Korea ya Kaskazini wasema wataendelea na jaribio la silaha

Korea ya Kaskazini wasema wataendelea na jaribio la silaha

watanzania tumekuwa washabiki na wapenzi wa vita kweli dunia ishafika mwisho...ila aangalie US isije ikawa kama ushindi wa trump dhidi ya hilary
 
Mkuu madhara ya nuclear weapons yanajulikana mkuu lakini US ndio anataka watu wa Asia Pacific makazi yao yawe ni kwenye mahandaki na sisi huku kwetu tufe kwa Radiation
Kwani Korea hana cha kupoteza na siku zote ogopa sana mtu ambae hana cha kupoteza ametengwa na Dunia toka 1962 KIM hata kusafiri sijui kama hata mkutano ya UN anakwendaga
Kwenye hiyo mikutano ya kinafiki ya UN Akafanye nini...?

Yani yule ni zaidi ya Dereva wa Lori.
 
Mnakosea sana kuwalinganisha SAADAM GADAFFI na kim hawa walikuwa wananunua silaha kutoka huko nchi za magharibi N korea kila kitu wanajitengenezea wenyewe iraq waliichangia wengi kuipiga na libya vile vile
Upo sahihi mkuu, US anapokwenda kuvamia nchi yoyote ile ni lazima vibaraka wake wawe nyuma yake (Uingereza na Ufaransa nk )
 
Endeleeni kumtia ujinga. Zama za ukoo wa Kim kuitawala NK kama mandondocha zimefikia ukingoni. Alitawala Babu, katawala Baba, natawala Mimi ndio mwisho. Nchi ni ya wananchi sio ya familia fulani.

Labda nchi yetu, yetu hatupangiwi hata Kama no familia moja.
 
NK haina uchumi wa kuendesha vita na Marekani
Vita ya kileo siyo ya kuchukua miaka lukuki! Ni vita ya Massa tu! Inategemea una midude gani! NK noma! Mchina keshasema hapo Hamna mshindi, kauli ambayo haijapingwa na yeyote mpaka muda huu akiwemo Trump mwenyewe!
 
NK haina uchumi wa kuendesha vita na Marekani
Uchumi wa kazi gani tena hapa, kama USA anatumia pesa kuendesha vita bc N.K wao hawahtaji pesa cos kila kitu kishaandaliwa miaka mingi tu.
 
Bingwa ni yule atakae bonyeza nuclear codes mapema
Haujui mfumo wa vita vya nuklia! Yule anayeanza Rais wa nchi husika ndo anabonyeza nuklia codes! Mara kombora LA nuklia likirushwa sekunde hiyo hiyo upande wa pili una-detect the upcoming nuclear arsenal na automatically mfumo wa ulinzi unatambua kama wamelengwa wao na ikiwa wamelengwa wao automatically na wao mitambo yao inaachia kombora LA nuklia kuelekea lilikotoka lile linalokuja na wakati huo huo makombora ya kujihami yanarushwa kukutana na kombora LA nuklia linalokuja! Midude yote itapambana angani! Athari ya moto mtikisiko inakuwa imepunguzwa sana lakini athari ya mionzi inakuwa pale pale! Watu wanakufa bila majeraha na wanaobahatika kupona watakuwa wanazaa vilema vya ajabu ajabu! Hapo ndipo inakuja dhana ya vita vya nuklia havina mshindi! Athari ni kwa viumbe hai vyote! Ni ukatili wa kiwango cha ibilisi!
 
NK haina uchumi wa kuendesha vita na Marekani
Vita sio uchumi ndugu, vita ni akili na utayari wa watu kuingia uwanja wa mapambano kwa moyo mmoja na kwa masilahi ya nchi yao.

Haiwezi kuzuka vita leo kati ya Tanzania na Rwanda tushindwe kupigana kisa uchumi wetu uko chini kuliko Rwanda.
 
Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake, Afisa wa juu nchini humo ameiambia BBC mjini Pyongyang, ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.

''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka," alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.

Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.

Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.

Bwana Han ameiambia BBC: ''Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.
 
Siamini kama marekani anaweza vita bila kuomba msaada wa nchi marafiki. Yeye kama kidume apambane bila kuomba msaada tuone
 
Mkuu madhara ya nuclear weapons yanajulikana mkuu lakini US ndio anataka watu wa Asia Pacific makazi yao yawe ni kwenye mahandaki na sisi huku kwetu tufe kwa Radiation
Kwani Korea hana cha kupoteza na siku zote ogopa sana mtu ambae hana cha kupoteza ametengwa na Dunia toka 1962 KIM hata kusafiri sijui kama hata mkutano ya UN anakwendaga


Kuna nchi zilikuwa zinatofautiana na Mataifa mengi ya dunia na Marekani lakini mikutano ya UN walikuwa wanahudhuria. Sasa hawa wako Isolated halafu hawajali na wamejitenga na kila kitu.
They have nothing to lose, ultimately.
 
Hivi hawa hawana msuluhishaji? Acha tuone!
 
Back
Top Bottom