Korea yanunua ardhi "kwa mkopo" Tanzania, Serikali yasita kuthibitisha

Mimi napenda sana na tena tabia ya South Korea kwa Taifa lolote lile lazima awe Mkristo hata hawa vingozi wetu ni lazima waonane kanisani ndio unaweza kupata misaada, hiyo ni HONGERA SANA kwa kazi nzuri ya kwenda huko Pinda
 
Kama ni hivyo ... hizi ni bangi mbichi
 
Mimi napenda sana na tena tabia ya South Korea kwa Taifa lolote lile lazima awe Mkristo hata hawa vingozi wetu ni lazima waonane kanisani ndio unaweza kupata misaada, hiyo ni HONGERA SANA kwa kazi nzuri ya kwenda huko Pinda

Ati na wewe ni great thinker..Shame!
 
Yaani ukitaka kujua jinsi tusivyothaminiana, hii habari mpaka itoke BBC kwanza ndiyo vyombo vya habari vya hapa nchini vihabarishwe. Kwanini kila kitu kinafanyika kisirisiri?! Hata kama mpango wote unafanyika kwa manufaa ya Watanzania, kuna ubaya gani wananchi kujulishwa wakati wa mchakato, walau kujulishwa tu viongozi wetu wamefikia wapi...
 
Bado hatujifunzi tuu? Naomba Pinda ajifunze Nicaragua jinsi wamarekani wanavyoshikilia ardhi ya nchi hiyo na namna serikali ya marekani ilivyoshiriki kupindua serikali au kuua watu walioonekana kushabikia ardhi ya kilimo cha migomba irejeshwe mikononi mwa wanicaragua. Nasi tunanaka kwenda huko?
 
Mengi tutasema lakini tena watanzania wanaosoma marekani ninawalaumu sana. Hivi masha, Ngeleja si wametoka huko?? mbona wanaboronga??
 
Kwani kuhamia nchi nyingine hata Congo tu ni shilingi ngapi? maana naona hakuna tunachoweza.Hii ni sawa tu na mtu kuja nyumbani kwako na kukwambia atakusaidia kupata mtoto ila ni lazima umkaribishe chumbani kwako umwache na wife kwa muda mfano huu hauna tofauti na mtu anayesema atakulimia lakini mpaka kwanza afue chuma akusanye na madini mengine ili aweze kuendesha mradi.. Sijui ni nini tunaweza maana hako ka mtaji wanakokataja watu wamepiga zaidi ya hizo mara ngapi sijui.. Daah haya bana
 
Bado hatujifunzi tuu? Naomba Pinda ajifunze Nicaragua jinsi wamarekani wanavyoshikilia ardhi ya nchi hiyo na namna serikali ya marekani ilivyoshiriki kupindua serikali au kuua watu walioonekana kushabikia ardhi ya kilimo cha migomba irejeshwe mikononi mwa wanicaragua. Nasi tunanaka kwenda huko?

Katika hili kinacho takiwa kufanywa na serikali (sijui kama wamefanya hilo ni kuwapa mkataba wa miaka 50 na si zaidi) ili kama kuna uharibifu wowote basi baada ya mkataba wanaondolewa
 
Yaani ukitaka kujua jinsi tusivyothaminiana, hii habari mpaka itoke BBC kwanza ndiyo vyombo vya habari vya hapa nchini vihabarishwe. Kwanini kila kitu kinafanyika kisirisiri?! Hata kama mpango wote unafanyika kwa manufaa ya Watanzania, kuna ubaya gani wananchi kujulishwa wakati wa mchakato, walau kujulishwa tu viongozi wetu wamefikia wapi...

SteveD, wanajua mpango hauna manufaa kwa Watanzania ndiyo maana wanafanya siri. Angalia ile mikataba ya kuchimba dhahabu yetu iliyosainiwa mwaka 2000 na Serikali ya Mkapa kati ya Tanzania na Barrick hadi hii leo bado ni siri kwa wenye mali.
Wanafanya hivyo makusudi ili kuficha madhambi yao ya kusaini mikataba ambayo haina maslahi kabisa kwa nchi yetu, labda walipewa mshiko wao ndiyo maana hawakuona umuhimu wa kutetea maslahi ya nchi.
 
Mimi napenda sana na tena tabia ya South Korea kwa Taifa lolote lile lazima awe Mkristo hata hawa vingozi wetu ni lazima waonane kanisani ndio unaweza kupata misaada, hiyo ni HONGERA SANA kwa kazi nzuri ya kwenda huko Pinda

udini mkuu hapa hauna nafasi, sema tu tumeliwa watanzania.
 
Ninacho omba kuuliza jamani hivi hakuna nchi duniani ambayo kuna wawekezaji ktk kilimo na maisha ya wananchi yanaenda vizuri??
 
Katika hili kinacho takiwa kufanywa na serikali (sijui kama wamefanya hilo ni kuwapa mkataba wa miaka 50 na si zaidi) ili kama kuna uharibifu wowote basi baada ya mkataba wanaondolewa

Ndugu system ya kibepari inavyo operate hata uwape miaka 50 watahakikisha kuwa itakapokaribia hiyo miaka marekebisho yanafanyika kuwahakikisha maslahi yao yanalindwa. Watahakikisha wanaandaa watu wa kushika dola ambao ni watiifu kwao kwa gharama yoyote ile. Hata hizi scholarships tunazopewa kwenda kusoma kwao usifikiri zina kuja bure. Watu wanaowasomesha miongoni mwao ndio watakaotumika hapo baadaye kuhakikisha kuwa wanashika dola na kuwafanikishia mambo yao
 
baada ya sera ya ARI MPYA ,NGUVU MPYA NA KASI MPYA KUPROVE FAILURE, sasa amekuja na SERa mpya ya KILIMO KWANZA
yaani hapo ni kilimo tu kama ni WENYE KUBEBA ALMASI SAWA, WENYE KUBEBA GOLD SAWA, WENYE KUBEBA CHUMA SAWA, LAKINI KILIMO KWANZA
TEHE TEHEE
 
"Some African countries export fruit and import fruit juice, or export olives and import olive oil, simply because their past colonialists did not teach them how to process food," he told the AFP news agency.

mh! haya matusi
 
  • Kama waliuza Loliondo, watashindwaje kuuza huko Pwani kusiko hata na wanyama pori?
  • Asemaye ukweli ni TZ Gov au Korea?

Korea yatangaza kununua ardhi kubwa Tanzania, serikali yakanaNa Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Ulaya kuwa imeuza ardhi ya ukubwa wa kilomita za mraba 1000 za kilimo kwa Korea ya Kusini kwa ajili ya matumizi ya kilimo si za kweli.

Taarifa zilizotolewa jana na vyombo hivyo zilieza kuwa Korea Kusini imekubaliana na serikali ya Tanzania kufikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya mataifa masikini na tajiri duniani.

Afisa wa Shirika linaloendeshwa na Serikali ya Korea linaloshughulikia maendeleo ya kilimo vijijini, Lee Ki-Churl, alinukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akisema kwamba mkataba huo utasainiwa mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkataba wa makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ni matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoifanya katika mataifa ya mashariki ya mbali.

Akizungumza jana, Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika, Steven Wasira, aliliambia gazeti dada la hili la The Citizen kuwa hakuwa na taarifa na mkataba huo.

"Nilikuwa sehemu ya ujumbe wa Waziri Mkuu Korea Kusini na kilichotokea kule hakikuwa zaidi ya kuwakaribisha wawekezaji wa kigeni katika sekta zote ikiwamo ya kilimo." Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko alikanusha na akasema hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na serikali katika kilimo na Korea Kusini.
 
Watanzania wengi tunatabia ya kuogopa mabadiliko. Hili ndilo linalotukwamisha sana. Katika kujadili hili, Wengine wanataka tutoe mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa kukodisha ardhi, huku wao wakisita kutoa mifano ya nchi kama Tanzania zenye ardhi tele lakini zinanunua juisi ya embe toka Uarabuni (na hili tunaliona ni tusi, lakini kwani ni uongo jamani? Maaza zinatoka wapi? Hata Kenya tu si wananunua machungwa Muheza halafu wanatuuzia juisi?

Wengi wetu tumejadili namna tunavyoshindwa kuitumia ardhi hii kwa miaka kadhaa, lakini mbona hatuna njia mbadala za kupendekeza?

Ni kweli uongozi hauna sera makini za kutufanya tutumie ardhi kwa kutunufaisha, lakini sasa ndo tufanyeje?

Kujadili mustakabali wa taifa kwa kashfa na matusi (nasoma kuna mtu kaita mchango wa mwenzake eti "utoko," ni kielelezo cha ufinyu wa mawazo yanayotegemea kuiga tu, na wala hakuna ubunifu unaotakiwa kutuwezesha kupambana na mazingira yetu.

Tunazunguka mbuyu tu pasi na kutoa muelekeo, tutafika wapi? Ni wajibu wetu kama "great thinkers" basi kujadili hoja ya kuleta wawekezaji toka nje tukichambua kwa umahiri faida na hasara za kufanya hivyo. Katika uchumi wa sasa, kama tutaendelea kujiziba masikio na kuendelea na fikra zetu tulizodumisha kwa miaka 45 iliyopita, tutajikwamua lini na lindi hili la umasikini?

Kuna mtu ameuliza, hivi tunaweza kufanya nini kama hata kulima mpunga kwa kiwango cha kibiashara hatuwezi? poor policies, so what's next?

Nchi kadhaa zimetusaidia miradi ya kilimo iliyokufa, je, tumerithi nini toka kwa Kapunga Rice Project ya Wajapani? kuna miradi mingi ya chakula inaanzishwa na kufa mara tu wenyewe wakiondoka, je hii inatufariji sana?

Tunajisikiaje tunapoona ardhi kubwa kule Ruvu, na maji yake yanamwagika tu Baharini, wakati kuna watu wanalala njaa?

Israel ina ardhi yenye kulimika ambayo ni 2% tu ya 23,000km hivi, lakini wanajitosheleza kwa chakula na kuuza sana Ulaya. Kuna ubaya gani tukitumia ujuzi wao wa teknolojia, kwa kuchanganya na maji yetu na ardhi yetu, kujikwamua kiuchumi?

Mimi naunga mkono kuwakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kilimo cha chakula ili mradi tu maslahi ya taifa yalindwe, kuliko kuwapa wawekezaji ardhi kubwa kwa ajili ya biofuel production, ambayo ni garantii ya kutuletea mfumuko wa bei ya chakula na njaa. Mbona mnaopinga Wakorea hampingi biofuel investments ambazo ziko tayari huko bagamoyo, Kisarawe? Mnajua kuna masikini wetu sasa hawalimi mashamba yao ya mahindi na wamekimbilia kufanya kazi kwenye mashamba ya jatropha?

Mimi naona hili jambo ni sensitive sana, na tujadili kwa umakini badala ya blah blah. Hasira na kejeli haisaidii kuzuia globalisation, na hatuwezi kujifungia na ardhi yetu wakati misaada yao tunapokea kwa mikono miwili!

Dawa yake ni kujifunza namna bora zaidi ya kunufaika na ushirikiano huu wa lazima, badala ya kupiga kelele tu.
 
Mbalamwezi,
Soma tena ripoti kwa makini. Hawa si wawekezaji. Wanakuja mkono mtupu, wachimbe madini, wakipata hela ndipo waziingize kwenye kilimo. Halafu mnagawana mavuno nusu kwa nusu wakati hela ya madini wanaweka mifukoni. Hii wala si win-win situation. Ni win situation kwa Wakorea.
 
Kumbe unajua kuwa unaweza kutumia technologia ya Israel. Swali unasubiri nini? Serikali?

Acheni longolongo.
 
Mbalamwezi,
Soma tena ripoti kwa makini. Hawa si wawekezaji. Wanakuja mkono mtupu, wachimbe madini, wakipata hela ndipo waziingize kwenye kilimo. Halafu mnagawana mavuno nusu kwa nusu wakati hela ya madini wanaweka mifukoni. Hii wala si win-win situation. Ni win situation kwa Wakorea.

Unaweza ukawa sahihi Jasusi,

lakini wanawezaje kuchimba madini wakiwa mikono mitupu, nasi tunashindwaje kuchimba madini hayo hayo mikono mitupu?
 
Back
Top Bottom