Korea ya Kaskazini wasema wataendelea na jaribio la silaha

Fundi mahiri wa ujenzi

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
4,039
2,585
Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake, Afisa wa juu nchini humo ameiambia BBC mjini Pyongyang, ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.

''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka," alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.

Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.

Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.

Bwana Han ameiambia BBC: ''Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.


Chanzo: BBC
 
Wanajisumbua tu..ni sawa na bondia wa uzito wa chini kutaka kupambana na ule uzito kama kina Tyson enzi zile.anakua kama anajiamini lakini anakuja kung'olewa pua
 
Mkuu hii si ya kuiombea unafikiri ikielekezwa ulipo.itakuwa je.
Mkuu madhara ya nuclear weapons yanajulikana mkuu lakini US ndio anataka watu wa Asia Pacific makazi yao yawe ni kwenye mahandaki na sisi huku kwetu tufe kwa Radiation
Kwani Korea hana cha kupoteza na siku zote ogopa sana mtu ambae hana cha kupoteza ametengwa na Dunia toka 1962 KIM hata kusafiri sijui kama hata mkutano ya UN anakwendaga
 
Mkuu madhara ya nuclear weapons yanajulikana mkuu lakini US ndio anataka watu wa Asia Pacific makazi yao yawe ni kwenye mahandaki na sisi huku kwetu tufe kwa Radiation
Kwani Korea hana cha kupoteza na siku zote ogopa sana mtu ambae hana cha kupoteza ametengwa na Dunia toka 1962 KIM hata kusafiri sijui kama hata mkutano ya UN anakwendaga
Hajawahi kusafiri. Ndiyo maana amejizira.
 
Source BBC na CNN
80c72c66026cf34d90601f963ffdf322.jpg
 
Mnakosea sana kuwalinganisha SAADAM GADAFFI na kim hawa walikuwa wananunua silaha kutoka huko nchi za magharibi N korea kila kitu wanajitengenezea wenyewe iraq waliichangia wengi kuipiga na libya vile vile
 
Air China imesema kuanzia leo inasitisha safari kuelekea Pyongyang
 
Back
Top Bottom