Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Demokrasia iliomba na kupata kibali toka Mamlaka ya Manispaa ya Ilala cha kufanya Mkutano huu wa Ndani katika Ukumbi wa Anatouglo kesho tarehe 13/05/2017. Na leo tarehe 12/05/2017 jioni Kamati ya Maandalizi ilikagua na kukabidhiwa Ukumbi huo na Maafisa wa Manispaa ya Ilala.
Hata hivyo kwa mshangao mkubwa, usiku huu tumepata taarifa kwamba Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imezuia matumizi ya Ukumbi huo kwa ajili ya Kongamano hilo kwa kile tulichoambiwa ni kujitokeza kwa shughuli nyingine za Mkoa kwenye Ukumbi huo hiyo kesho.
Kutokana na hali hiyo na muda uliopo, tunalazimika kuahirisha Kongamano hilo hadi litakapotangazwa tena. Tunaahidi kutoa taarifa kamili ya jambo hili kwa vyombo vya habari mapema iwezekanavyo.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Pamoja na hayo tunapenda kuweka wazi kwamba pamoja na taasisi zingine za kiraia na kijamii, na baadhi ya watu maarufu, mwaliko wa kuhudhuria Kongamano hili ulipelekwa pia kwa viongozi wakuu wa Vyama vyote vikubwa vya siasa nchini vikiwemo CCM, CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi, ACT Wazalendo na CHAUMMA. Hata hivyo inawezekana kabisa vyama vingine vingeweza kushindwa kutuma wawakilishi kwa sababu mbalimbali.
Dr. Makongoro Mahanga
k.n.y. KAMATI YA MAANDALIZI