Korea yakubali Kuisadia Tanzania Usalama wa Mtandao wa Internet

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
tz-kr-jpg.498358

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mapema leo Aprili 19.2017, imetiliana saini ushirikiano katika masuala ya Usalama katika mitandao ya hapa nchini na Shirika la masuala ya Usalama na Internet kutoka Korea lijulikanao kama KISA (Korea Internet & Security Agency).

Utiliaji wa saini huo umefanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo alliweza kuiwakilisha Wizara hiyo na kueleza kuwa, ushirikiano huo utasaidia utendaji wa kazi nakuboresha maisha ya kijamii kwa kuwa na usalama na matumizi mazuri ya mitandao.

Dkt. Sasabo amebainisha kuwa, Ushirikiano huo utasaidia kuboresha maisha ya kijamiii na kuwezesha ushiriki wa wananchi wengi katika mifumo yote ya kifedha kwa sababu sasa hivi kila mwananchi mwenye simu ni kama vile amepata benki kwani kuharakisha kupata huduma za kulipa ndipo unapopata unachohitaji hivyo pamoja na kukuwa kwa teknolojia na faida zake za uchumi , zimekuja na changamoto za usalama wa mitandao hivyo Serikali imeamua kushirikiana na Shirika hilo la KISA.

“Mapema leo kabla ya zoezi hili, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameshiriki katika tukio la makubaliano na shirika la KISA ambao ni wataalamu wa mitandao . ushirikiano ambao ni wa kuanzia miaka mitano (5). tutakuwa na mashirikiano ya karibu katika kupata elimu, kubadilishana wataalamu na pia kuangalia usalama wa miundombinu yetu.

Wenzetu wamepiga hatua zaidi kwenye mawasiliano. kwa mfano simu za Samsung zinatokea Korea kwa hiyo kidogo wametutangulia katika baadhi ya maeneo na tunaangalia uwezekano hata wao kuja kuwekeza baadhi ya viwanda hapa nchini mwetu.” Alieleza Dk. Sasabo.

Kwa upande wake Rais wa KISA, Bwana Oh JinYoung (Jeffrey) ameshukuru Serikali ya Tanzania katika makubaliano hayo ambapo wataendelea kuhimalisha ushirikiano wao katika kufikia malengo.


-----
Maoni Yangu

Sasa Vijana Mnaotukana Hovyo Kaeni Mkao wa Kuliwa maana wale jamaa kwa tekchnolojia ya Mawasiliano wako Mbali sana.

Tuombe Mungu wasimshauri Rais Kuzifuta Facebook, Instagram, Twitter na na WhatsApp

NB: SOUTH KOREA
 

Attachments

  • IMG_20170419_154048_831.JPG
    IMG_20170419_154048_831.JPG
    55.5 KB · Views: 67
Hii inamaanisha jamaa pia wanaweza kutumia njia hii kufahamu siri zetu. Mbaya sana!
 
Hapo kinachofanyika ni wao kutupatia teknolojia wanazotumia halafu sisi wenyewe tunazifunga na kuzitumia kwa utashi wetu kung'amua shughuli za udukuzi wa kijasusi na uhalifu mwingine wa kimtandao.

Naona serikali ya Tanzania imeona umuhimu wa ulinzi wa mitandao yake na mawazo kama hili kupitia hapa na mengine yanasaidia sana: Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari

Hii ni serikali makini, big up.
 
Yule Mwanausalama wa Uskochi Evarist Chahali alilisema hili, Kuwa Serikali ina mpango wa kudhibiti Internet sasa naona yanatimia.
 
Sipati picha kama iwe tumeingia mkataba na Korea ya yule Dogo mapanki (North Korea).

Maana wakat Wa msako Wa Trump hakuna atayesalimika...chezea marekan wewe..utaumia
 
Hebu waboreshe huduma za jamii waachane na hizi kuwapa hao wakorea mihela kibao wakati vijijini watu wanakufa hawana madawa, mfano tu juzi mumesikia geita huko.
 
Back
Top Bottom