GE2025 Komesha ahadi feki kipindi cha kugombea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

alexjosephat

Member
Joined
Feb 8, 2020
Posts
33
Reaction score
35
Kila mwaka wa uchaguzi, tunaahidiwa miujiza – shule mpya, ajira kwa vijana, hospitali kila kata… lakini ikishapita miaka miwili, hakuna hata kokoto moja iliyosogezwa. Na wananchi tunaambiwa tusubiri. Mpaka lini?

Ni muda sasa tuanzishe sheria mpya – sheria ya kuwalazimisha wagombea kutekeleza ahadi zao. Kama uliiahidi barabara, hospitali au ajira, basi iwe ni lazima utekeleze. Ukishindwa – si kusingizia bajeti – ushikwe kwa kosa la kudanganya umma.

Hatuwezi kuendelea kuvumilia siasa za porojo zisizo na dhamira. Wananchi si wa kuchezewa akili kila miaka mitano.

Unaonaje? Tuanzishe mjadala huu sasa. Drop maoni yako hapa chini."

Sheria ya kuwajibika kwa ahadi za kampeni ni haki ya mwananchi. Na kama kweli tunataka maendeleo – basi na viongozi wetu wawajibike kwa wanayosema. Maana maendeleo hayatokani na maneno, bali ukweli na vitendo."
 
Screenshot_20250904-083740~2.png
 
Gharama za ex ray kule mloganzila ni elfu 50
mgombea wa ccm anasema ataondoa gharama za maiti tena baada ya siku 100 kwani hizi za sasa aliweka nani?
 
Back
Top Bottom