koo langu mie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

koo langu mie

Discussion in 'JF Doctor' started by toghocho, Jun 11, 2011.

 1. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jamani nina tatizo ambalo mwanzo sikuliona kubwa, lakini sasa naanzza kuji doubt, mwanzoni mwa february mwaka huu nilianza kusikia kooni kwangu kama kuna kitu kimekwama, nikajua kawaida labda msosi, baadae kikawa kama kinakua hivi yaani naanza kusikia kooni karia pote pamekabwa, nikaenda hospitali, dokta akanambia ni minyoo akanipa dawa za minyoo nikatumia,nikapata nafuu au tuseme nikawa sisikii tena kitu chochote kooni, baada kama ya wiki tatu, tatizo likajirudia, nikajua minyoo tena, nikanunua dawa nikameza, baadae nikapata nafuu kama wiki mbili, likaanza tena nikaenda hospitali tena april(mwezi wa nne) . nikamwelezea daktari(ambaye alikuwa mwingine sio yule wa kwanza) maelezo yote ikiwemo dawa nilizotumia na jinsi zilivyonisaidia kwa muda, akanambia tatizo langu sio minyoo, akasema ni kuchafuka kwa njia ya hewa, akaniandikia dawa kama sikosei zinaitwa broadcloax nikazitumia zikaisha nikaanza kujisikia nafuu baadae tatizo hilo likapotea, wakati nikijua limeisha miezi kama miwili baadae, kwenye wiki iliyopita nikaanza kujisikia tena tatizo hilohilo, leo nimeenda hospitali tena(ileile ya siku zote) dokta baada ya kusoma historia ya mgonjwa(patient history) eti anashangaa, mbona hilo tatizo (lako) linakuruduarudi? asa mi ntajuaje jamani si ndio maana niko hapa?
  wamenipa dawa tena, safari hii ni ampicilin na nyingine za minyoo, sasa najiuliza nina tatizo gani hasa? na nini ufumbuzi (solution) yake ya kudumu, maana inaonekana hospitali wanabahatisha na wananipa dawa za kupoza tu, sio kutibu... msaada wadau tafadhali maana hata raha sina nasikia kitu kimekwama natamani ningekimeza..yaani...wakati mwingine najisikia maumivu yaani kama nimekabwa...nisaidieni
   
 2. m

  menny terry Senior Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kunywa konyagi au valuur chupa 9 kila siku.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Duh! Pole sana jaribu kwenda kumuona daktari tofauti na huyo uliyekuwa naye.
   
 4. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  mkuu pole sana, ningekushauri umuone daktari anaedeal na mambo ya koo. Pia nenda hospitali nyingine iliiyo kubwa zaidi coz huko unakodhani kubahatisha kwa hao madaktari inawezakana tatizo ni kutokuwepo kwa vipimo maalum kwa tatizo lako hapo hospitalini, kwa hiyo wanakuwa wanatumia uzoefu tu.
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu. Kama wengine walivyosema jaribu kwenda hospitali tofauti hili waangalie tatizo nini.

  Manake bora hujue nini inasababisha hio kitu hili huweze kuepuka na hivyo vitu vinavyosababisha kuumwa kwako.

  Kila la kheri.
   
 6. Y

  Yetuwote Senior Member

  #6
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maelezo yako na unafuu unaoupata baada ya tiba vinanichanganya. Inaonekana tatizo ni lilelile lakini kila aina ya dawa inakupa nafuu! Je walishawahi kukuchunguza kooni?

  Kwanza: Nakushauri uwende hospital nyingine kwa sababu madaktari wa hiyo umeisha waona wababaishaji hata kama watakwambia la kweli hautaamini.

  Pili; Nakuomba utoe ushirikiano kwa wahudumu wa afya, acha dharau na kuwaona wababaishaji. Ukiobwa lete stool/choo wakati unaumwa kooni usikatae, peleka, ukiulizwa kwanini tatizo lako lina kurudia rudia usishangae toa maelezo alitaka kujua your life style na health seeking behaviour. Ukiulizwa umeoa toa jibu la kweli.
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,116
  Likes Received: 6,598
  Trophy Points: 280
  pole sana fuata ushauri wa wataalam, usisahau kutumia virutubisho kwani navyo ni muhimu sana. Stay blessed:cool2:.
   
 9. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Code:
  
  
  shukrani mkuu ntajaribu hii nione
   
 10. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Code:
  
  
  thaanks mkubwa
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Walevi bwana, wao muda wote wanawaza kilevi tu!!
   
 12. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pole ndugu zamani sana sikumbuki hata mwaka niliwahi kuwa na tatizo la tonsil zilinishika kisawasa baada ya daktari kunipa amplicilini nilipona then kama wiki mbili baadaye nikawa nasikia kama kitu kimenikwama kooni ( sijui kama litafanana na lako) basi nikawa najaribu kukohoa labda kitatoka wapi, nakula matonge makubwa ya ugali labda kitasukumwa wapi basi nikawa un-comfortable balaa wengine wakawa wanesema labda kimeo kikubwa nikakatwe kwa usumbufu nilioupata nikaona nirudi tena hospital. basi nilimkuta Dk. mama mmoja akaniambia hilo tatizo ni la kawaida na wala sio kimeo, kimeo hakikui, hata mimi some times hunitokea ila usihofu akaniandikia magnesium sikumbuki nilitumia siku ngapi kama wiki hivi halafu akaniambia niwe nakunywa na maziwa fresh.

  Baada ya siku ya pili tangu nianze kutumia dawa na hayo maziwa fresh tatizo likaisha sikuhisi tena kukambwa ila kwa kweli hakuniambia sababu iliyosababishwa na kujihisi huko kukabwa na sikua na udadisi wa kuuliza kama siku hizi. ila nahisi chanzo ilikuwa kuumwa tonsils.
   
 13. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pole mkubwa.
   
Loading...