FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
BONIFACE BIRAGE
KOMBORA KIOTANI-37
Tulipoishia Kilua agundua maadui wa taifa lake na wahujumu rasilimali za taifa.Atafanyaje kuwajua nakuwadhibiti.Je,ataweza kuwa fahamu wote waliohusika kusuka mpango wa kuisambaratisha serikali ya Kisusi?Upande mwingine tunamuona Shunie akiwa katika wakati mgumu akieleza hisia zake za mapenzi kwa mume wa rais Kilua ambaye anamkataa nakutishia kumshtaki kwa mkewe hali inayomfanya Shunie kuogopa hasira ya rais Kilua dhidi yake.Shunie anaamua kujitupa kutoka ghorofani.Je,nini kitaendelea?Tuwe pamoja.
Pambana nayo…
Shunie alipulizwa na upepo akiwa kwenye kingo za roshani ya ghorofa ya hospitali ile.Alitizama chini nakuona urefu uliomfaa ikiwa anaweza kujirusha hadi chini atafanikiwa kuumaliza uhai wake au aumie vibaya sana.Dhamira ilikuwa kuukatisha uhai au kujiweka katika hatma itakayoondoa maumivu yanayomtesa moyo.Kumpenda kwake mume wa rais Kilua ilikuwaa ghafla sana na hawezi kujidhibiti kiasi hakujielewa kabisa ilitokeaje?Yeye alkkuwa mkombozi nasio mpendaji lakini hii inaitwa ajali kazini alishajiapiza kupambana na hisia hizo lakini zimeonekana kumshinda nguvu kiasi anajikuta akizidiwa.Alijihisi mpweke sana na alijua kwa namna anajisikia hata utendaji wake wa kazi unaweza kuathirika kwa namna moja au nyingine.Aliona muhimu ni kuidhibiti hali hii kabla mambo hayajawa magumu zaidi.
Shunie alijitupa kutoka kwenye roshani wakati anajiachia tu alijikuta mkono wake ukishikwa na mtu!Ilikuwa ghafla sana mwenyewe hakutegemea kama mtu huyo angetokea kuudaka mkono wake kwa namna ile.Ukweli ulikuwa dhahiri kwamba kuna mtu alikuwa ameushikilia mkono wake wakti yeye akijiachia kutoka kwenye roshani!Mkono ulimkamata kama wa mkombozi kwa uimara na hakuwa tayari kumuachia.Alijua akadakwa leo!Aligeuza shingo kumkabili aliyeshika na kweli alikutana na Dedani akiwa amemdaka!Kumbe Dedani alimuona Shunie akiwa anaelekea eneo hilo na alijikuta nay eye akimfuata kwa kunyatanyata.Huzuni ya Shunie ilikuwa kwenye uso wake na yeyote angeusoma huzuni iliyojipaka katika wajihi wake.
Shunie alibaki kutumbua macho akimuona Dedani kama mkombozi wake aliyekuja kumfuata.Dedani alimvuta kwa haraka na kumuondoa katika hiyo hatari hiyo.Shunie alihisi moyo wake ukibubujika nakuzidi kumiminika.Kama vile ndoto ya kila mwanamke kuwepo kwa mwanaume Fulani amjie akiwa juu ya farasi katika mwanga akimpa mkono nakumshika waapande pamoja.Kuwa na Yule mtu ajaye kama mkombozi wake amsimamie siku ya uhitaji wake.Aje siku ya huzuni yake nakumpa uhakika wa kutabasamu basi Shunie aliona nyotanyota nakuhisi kumbimbi zikimcheza mauongoni.Shunie hadi anatolewa kwenye roshani nakusimama sakafuni alibaki kumpa Dedani nuru ya macho yake yaliyomuangalia bila kupepesa wala kumkwepa alimuangalia kwa macho ya kike yenye tumaini nakujaribu kuona kilichomo kwa Dedani kimejificha wapi?
“Unataka kujiua?”alimuuliza kwa ukali kidogo huku moyo ukimwenda mbio.
“Bora nife kuliko kushtakiwa kwa mkuu wa majeshi!”alisema Shunie mwenyewe alijua jinsi gani ilivyo vigumu kupambana na mkuu wan chi.Hakujielewa kama anataka kumpindua Kilua au la!
“Kifo ndo suluhu kwa akili zako za kipumbavu?”aliuliza Dedani kwa hasira?
“Ndiyo!”alijibu kwa kukata tama.
“Usiwe mjinga sasa unanipa sababu za kukushtaki!”alisema Dedani akifoka kwa hasira sana.Hakutegemea kukataliwa.
“Dedani kwanini unanichukia?”
“Sikiliza wewe mwanamke.Mimi kwasasa nipo na mke wangu chochote kilichotokea kati yangu na wewe kilisababishwa na Kavu sio riddhaa yangu na si ya kwako.”
Dedani aliondoka nakumuacha Shunie katika sintofahamu huku akifoka kwa uukali kidogo,”Sitegemei utaondoa uhai wako kisa huo ujinga wako.”alisema akikatiza korido.
Penzi la moyo wake likaitwa ujinga!Kukataliwa kulimshusha imani na mwanaume huyo.Wakati anataka kupiga hatua kuna ujumbe wa simu uliingia kwake.Alishtuka sana kiasi akajikuta akitetemeka.Ujumbe ulitokea ukweni kwake akihitajika kwa haraka sana.Alipanga watakapotoka kwenye ziara ile bila shaka angeenda.
Alirudi katika msafara wa rais.Kilua alikuwa anamaliza mazungumzo na kapteni.
“Tengeneza baraza imara la mawaziri unakipindi cha miaka kama mine hivi.Pamoja nakuwa haukuandaliwa lakini inabidi ujiimarishe kwa kipindi hiki uhakikishe hakuna kidudu mtu wa kushusha.”
Kilua alifikiria kidogo kisha akatikisa kichwa kumuelewa.
“Pitia usalama wa taifa ufanye uchambuzi yakinifu uweze kupata watendaji wazuri ambao hawadanganyiki nakuhakikishia ukipata timu nzuri nchi itakuwa salama.”alisema bwana Pangabutu.Rais Kilua alikubaliana na ushauri wake.
“Ongea na mumeo akusaidie ushauri ni mtu mwerevu sana hasa linapokuja swala la kudeal na serikali iliyofisadika anajua namna ya kuisuka.”
“Dedani mbona ni mtu wa kawaida tu?”alisema Kilua asijue jambo nyuma ya pazia kuhusu mume wake.
“Hahaha.”mgonjwa alicheka Pangabutu kisha akaendelea,”Hujajua uwezo wake ila tu nakuambia mtumie huyu atasaidia kutoa ushauri mzuri.Dedani ni ngao chache za taifa na mistake kwa the big boys kumuachia ndo maana walimteka kwanza.”
Ufahamu mpya kuhusu mumewe ulimshangaza sana Kilua kwanini mumewe ajulikane na Pangabutu.
“Ina maana Dedani ni nani?”
“Dedani ni miongoni mwa watu wachache wanaochaguliwa kuwa ngao lala za taifa ni kama kikosi maalum ambacho hukuwa-active endapo mambo yanaonekana mabovu.Ila hakikisha ulinzi wake unakuwa mkubwa sana.Mpe usalama wa taifa umlinde.”alisema mgonjwa.
“Nashukuru bwana Pangabutu umekuwa na ushauri mzuri sana kwangu.”Kilua alittamka maneno hayo nakumpa mkono mtu huyo.Ulikuwa umefika wakati way eye kuondoka.Waliagana kisha Kilua aliungana na mumewe safari ikaanza kundoka eneo lile la pale hospitali.Muda mwingi Kilua alikuwa ameushika mkono wa mumewe.Alijiegeza ubavuni mwake.Dedani alikuwa mbali sana kimawazo.
“Leo nimegundua mambo mengi sana.”alisema Kilua.
“Nadhani umeelewa nchi inapoelekea.”alisema Dedani.
“Naomba ushauri ni jambo gani nifanye.Nahisi kuzidiwa.”
“Kwasasa tengeneza baraza la mawaziri kwanza.Pia teua makamu wa rais pamoja na waziri mkuu.Tunatakiwa tuone nani anapaswa kuwa makamu kwa sasa nafasi hizi zimeonekana kuwa wazi kwa kipindi kirefu.Inatakiwa wawekwe kwa haraka.Pia kuna maeneo yanahitajika kufanya uchaguzi hasa kwa wale waliopoteza viongozi wao.Tuarudi kwenye mtandao wa utawala.”
“Kweli umesema kitu ambacho sijawahi kukifikiria.”
“Pia kumbuka lazima ujiimarishe kwenye chama chako cha kisiasa.Sio kwamba chama kinaridhika na wewe.Lazima na wao wanajipanga kivyao.Je,utawala wako unakomea miaka mine hii ya urithi kabla hujagombea au una mpango wakuachia madaraka punde utakapo fikia mwisho wa muda?Umejua siri nyingi za nchi kwa namna yoyote yapo ambayo yatahitajika wewe binafsi kuyasimamia na kushughulikia.Kwasasa huna wa kumjibia maana umepewa lakini jipange kuudhibiti utawala.”
Dedani alikuwa anamfundisha mkewe kutawala nchi na hatua za kuchukua.Ikulu itakuwa bize sana kutoka sasa hasa anapoandaa baraza la mawaziri pamoja na makamu wa rais akiongeza na waziri mkuu.Ni wazi kwa hatua hiyo atafanikiwa kutengeneza mtandao wa kiutawala utakaokuwa imara.Ilikuwa kazi ngumu lakini yenye manufaa.
“Dedani nataka usimamie jambo hili.”
“Nikiweka makucha yangu sana watasema unaleta ufamilia kwenye uongozi.”
“Wewe ndo ninayekuamini hakuna mwingine.”alihakikisha rais Kilua.Muda ule walifika ikulu.Kilua aliitisha kikao kuhusiana na hatua anayotaka kuichukua.Kutakuwa na mabadiliko makubwa sana kiutawala kuna mengi yanaenda kubadilishwa ili kuusimamisha utawala wake.Aliihitaji kwanza kuanza na hawa wa juu ikiwemo makamu wa urais.Majina kadhaa yalianza kupita Dedani alikuwa makini katika hilo akihakikisha atalishughulikia jambo hilo ila yeye alijiweka kama kivuli.Serambovu alijua hii ni fursa ya wao kupandikiza watu wao katika utawala wa Kilua.Japo Kilua hakuwa na maono yakuendelea na kazi hiyo lakini sasa aliona kuna haja ya kuendelea na kazi hiyo na tena aifanye kwa umakini wa hali ya juu kuliko hata mwanzo.Kulikuwa na uozo mkubwa sana.Kilua alijiapiza kama mabaradhuli hawa walifanikiwa kuigusa familia yake ilitakiwa alipize kisasi maalum na njia pekee ni kuwadhibiti katika utawala wake.
***
Kilua alikuwa na kikao cha siri pamoja na moja ya wanajeshi wake.Kikao hiki kilikuwa mahsusi kikiongozwa na Kilua pamoja na Kanali Pasua,”Nataka nifanye jambo la hatari sana.”
“Kuna meli ipo bandarini na kwa muda sasa haijafanyiwa clearance.Mara kadhaa wametaka kupata kibali kutoka ikulu.Meli hii siyo nzuri kwa uupande wetu.Kuna watu wanashikiana na wamiliki wa meli hii kunifanyia hujuma lakini binafsi ninampango wa kuwakomesha.Nataka meli hii ilipuliwe.”
Ilikuwa kauli nzito sana kwa rais KIlua kuitoa.
Wote walibaki kutumbua macho.
“Kwani mheshimiwa hakuna namna nyingine ya kushghulika na jambo hili hadi ifikie hatua ya kutumia nguvu kiasi hiki?”
“Watu hawa wamejidai wana nguvu sana kiasi cha kutaka hata kunitikisa mimi binafsi.Ninawachukia kutoka moyoni na lazima nitume ujumbe kwamba na mimi najeuri.”
“Kwani mheshimiwa hii meli ina nini?”
“Kilichomo ni mitambo ya kuchimbia mafuta inayokuja kutumika nchini kwetu.Hadi sasa hakuna maelezo yoyote yaani wanafanya jambo hili kimyakimya kana kwamba nchi hiii ni ya mama zao.”
“Huoni jambo hili ukifuata utaratibu wa kisiasa utaweza kuwadhibiti.”
“Kabla halijafika huko nataka kuwatikisa.Nataka bomu litegwe lilipue meli nzima na kila kilichomo kiwe majivu.”
“Lengo hasa ni nini?”
“Natuma ujumbe kwao kwamba nipo macho.”
“Tukiilipua meli ikiwa pale bandarini tutegemee maafa makubwa sana kwa bandari na meli zilizoegeshwa jirani.Pia kutaonesha bandari yetu si salama ikiwa milipuko tena ya mabomu inatokea.Hiii ni ishara mbaya sana.”
“Kwa vyovyote watu hawa wamejipanga kulinda kilichomo kwenye meli yao.Lazima watajua tu kwamba meli yao imelipuliwa kwa bomu.”alishuri Dedani.
“Mnafikiri tufanyeje?”aliuliza Kilua.Kilua ni mbabe kiasili alitaka kuwatia hasara kwa kuharibu meli yao.Hadi sasa binti yake anasota mikononi mwa hao afriti.
“Tukiichukulia hatua kwamba meli yao haina vibali au tuifukuze binti yangu atakuwa mashakani.Lakini tukiipiga kimyakimya pia waatajua ni mimi na bila shaka watamchukilia hatua kama kisasi.”
“Nitaomba wote muende mkafikirie mkirudi nataka jibu la maana hapa mezani.”
Walipitia ajenda nyingine katika kushughulika na jambo hilo kisha kikao kikaisha na watu kutawanyika.Wakati wanaondoka Kilua alipokea ujumbe wa simu ulioambatana na picha ya binti yake akiwa kwenye huzuni kali sana.Ujumbe ulisomeka hivi,”TURUDISHIE MUMEO LA SIVYO MWANAO TUTAMSHUGHULIKIA.UNA MASAA 24 KUAMUA.”
Kilua alihisi moyo kwenda mbio sana.Dedani alimshika mkono mkewe kisha akampeleka hadi pembezoni nakuamua kumsaili.
“Una tatizo gani?”alisema Dedani akimuangalia mkewe kwa umakini wa hali ya juu.
Kabla Dedani hajajibu na yeye akasikia ujumbe kwenye simu.Aliufungua kwa haraka alichokutana nacho kilikuwa cha kutisha.Alikutana na ujumbe mfupi ulioambatana na video fupi akaifungua nakuona ni tukio lile akiwa faragha na Shunie.Mwili wote ulipika mkambi halafu kuna ujumbe unasomeka hivi wa maneno,”TWALIPO NDO MAKAMU WA RAIS VINGINEVYO VIDEO ITAFIKA KWA MKEO.”
Dedani aliduwaa nakhisi mwili wote kufa ganzi hakutaka kumfedhehesha mkewe kwa video ile wala kuitia aibu familia yake.Ni kitu kilichomkera sana.Kumleta mtu huyo kwenye serikali ya Kilua ni kuleta tena kundi lililofisadika.
***
Shunie aliwekwa kati huko ukweni tayari amekwisha semwa kwamba amekuwa mbali na mchumba wake bwana Pablo ambaye ana majeraha makubwa sana.
“Tangu mwenzako awe mgonjwa hujaenda kumuuguza kwanini?”
“Kazi hata mimi nilikuwa kwenye matatizo makubwa na tangu nitoke huko sijapata muda wa kuwa huru kila mara nimekuwa nikiitwa na rais kupeleka ripoti.”
“Hata kama lakini simu hujapiga wala kuuliza chochote.Familia ilikwisha kaa kikao tukapanga Pablo akitoka hospitali harusi yenu ifanyike ndani ya mwezi.Hebu ingieni kwenye ndoa haraka mpate watoto.”alisema baba Pablo.
Shunie alikwisha poteza ndoto ya kuolewa kabisa.Hakuwa na taarifa kama Pablo alikwisha toka hospitali na sasa anaugulia nyumbani.Hata kwenye kikao hiki hakuwa na habari kwamba Pablo alikuwepo nyumbani .
“Lakini baba sioni umuhimu wakuifikiwahi kufunga harusi wakati bado tuna majukumu mengi ya taifa.”
“Unajua kuna maswali kama familia tunajiuliza sana ni kwanini wewe haupo karibu na mchumba wako.Imekuwa kama nii yeye analazimisha ndoa hii.”
Shunie alihisi kubanwa ukweni.
“Hapana baba.Nina operesheni maalum kwasasa sitakuwa na nafasi maalum ya kushughulika na ndoa.”Shunie alitoa kauli hiyio wasiwasi ukimshika nakumtafuna ini na moyo ukweli hakuweza kuikabili.
“Msichana mbona kama hatukuelewi?”
Akasikia mtu anaguna kwa nyuma.Ile anageuka kutizama akakutana na Pablo akiwa kwenye kiti cha magurudumu.Pablo alisikia kauli ya Shunie kuipeleka harusi mbele.Uso wake ulivaa huzuni sana kitendo kile kilimpiga fedheha.
Shunie alijikaza kisha akasema,”Sorry sipo tayari kuendelea na ndoa kwa sasa.”
Pablo alitizama tu bila kusema chochote huku machozi yakimtoka.Shunie aliwaza kunywa sumu saikolojia yake ilikuwa imeharibika.