Korea Kusini vs Korea Kaskazini

Marconho

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
288
444
Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia 'ziara ya kihistoria' ambapo *Kim Jong-Un*, Rais wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (Korea Kaskazini) akikutana na Rais wa Jamhuri ya Korea (Korea kusini) bwana *Moon Jae-In*. Ziara hiyo ni ya kihistoria kutokana na ukweli kwamba Kim ndio anakuwa Rais wa kwanza wa Korea kaskazini, kuvuka mpaka wa kijeshi (DMZ) na kuingia Korea kusini tangu kumalizika kwa Vita vya Korea mnamo mwaka 1953.

Nchi hizo zimekuwa na uhasama wa muda mrefu sana kiasi kilichopelekea Marais wa nchi hizo wasiwe na mahusiano mazuri toka kuundwa kwa nchi hizo.

Sasa katika Makala hii, nitajadili historia ya nchi hizo. Na hasa nitalenga kuelezea imekuwaje hadi kuna Korea mbili?

Karibu!.

Kwanza Itabidi tufahamu kwamba hapo mwanzo, Korea ilikuwa *moja Tu*

Mnamo mwaka *1904 hadi 1905,* kulitokea vita kati ya dola ya Urusi na dola ya Japan *(Russo-Japanese war)*
Na sababu ya Vita hiyo ilikuwa ni kwamba walikuwa wanagombania eneo la *Manchuria* na eneo la *Korea*

Ikatokea kwamba Japan *akashinda* Vita, na Hivyo kuweza kuvamia Korea na kuanzisha utawala wake hapo.

Kwa hiyo kuanzia *mwaka 1910*, Korea ikawa chini ya Dola ya Japan. Na aliyekuwa kiongozi wa Korea *Jogong* aliondolewa.

Miaka 29 baadaye, Japan ilipigana *vita kuu ya pili ya dunia*, ikishirikiana nchi ya Ujerumani na Italia dhidi ya Uingereza, Ufaransa, marekani, china, urusi.

Lakini *mwaka 1945*, tulishuhudia vita hiyo ikimalizika kufatia Marekani kushambulia Japan kwa *silaha za atomiki* katika Miji ya Hiroshima na Nagasaki.

Hivyo Japan pamoja na washirika wake, *Wakashindwa Vita*

Hivyo basi, Japan ikaitawala Korea kwa kipindi cha *miaka 35* kuanzia 1910.

Viongozi wa mataifa yaliyoshinda vita Hiyo, hapa nazungumzia Rais wa Marekani *Franklin Roosevelt*, waziri mkuu wa uingereza bwana *Winston Churchill* pamoja na kiongozi wa China *Chiang kai shek* walikaa kikao huko Cairo, Misri.

Na katika kikao hiko walikubaliana kwamba Makoloni yote yaliyokuwa chini ya nchi zilizoshindwa vita, *YAACHWE WAZI.*

Hivyo ikabidi Japan 'ifungashe virago' na kuondoka nchini Korea.

Na katika mkutano ilijadiliwa kwambà baada ya Japan kuondoka, Korea iwekwe chini ya uangalizi na USSR na US (trusteeship).
Na ili kusiwepo mvutano baina ya nchi hizo, Korea ikagawanya katika nyuzi 38° za mstari wa latitudi, marekani ikichukua kusini kwa latitudi na USSR ikichukuà Kaskazini.

Lakini makubaliano hayo hayakwenda kama ilivyopangwa na badala yake tukashuhudia Majeshi ya marekani yakiivamia Korea wakitokea kusini.

Majeshi hayo yaliyoongozwa na *jenerali John Hodge* yaliingia Korea mnamo mwezi *Septemba 1945*

Kufatia *utawala wa kijeshi* huko kwenye maeneo ya kusini mwa korea, Wananchi walioishi maeneo hayo *walichoshwa* na utawala wa kijeshi wa marekani, hivyo kupelekea kuibuka kwa migomo na maandamano ya fujo mnamo *mwaka 1946.*

Maandamano hayo haliyojulikana kama *'Daegu Riots'* yalilenga kutaka serikali ya jeshi kuboresha Huduma za afya, maji, miundombinu, haki, n.k..
Lakini matunda hayakuweza kupatikana kutokana na *kukandamizwa* kwa maandamano hayo.

Majeshi ya Usovieti yaliwasili katika mji wa *PyongYang* mwaka 1946, na walipofika hapo wakaunda Serikari ya muda iliyoongozwa na *Kim II Sung*.
Pia katika serikali hiyo walihakikisha wanapandikiza viongozi wenye itikadi za *kikomunisti.*

Serikali hiyo ilidumu kwa muda wa miaka miwili na baadhi ya mambo waliyofanya ilikuwa ni pamoja na kutaifisha viwanda vyote vilivyokuwa vinamilikiwa na Japan, pia waligawa Ardhi kwa wakulima n.k.

Hivyo Korea ikawa inaongozwa na *Tawala mbili,* Muungano wa *Usovieti* ukiongoza maeneo ya kaskazini huku maeneo ya Kusini yakishikiliwa na *Marekani, kupitia jeshi lake*

Hali hiyo ikapelekea Mapigano na machafuko ya kila Mara baina ya pande hizo mbili, huku chanzo kikuu kikiwa ni *kugombania Mipaka*

Lakini mapendekezo hayo hayakuweza kuafikiwa na *Usovieti*, kwa madai kwamba UN isingeweza kusimamia uchaguzi kwa huru na haki.

Hivyo, serikali ya Umoja wa Usovieti inayotawala maeneo ya kaskazini mwa korea, ikawazuia UN kuingia kwenye maeneo yao kuratibu uchaguzi.

Hatimaye, kutokana na usovieti kupinga uchaguzi, iliwalazimu UN waratibu uchaguzi kwenye yale maeneo ya kusini tuu.

Hatimaye mwezi Mei 1948, uchaguzi mkuu Kwenye maeneo ya kusini tuu.

Hiyo ikapelekea miezi mitatu baadae tarehe 15 Agosti, 1948 serikali mpya ikazaliwa na ikajulikana Kama *Republic of Korea* ikiongozwa na bwana *Rhee Syngman* akiwa ndio Rais wa kwanza wa *Korea Republic*

Wiki chache zilizofata baada ya kuzaliwa kwa serikali ya Korea Republic iliyotawala kusini mwa Korea, Mara tukaona kwa upande wa Kaskazini napo, kuliundwa kwa serikali mpya.

Na nchi hiyo ikajulikana kama *Democratic People's Republic of North Korea, DPRK* na Kim II Sung, akateuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali hiyo.

Huyu ndie baba mzazi wa Kim jong Il aliyekuwa rais wa Korea kaskazini kabla kumrithisha bwana Kim Jong Un, rais wa sasa.

Hivyo kwanzia hapo kukawa na tawala za nchi mbili, DPRK au *Korea kaskazini* na Republic of Korea ROK au *Korea kusini*

Usovieti iliondoa majeshi yake nchini mwezi disemba 1948, Pia marekani nayo iliondoa majeshi yake nchini ROK mwaka uliofatia, lakini ukabakisha taasisi iliyoitwa *US Korean Military Advisory Group*, ambayo ililenga kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wanajeshi wa Korea kusini.

Kutokana na Uchu na Nia ya kuunganisha Korea zote kuwa chini ya utawala wake, Kim II Sung alivuka mpaka ule wa *nyuzi 38° za latitudi* na kuivamia Korea kusini kijeshi.

Hatua hiyo ndio ilipelekea kuanza upya kwa mapigano na hatimaye Vita ya Korea *Korean War* (1951-1953).

Katika hiyo Korean War, tuliona Korea Kaskazini Inaivamia korea kusini.

Kwa msaada wa usovieti, ilivuka mpaka na kuingia Korea kusini.

Korea Kusini ilijaribu kujibu mashambulizi, lakini ilionekana *kuzidiwa nguvu,* kwani majeshi ya Kim II Sung yalikuwa yameteka karibia asilimia 90 ya Korea kusini.

*China* ikawaonya Marekani, na kuwataka wasivuke mpaka wa *nyuzi 38° za latitude* kuingia Korea Kaskazini, la sivyo na wao *wataingia vitani* pia.

Baada ya mapigano kuendelea kwa kila upande *kuvuka mpaka* tukio lililosababisha vifo vya raia wengi, jitihada za kutafuta amani zikafanyika.

Hivyo mnamo mwaka 1953 serikali ya China, Korea Kaskazini na Marekani ziliandaa makubaliano yaliyolenga kulinda mpaka ili kuzuia majeshi kuvuka kwenda upande mwingine.

Hivyo Kwenye mpaka wa kijeshi wa hizo nchi mbili, kukatengwa eneo linalojulikana kama *Demilitarized Zone, DMZ* ambalo hakupaswi majeshi ya nchi moja kusogea hapo. Na eneo hili linalindwa na kudhibitiwa na majeshi ya ulinzi wa kila upande, Ikiwemo majeshi ya Marekani,

Hivyo kwanzia mwaka huo 1953, kuaendelea kuwapo na uhasama wa chinichini ambao ulichochewa hasa na Vita baridi kufuatia ukweli kwamba Korea kusini iliendeshwa kwa misingi ya Sera za kibepari na kusapotiwa na Marekani, huku Korea kaskazini Ikijikita na Sera za kisoshalisti ikisapotiwa na umoja wa usovieti.

Naomba kuishia Hapo.

***
Imeandikwa na
kichwa kikuu.
 
Back
Top Bottom