Kompyuta milioni moja kusambazwa kwa wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kompyuta milioni moja kusambazwa kwa wanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Oct 1, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Thursday, 30 September 2010 20:09 0diggsdigg


  Exuper Kachenje
  KATIKA kusaidia sekta ya elimu nchini, kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Dell ipo mbioni kusambaza kompyuta milioni moja kwa wanafunzi nchini ili kupunguza matumizi ya madaftari na vitabu.

  Meneja wa fedha wa Dell, Kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi, Alwin Thankachan, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa wakala wa bidhaa za kampuni yake nchini ambao umepewa kampuni ya Mitsumi.

  Kampuni ya Mitsumi pia imepewa uwakala wa bidhaa za kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Toshiba ya nchini Japan ambayo kwa pamoja na Dell watasambaza bidhaa zao kupitia Mistumi zikiwemo kompyuta, vifaa vya studio, betri na vifaa mashine ya kuhifadhia umeme (Power Sever) vya Dell na Toshiba.

  Thankachan aliyezungumza kwa kupokezana na meneja mkuu wa Mitsumi, Hitesh Shah ,alisema Dell kupitia kampuni ya Mitsumi inajipanga kuzungumza na serikali, Benki ya Dunia (WB) na wadau wengine ili kuwezesha mradi huo kuanza. "Kenya upo mradi kama huo unaendelea, tunasambaza kompyuta milioni moja kwa wanafunzi kusaidia sekta ya elimu, ikiwa ni mradi wa Benki ya Dunia," alisema Thankachan. Naye meneja mkuu wa Mitsumi, Hitesh Shah alisema,

  "Tunajipanga kuzungumza na serikali, serikali ikiruhusu, mradi huo utaanza katika kipindi kisichozidi miezi sita ijayo." Kuhusu biashara Hitesh alisema kampuni inafanya kazi katika nchi 12 tofauti baadhi zikiwa Kenya, Uganda, Rwanda, Hongkong na kuwa nia yake ni kuwawezesha

  Watanzania kuondokana na bidhaa bandia katika sekta hiyo zinazoathiri wateja na uchumi wa taifa, na kwamba wateja watakaonunua bidhaa za kampuni hizo kupitia Mitsumi watafanyiwa matengenezo bure. Akizungumzia Jumuia ya Afrika Mashariki, Hitesh alisema hatua hiyo ni ishara njema kwa wapenda maendeleo na kuwa itakuza biashara na uchumi wa nchi husika. Mwisho

  Source:Mwananchi
   
 2. H

  Haika JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  kweli kabisa ukijumlisha na zile alizoahidi kikwete shule zote naona zitatutosha, je umeme utakuwa umefika au ni za solar?
   
 3. m

  magee Senior Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  poor us.....wenzetu wanatengeneza hela sisi tunakinga mikono,toshiba na dell wanalipwa na word bank!!!
  SERIKALI ITAKUWA YA KIJINGA NA KIBOYA IKIKUBALI HILI.....BORA WAOMBE UMEME,MADAWATI,VITABU NA HELA ZA KUSOMESHEA WAALIMU PIA WABORESHE MAZINGIRA YA ELIMU.We dont need cheap things........DEL KAMA WANATUPENDA WATUPE BURE HIZO COMP NA WASILIPWE NA WORD BANK.
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  zitakuwa za solar mkuu
   
 5. A

  Alpha JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Exactly, apparently 10% of the population has access to electricity.
   
 6. t

  tajirisana Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  wana jf, ni mara ya kwanza kuingia na kuchangia hoja, huu mpango ni mzuri ila nahisi utawanufaisha wachache hususani shule za mijini ambapo hata walimu wao wanajua computer za vijijini ambao kiswahili kinatumika ila kiluga ndo zaidi itakuwaje?
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  TandaleOne,
  Mkuu wangu hizo kampuni zikisambaza Komputa utakuta kwamba thamani yake halisi ni dollar 300 kwa moja lakini tutauziwa kwa dollar 1,000 kila moja. Pamoja na kwamba ni mkopo wa Benki kuu ya dunia, tutalipa sisi (walipa kodi) na interest juu. Hivyo ni bora zaidi wananchi wakanunue Komputa ktk maduka yenye ushindani kuliko kuwapa shirika moja.

  Na kikubwa zaidi ni bora kuwapa wananchi wako ELIMU bure kuliko kununua Komputa millioni ambazo hupoteza thamani yake kwa asilimia 30 kila mwaka..
   
 8. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeongelea kitu muhimu sana.

  Tukikadiria hata kwa bei ya chini ya dola 300 kwa computer ni dola milioni 300 kwa computer milioni moja.Kama gharama ya kumsomesha mwanafunzi mmoja shule ya msingi ni Dola 20(naomba kusahihishwa hii) kwa mwaka,Dola milioni 300 inaweza kusomesha wanafunzi 2.14m kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba.
   
 9. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba computer kwa standard hiyo ya dell ni kama US Dollar 500. Hapo in maana zitahitajika dolla Millioni 500 ambazo ni sawa na Ts. billioni 750(kwa 1US$=Tsh.1500)

  Billioni 750 ni fedha ya kutosha kujenga vyumba vya madarasa 4700 kwa kila mkoa (Gharamba ya chuma kimoja = 7.5 Miln)

  **Chukua 750 bn/7.5 Mil = Madarasa 100,000/Mikoa 21 = 4700.
  Vumba vya madarasa 4700 kwa kila mkoa litakuwa limemaliza kabisa tatizo la ukosefu vya vyumba vya kusomea.


  Ni bora serikali ikafanya hivi kuliko kugawa computer kwa wanafunzi ambao kwanza utahitaji kumfundisha kingereza,kila shule kuwe na wataalamu wa IT kwa ajili ya kurepair n.k kuwe na walimu wenye utaalamu huo, vijijini hakuna umeme, Hii ni janja tu ya hawa jamaa kutuingiza mkenge na kufanya tukope deni watakalolipa watoto wetu kwa manufaa ya hawa wanaojifanya wanataka kutusaidia. Nitaishangaa serikali kama ujing huu wataukubali
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  mkuu umefanya unyambulisho mzuri.

  LAKINI umesoma vizuri hiyo habari? sio DELL kusambaza computer, ni kuhusu mitsumi kupata uagent wa dell, then wanafikiri kwa vile dell wameshafanya deal ya kuuza computer zao huko kenya kwa kutumia mradi wa world bank, then, matsun/mi or whatever that name is can explore opportunities within the government and world bank.

  CRAP!!!!!
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Je, ni brand new au refurbished
  Inawezekana zikawa zinauzwa dollar 250 watu wakauziwa dollar 500. Lakini jambo la kujiuliuliza ni TIMING ya Tangazo hili. Wafanya biashara ni opportunistics wakubwa, hapa si kama wanamuunga mkono JK baada ya kukosolewa vikali na sera za kompyuta katika madarasa ya nyasi yasioweza kuhimili hata nyaya za solar.
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  our kids in the villages need proper classrooms, desks, text books (to hell with online books coz' hata hapa mjini hakuna anyways) then qualified teachers - wa kutosha, then laboratories then other crap like computers........WHAT DO YOU THINK!!!

  Hatuwezi kuruka hatua za maendeleo........unampa mtoto computer wakati hajui kusoma na kuandika? au hajui simple east africa geography just for a starter!! and off all the things, mwalimu hakuna na kama yupo hajawahi kuiona computer
   
Loading...