CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,827
- 1,858
Ni kisa cha kweli kilichotokea miaka michache iliyopita. Ni familia moja mkoani Mbeya ambapo mme akiwa mfanya biashara mke alikuwa mama wa nyumbani. Mume alikuwa ana kawaida ya kuhifadhi kiasi fulani cha fedha ndani ya nyumba kama sh laki 2,3 au zaidi lakini hakumshirikisha mkewe kwa sababu ambazo alizijua yeye mwenyewe. Mambo yalienda vema mwanzoni, mume akiweka hela anazikuta ziko salama ukizingatia kuwa mke hakujua zimewekwa wapi.
Mambo yalibadilika pale mke alipojua mahali mumewe anapoficha hela. Sasa sijui alikuwa hamtimizii mahitaji yake au ni tamaa zake tu,mke alianza kudokoa hela za mumewe. Mume akawa anashangaa anahifadhi labda sh laki 4 atakapozichukua akafanyie kazi anakuta zimepungua labda sh elf 20 haipo. Mwanzoni alifikiri labda hakuhesabu vizuri anapoweka anapotezea. Isitoshe alijua mkewe hajui mahali anapoficha hela zake. Nani angechukua? Lakini kadri muda unavyopita kila akiweka hela anakuta 20 au 30,000 haipo. Akaanza kuwa na wasiwasi akawa makini zaidi kuhesabu hela kabla ya kuziweka lakini kila akiweka kiasi fulani kinapungua. Akajiuliza:"ndani tuko wawili kama ni watoto bado ni wadogo nani atakuwa anachukua hela zangu zaidi ya mke wangu? Atakuwa yeye lazima "
Baada ya mume kufikia conclusion kuwa mwizi wake nikewe akaamua kumuuliza:
Mme: " Ni wewe unayechomoa hela ninazohifadhi ndani?"
Mke: "Kwani mimi najua kuwa unahifadhi hela humu ndani? Uliwahi kunionyesha mahali ulipoweka hela? Nimi nichukue hela zako nimeziona wapi?"
Mme: "Sasa nani atakuwa achukua hela ndani?"
Mke: (kwa ukali) " Nitajuaje nani anachukua? Mimi sijui kwani unanikabidhi mimi?"
Mume akachanganyikiwa maana mke wake anakataa kata kata hajawahi kudokoa hela za mumewe. Lakini mume alitafakari sana akajiuliza:"Mwizi kutoka nje anawezaje kuchukua elf 20 kati ya laki 3? Kwa nini asibebe zote? Kwa vyovyote haiingii akilini lazima huyu mdokozi awe mke wangu" Akaamua ambane tena mkewe maana hela zikiendelea kupotea.
Mume: "Mke wangu sema ukweli, humu ndani tupo wawili kama ni wewe unachukua hela sema ukweli"
Mke: "Hivi baba ...unanitafutia nini? Nilishakwambia hela sijaziona unapoweka na wala sijawahi kuchukua"
Mme:" Hata ukatae lakini mimi najua ni wewe"
Mke: "Kwa hiyo mimi mwizi? Kama umenichoka si uniambie tu kuliko kunichafua kiasi hicho? Nianzie wizi kwako? Mwanaume wewe? Sijapata kuona"
Mme akazidi kuchanyikiwa mke ndio huyo anaruka juu meta 100 kwamba hajui lolote kuhusu upotevu wa hela za mumewe. Sasa mwizi nani? Lakini akili yake inang'ang'ania kwa mkewe kuwa ndiye anayemchomolea. Lakini atamnasa vipi ili aondoe utata huo? Alitafakari sana kisha akaibuka na solution ya kustaajabisha sana.
Mume alienda kununua pakti moja ya kondomu akaja nayo nyubani akachukua bundle ya fedha akaifungua akatoa zile kondomu 3 akazipachika katikati ya noti akahifadhi hizo hela ndani kama anavyofanya siku zote. Kisha akaendelea na mishe zake kama kawaida. Mke kama kawaida akaenda kudokoa hela alipohifadhi mume wake.Alipozishika,hamad!!! akakutana ma kondom 3 ziko katikati ya hela!!! Akasinyaa ghafla,mwili unatetemeka,amechanganyikiwa,akapoteza network kwa muda. Kisha: akiwa na hasira "yaani......ndio mambo anayofanya mume wangu!!! Amefanya umalaya wake hukp ameona haitoshi kaamua kuniletea kondomu ndani? Ananionyeshea? Mwache.....atanitambua!" Lakini kweli mume wake angemtambua arudipo?Ataanzaje kumuuliza kuhusu hizo kondomu? Si atahojiwa aliziona wakati anatafuta nini? Ni wazi haitakuwa rahisi kumuuliza. Kwa hiyo hata hela alizokusudia kudokoa hazikuwezekana maana zishakuwa za moto.
Mume aliporudi mke kimyaaa. Hakumuuliza chochote kuhusu zile kondom. Kwa kuwa mume wake pia hakutegemea kuulizwa,alitarajia kuona mabadiliko ya hali ya hewa kwenye uso wa mkewe ili kutambua kama ujumbe umefika. Mume alipomtazama akaona mabadiliko kisha akajisemea moyoni: "Yes message sent, time for the next step" Alienda kwenye hizo hela na kuchomoa kondomu moja akaihamishia sehemu nyingine akaendelea na shughuli zake.
Mke akaenda tena kuangalia hizo hela akakuta kondomu moja haipo zimebaki 2 akajua moja imeenda kutumika. Kapagawa, hasira zikawa mara 2 akatamani mumewe atokee ampashe lakini suala liko palepale ataulizwa alizionaje? kwa hiyo suala la kuuliza mumewe lilikuwa bado ni jambo gumu mno (wenzetu wanasema "a tough nut to crack"). Akaamua kupunguzia hasira kwa mashosti wake:
Yeye: "Mwenzenu mume wangu simuelewi, kumbe anafanya ufuska huko na sasa ameamua kunilitea kondomu hadi ndani, sijui ananikomoa? Sijui ana nia gani na mimi?"
Mashosti:" Analeta kondomu ndani? Hiyo ni dharau kubwa sana. Ulipuuliza akasemaje?"
Yeye: "Sijamuuliza"
Maahosti: Hujamuuliza? Unamuogopea nini? Akirudi leo lazima umuulize. Si atakuchezea hivyo hivyo?"
Yeye: "Sawa lazima akija leo nitamuuliza"
Mume aliporudi bibie kauchuna pamoja na mzigo wa hasira aliokuwa nao. Mume kama kawaida kacheck mabadiliko ya hali ya hewa akatambua kuwa kila kitu kinaenda sawa. Baadaye akaenda kwenye pesa akatoa kondimu moja akaihamisha. Mke alipoenda kuangalia akakuta kondomu imebaki 1. Akapagawa mtoto wa watu!!! Hasira sasa hazibebeki tena,uzalendo ukamshinda akaamua: "sasa liwalo na liwe ngoja arudi"
Mume aliporudi kadakwa juu kwa juu:
Mke:"Malaya mkubwa wewe umefanya umalaya wako huko umeona haitoshi unaniletea kondomu ndani ya nyumba?"
Mume: "Mbona sikuelewi? Umalaya umeuona wapi na hizo kondomu umeziona wapi?"
Mke:"Si umeziweka huko?"
Mme: " Wapi?"
Mke; "Si umechanganya kwenye hela uliziweka huko?"
Mme:" Eheee! Ndicho nilichokuwa nataka. Sasa nikwambie hizo kondomu mimi sijazitumia ngoja nizichukue (baada ya kuzichukua) Hizi hapa. Kwa taarifa yako niliziweka pamoja na hela ili kumnasa mwizi anayeniibia hela zangu. Sasa uniambie, ulisema hujui ninapoweka hela, sasa kondomu ulozionaje wakati nimeweka pamoja na hela? Nataka jibu sasa hivi.
Mke aliishiwa pozi kabisa. Kesi ilibadilika ghafla, mtuhumiwa akawa mlalamikaji,mlakamikaji akawa mtuhumiwa. Mke alilazimika kukiri wizi wote alikuwa anafanya kwa mumewe. Akampigia magoti mumewe kuomba msamaha. Mume alimsamehe na kutoa onyo kali kuwa mchezo huo usirudiwe.
(Hiki ni kisa cha kweli sio hadithi tu)