Kondoo mwenye pembe.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,403
KONDOO MWENYE PEMBE.


1)mbwa kapanda mtini,chura kazama majini.
Swala yumo mlimani,tembo nyuma mbuyuni.
Paa karuka angani,mbega kashuka mtini.
Na kondoo mwenye pembe,ameshusha kichwa chini.




2)simba kajificha ndani,mbuni atamba mtani.
Njiwa kabana tunduni,kinda wapo mawindoni.
Wanacho kiu kooni,wala wadudu shimoni.
Na kondoo mwenye pembe,anatazama angani.




3)farasi yule njiani,nae kasi yu mbioni.
Miguu mbele siyo chini,ya nyuma i aridhini.
Hatamu i mdomoni,n kitiye mgongoni.
Na kondoo mweye pembe,atoa nuru jichoni.





4)kuku toroka bandani,fata mbuzi machungani.
Bata yu mferejini,shingo yazama topeni.
Paka kaenda pangoni,kutambika mzimuni.
Na kondoo mwenye pembe,kashindwa kula majani.





5)nyoka ngozi mgongoni,vua gamba kisikini.
Kichwa fukia mtoni,kichwa tupa baharini.
Na kondoo mwenye pembe,kapandaje mkuyuni.




Shairi=KONDOO MWENYE PEMBE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom