Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Jumuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) imeandaa Kongamano la Pili la Katiba litakalofanyika katika ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumamosi, tarehe 02 Aprili 2011 kuanzia saa 4 asubuhi. Mada kuu katika kongamano hili ni: Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya.
Tangu Kongamano la Kwanza la Katiba lilipofanyika tarehe 15 Januari 2011, ambalo lilijadili kwa kina haja na mchakato wa Katiba Mpya, maendeleo mbalimbali yamepatikana kuelekea hatua za kupata Katiba Mpya, ikiwemo Serikali kukiri kwa dhati juu ya umuhimu na haja ya kuwa na Katiba Mpya. Aidha, Serikali imeshaandaa Mswada Maalumu wa Sheria unaopendekeza kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Nchi.
Kwa hivyo basi, kwa kiasi cha kutosha, mjadala juu ya haja na mchakato wa Katiba Mpya unaelekea kuitimishwa baada ya kuwa kila mtanzania mwenye uzalendo na mapenzi mema kwa nchi yetu kutambua umuhimu na haja hiyo. Hata hivyo, swala la maudhui na misingi ya Katiba Mpya limebaki kuwa tata. Kwa sababu hii, Kongamano hili la pili litajikita katika kuanisha na kutoa fursa kwa washiriki kutoa maoni yao juu ya maudhui na misingi ambayo wanafikiri ni muhimu ikazingatiwa katika Katiba Mpya.
Kwa kuwa Serikali imetoa Mswada maalumu wa Katiba wenye kulenga kutunga sheria itakayotoa mwongozi wa kufikiwa kwa Katiba Mpya, Kongamano hili pia litaupitia na kuujadili kwa kina Mswada huu.
Katika kufikia lengo hili, UDASA imewaomba na wamekubali wananchi wawili waliobobea na wenye uzoefu wa muda mrefu katika mambo ya sheria na siasa za katiba. Wananchi hawa ni Jaji Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Barnabas Samata na Ndugu Francis Kiwanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Mbali na watoa mada hawa wakuu, vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni vitapatiwa dakika 10 kwa ajili ya kutoa maoni ya vyama vyao kuhusu mada hii. Aidha, tumemuomba Ndugu Onesmo Kyauke, Mhadhiri Mwandamizi katika Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu cha DSM, kuzungumiza juu ya Mswada Maalumu wa Sheria kuhusu Katiba Mpya ya Nchi.
Tunarajia kuwa kongamano hili litatoa mwongozo kuhusu maudhui na misingi inayofaa kuwamo katika Katiba Mpya ili Katiba hiyo iwe na tija pana na endelevu katika ujenzi wa demokrasia hapa nchini na mustakabali mpya wa Taifa letu. Aidha, Kongamano hili litatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada Maalumu yatakayowasaidia wabunge kuneemesha michango yao katika kuboresha mswada huo kabla haujawa sheria kamili.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Kongamano hili, tafadhali tuwasiliane kwa simu 0754 301 908 au email kitilam@udsm.ac.tz
Wananchi wote wanaalikwa kuhudhuria kongamano hili.
Dk Kitila Mkumbo
Makamu Mwenyekiti wa UDASA na Mratibu wa Kongamano