FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI-32
BONIFACE BIRAGE
Kilua alikuwa akilipapasa tumbo lake huku akijiangalia kwenye kioo.Tayari alikuwa ametuma watu wamlete Serambovu ofisini kwake muda mfupi uliopita.Sasa alipokea taarifa tena kwamba mummewe kapatikana na yupo njiani kuletwa ikulu.Alikuwa na kibarua kigumu sana kumkabili mumewe.Japo alipata faraaja nusu kwani bado mwanaye hajapatikana.Ujio wa Dedani ni jambo lenye kheri isiyo na shari,lakini upande wa pili alikuwa na kibarua kigumu sana.Kilimshinda akili yake kiasi aliona chungu na joto ya jiwe.Kulikuwa na wingi wa maswali.
Kioo hakikudanganya mama kwani alizini na kuzinika akapata ujauzito ambao kwa hakika si wa mume wake bali ni mtu mwingine kabisa.Kkujieleza halikuwa jambo dogo na pengine angezua shutuma kubwa zaidi a zile za mwanzo.Kulikuwa na mgogoro wa kidiplomasia kati yake na rais wa Savanna lands ambao ulionekana utakuwa na mlolongo mrefu hadi utakapo kamilika na hadi sasa ameshaandaa timu ya wanadiplomasia kuandaa makubaliano yakuingia baina ya mataifa hayo. Makubaliano kwa manufaa ya taifa lolote.Hii ingeepusha mzozo kwa vizazi vijavyo.Ilikuwa njia bora kulinda mengi ambayo yalionekana kuwa na faida hapo usoni.
Kwenye lindi la mawazo mlango ulifunguliwa. Akaingia moja ya wasaidizi wake.Nywele zzilicheza kwa kusimama akihisi kuna sintofahamu fulani zilizochimba kuta za moyo wake huku akijifikiria yeye na mustakabali wake dhidi a jambo linaenda kujiri.Dakika zile alikuwa amewasili asiemtegemea kama angekuja.Pengine ujio wake ulionekana kama taswira ngumu kuipata lakini yametimia mbele zake.
“Mheshimiwa mumeo amewasili ikulu.”kwa heshma mlinzi yule alitamka kauli ile huku uso wake ukionesha utiifu wa hali ya juu.Utii usio na shaka wala mashaka yoyote!
Kilua aliitikia kwa kutikisa kichwa.Ila kabla ya kauli alishtushwa na msaidizi wa pili kuingia akiwa pamoja na Serambovu huku akiwa chini ya ulinzi mkali sana.
***
Zee Kavu alikkuwa ameshika tama usso kuwa umesawijika kwa namna binti Shunie alivyomchezea karata dume na kumharibia mipango yake kuipanga upya siyo mzahaa wala kitu cha kuchekelea.Alitakiwa awe imara na kuja na mbinu mpya kumdhibiti rais Kilua.Kuwepo kwa Dedani mikononi mwake ni hatari kubwa sana kwa zee Kavu.Japo mtoto wa Kilua yupo kwake lakini siyo dhamana ambao ingedumu kwa namna moja au nyingine.Kilua atapata ujasiri zaidi hasa akiwa mumewe yupo pamoja nae.vile baba karudi na nguvu pia ya kumtafuta Kavu itaongezeka hasa kwakuwa Dedani alikuwa katika ngome ile alijua chungu zote wala humdanganyi kitu na hilo litaweka kisasi.Pengine Dedani atakuwa wa kwanza kutumia vyombo vya usalama kumuwinda zee Kavu.Ataipindua ardhi ya Kiota juu chini ili huyu afriti kibiriti awe chambo.
“Hatua ya Shunie inatuweka mashakani sisi sote.Huu ni uzembe wa hali ya juu kuwahi kutokea.”alianza mr Tufe lawama haziepukiki.Kila njia inapofeli basi yupo wa kuvishwa lawama hizo. Uwanja mzuri wa kumimina kuchuja na kupembua.
Zee Kavu alimeza shutuma hizo.Alijinasua kwa kujitetea.
“Jamani mimi sikujua kama binti angefikia hatua hiyo.”
“Wazo lakutengeza mahojiano kwa lengo la kumchafua Kilua ni feki tena upumbavu wa hali ya juu sana.”mr.Tufe alizidi kupigilia msumari wa moto hilo tosha ni mwiba kwake.
“Tumeona hilo japo lilikuwa wazo zuri lakini lilipangwa kizembe.Kavu huku waandaa mateka wako vilivyo.Ulitakiwa uongeze bidii kwenye mpango.”
“Yule msichana ni mjanja ni mjanja tena sana.”
“Na sasa yupo nje.”
“Uhuru wake ni hatari kwetu.”
“Tena kubwa sana.Si ajabu wanajipanga na sasa Kilua atakuwa hatari zaidi siri zetu zinagundulika kwa uzembe huu.”
Ni wazi timu nzima iliona mambo sio rahisi tena.
“Tena the big boys Tumepakwa Tope kwa jeuri yake.”mwingine aliongeza.
Chumba kilitokota kwa kutota lawama ambazo zilionesha ni kweli the big boys wamekubali kudharauliwa na bibie Shunie jeuri.
“Kulaumiana haita mrudisha bwana Dedani mikononi mwetu wala kuondoa mistake iliyotokea bali ni kujilisha sumu ya majuto.Ni kheri tujipange kwanza inatakiwa tumshurutishe rais Kilua afanye tunachotaka sisi la sivyo tutamzimisha mwanae tena kwa mateso makubwaa sana.’’ Alishauri bwana Tufe.
Hoja hio ilipokelewa kwa hisia mseto.Kuna walioiona kama ni njia bora kuzidisha urefu wa makucha yao na wengine waliona kama kujipeleka kijinga itaonekana fika kwamba wanashindana nae.Mashindano ambayo hayaeleweki kabisa kwamba dhamira kuu ni nini?
“Kufanya hivo sioni mantiki husika hasa ni nini?Tayari tunamdhibiti vya kutosha…”
“Kilua hatuja mdhibiti nyota yake ina ng’ara sana.”
“Kumuacha aipate familia yake ni sisii kujilisha upepo.”Kavu alisisitiza.
“Bila uzembe wako haya yasingejiri.”
Akameza dabali moja ya shutuma tena.Kavu hasira zilijipanga kwenye lindi lake la lawama huku akijiapiza kulipiza kisasi cha uhakika kwa uchafu wa dharau Shunie aliomuonesha ubabe wa kimataifa
Akakumbuka zile picha za video alizozirekodi wakati binti huyo akiwa faragha na Dedani.Hizo ni salaha bora kwake kuzitumia.
“Niachieni Shunie nitamdhibiti mwenyewe.”
Wote wakabaki wakimshangaa.Lakini jibu alikuwa nalo mwenyewe.
“Ok tunakupa nafasi yamwisho dhibiti huyo malaya.”alisema bwana Tufe ambaye alishajua Shunie wanaemzungumzia hapa ni msichana ambae ni mchepuko wake wa muda mrefu na kama akikiri hilo bila shaka itaonekanaa amekuwa akiuza siri zao kwa kutembea na mtendaji wwa usalama wa taifa.Ina maana Shunie amekuwa akimfanyia ushushushu wa muda mrefu sana na siajabu kuna siri nyingi sana zinajulikana dhidi yake.
Inamaana hata meli yao ilipovamiwa na wale maafisa usalama hadi Shunie kukutwa ni kupitia yeye ndo siri ikajulikana haata maongezi mengi ya simu amekuwa akiyafanya mbele za mlimbwende huyo.Ni wazi sasa wamekuwa wakifuatiliwa na serikali bila wao kujua.Bwana Tufe alitamani kuwaambia wenzake hofu yake lakini akaona akifanza hivyo nikujionesha jinsi alivyo mzembe kiasi cha kuuza siri kwa nduli wake.Pengine big boys watamchukulia hatua kali za kinidhamu.Tayari Kavu kesha ondolewa jicho moja na Shunie sio mchezo tena kwamba Shunie aanaacha makovu.Kaacha kovu kwa zee Kavu kwa kumtia chongo la maisha pia mr Tufe kawekwa kovu kubwa la kufanyiwa ushushushu wa muda mrefu.Makovu hayaa ni hasara tupu.
“Nitamshughulikia vilivyo.”alihakikisha zee Kavu.
“Namtaka balozi wa Savanna Lands anyamazishwe yeye pamoja na Serambovu wametupaka tope kwa shambulio la kizembe sana.Serikali iemedhibiti na tayari balozi yupo mikononi mwa serikali.Serambovu naskia kawekwa kizuiizini ni kwamba Kilua ameshtukia mipango yetu.”
“Lengo la shambulio wanadai ni kutikisa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Savanna lands na Kiota.Kweli wamefanikiwa kwa namna moja au nyingine na hii ni mbinu ya kumshtua rais wa Savana lands alionekana aking’ang’ana kudhibiti ishu 13:14.Alitaka kuingilia na ndo maana Serambovu na balozi wa Savanna lands waliamua kutekeleza jambo hilo kupitia balozi wa Savanna lands japo Serambovu hakuwa na uhakika wa dhamira lakini wakubwa walichonga huo mpango.Tena naskia hali imekuwa mbaya sana kwa rais wa wa Savanna lands.”
“Kwani hakujua shambulio hili?”aliuliza mr Zungu.
“Iwe alijua au hakujua alikuwa sehemu ya big boys lazima akutwe na kadhia hii.Iwe fundisho kwa wote ukileta kidomo utamalizwaa naskia hata alizuiwa kuondoka Kiota na sasa mataifa yanampeleleza.Wakati aangaika kujisafisha sisi tutakuwa hatua nyingine kabisa kimipango.”
Ilidhihirika kuwa shambulio la kwenye msiba lilikuwa la kupangwa na wakubwa wanaojiita Big boys.Wazee wezito wampango wa faili nambari 13:14.Sasa hali ilikuwa tete kwao kumbe unaeza ukageuka kwa tukio kuundwa illi na wewe uchafuliwe pamoja.Rais wa Savanna lands walimtengenezea zengwe la shambulio akiwa katika ardhi ya Kitoa kwa kumhusisha balozi wake huku silaha zilizotumika zilionekana kutokea taifa lake kuja Kiota.Sasa alikuwa katika hatia kubwa zaidi ya vile alivyodhani.Kuhusishwa kwake na shambulio ni muunganiko wa doti za lawama na kweli wamefaniikiwa pakubwa kwa hilo kiasi cha mzimisha kabisa.Big boys wamemtuliza bwana huyu.Mr Tufe aling’ata meno kwa dhihaka ile.
“Ukijidai unajua unazimishwa.”
Wote waliwaza sana dhidi ya tukio lile.Uchonganishi mkubwa sana ulikuwa unafanyika baina kundi la Big boys na vibaraka wao.Kundi hili lilifanikiwa hata kuleta mgogoro wa kidiplomsia kati ya taifa la Kiota na Savana lands.Kundi hili ndo chachu ya yote.
** *
Katika chumba cha hospitali alimolazwa balozi wa Savanna lands anaonekana nesi akiingia chumba hicho.Mashine za kupumulia zikiwa zimefungwa vizuri puani mwake.Nesi alifika akiwa ni chano cha madawa safi na nadhifu.Aliviweka kando huku akichukua sindano nakuvuta dawa fulani kwenye kchupa kisha akaiminya kidogo dawa iliruka kidogo.Akamshika mgonjwa mkono akautafuta mfupa halafu kwa umakini akamdunga sindano.Ndani ya dakika kumi mgonjwa alianza kutapatapa huku ngozi ikibadilika nakutoka vitu kama majibu huku vikitumbuka halafu akatikiisika kisha alijipigiza kwenye godoro lake kichefuchefu na tumbo kusokota vilipelekea balozi kuapika damu ambayo ilifurika kwenye kifaa cha kupumulia kikaajaa top!
Mashine ya kukagua mapigo ya moyo ilitoa mlio wa ulalamishi na ghafla ikazimwa na yule muuguzi.