shekalage
Member
- Apr 26, 2013
- 47
- 3
Msemaji wa kundi la waasi wa M23 amelaani vikali hatua ya kutofika ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mazungumzo ya amani yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana Jumanne mjini Kampala, Uganda.
Amani Kabasha amesema kuwa, kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo ya amani ili kundi hilo liweze kutoa mapendekezo kwa serikali ya Kinshasa.
Naye Francois Mwamba Tshishimbi mratibu wa kamati ya utendaji na kufuatilia mikataba nchini Kongo amesema kuwa, waasi wa M23 wanataka kuuonesha ulimwengu kwamba hawatashambuliwa na kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichoundwa kwa shabaha ya kupambana na waasi nchini Kongo. Francois Mwamba ameongeza kuwa, serikali ya Kinshasa haitashirikiana na waasi wa M23, bali itaendelea kufanya mazungumzo na mpatanishi wa mgogoro huo, yaani serikali ya Kampala.