wa Kijiji cha Mlungi kuwa tatizo la maji na umeme viko mbioni kutatuliwa ndani ya mwaka huu na kwamba wale wanaoeneza maneno kuwa hakutufanyia kitu wanajidanganya kwa vile mambo yanakwenda sawa
Majimarefu alisema katika kuhakikisha wananchi watapata maendeleo, alisema ameamua kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kusimamia Mfuko wa jimbo kusaidia miradi.
Chanzo: Nipashe