Kombora jingine la Korea Kaskazini lafeli majaribio

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
_95838380_northkoreamissile.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump ameishtumu Korea kaskazini kwamba imeikosea heshima China, mshirika wake mkuu, kwa kufyatua kombora la tatu katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kwenye ujumbe wa Twitter, bwana Trump amemsifu rais wa Uchina, Xi Jinping.

Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema jaribio hilo lilitibuka, kwani kombora hilo lilianguka punde tu baada ya kupaa angani.

katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Rex Tillerson, ameonya kwamba huenda kukaibuka majanga mabaya sana iwapo miradi ya Kim Jong Un ya kutengeneza zana za kinyuklia na makombora ya masafa marefu hiatositishwa.

Maafisa wa Marekani wanasema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka.

Hii ni ishara kwamba Korea Kaskazini haina ujuzi wa kutosha kiteknolojia, ama pia huenda ikawa Marekani imepata mbinu ya kuingiilia mifumo yake ya teknolojia.

Maafisa wakuu wa Korea kusini na Japan wamekashifu vikali majaribio ya hayo.

Msemaji wa wizara ya mabo ya nje wa korea kusini anasema Pyongyang inacheza na moto.

Msemaji wa serikali ya Japan anasema jaribio hilo ni kinyume na mapendekezo ya umoja wa mataifa.

Gazeti la the Newyork Times, linasema kwamba Marekani imeweka virusi kwenye kompyuta za kijeshi za Korea kaskazini, japo madai hayo yanatiliwa shaka.

Haya yanajiri siku moja baada ya Marekani kulaza wazi mikakati yake ya kukabiliana na Korea kusini ikiwemo kuanza vita dhidi ya taifa hilo, na kutoa ahadi kwamba serikali ya Kim Jong un haitapinduliwa iwapo atasimamisha miradi yake ya kutengeneza zana za nyuklia na makombora ya masfa marefu.

Korea Kaskazini imefyatua makombora 75 tangu rais Kim Jong un aanze kutawala
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kwa hiyo mnafurahi sana wenzenu makombora yao yanavyofeli?

Kwa taarifa yenu anarudi tena Maabara kuboresha zaidi.
 
Hawa jamaa wanajitutumua tu hawana uwezo mkubwa kuliko wanavyojitutumua. Gwaride la mjuzi limebainika kujumuisha silaha za bandia kwa mujibu wataalamu wa mambo ya ujasusi..:D:D.. Yaani uwezo wao ni mdogo kuliko ule wanaotaka dunia ione.
 
Hawa jamaa wanajitutumua tu hawana uwezo mkubwa kuliko wanavyojitutumua. Gwaride la mjuzi limebainika kujumuisha silaha za bandia kwa mujibu wataalamu wa mambo ya ujasusi..:D:D.. Yaani uwezo wao ni mdogo kuliko ule wanaotaka dunia ione.
Watu wenye akili tuu ndo watakuelewa,.Wale mashabiki wa mirengo hawaezi elewa.
 
Huyu kiduku anapapara sana. Take my word. NK imejitengenezea mazingira ya kushambuliwa kwa kutumia teknolojia na watu walio na Suti maabara. Kamwe hatafanikiwa kwenye Vita hii maana kwa akili zake mbovu anadhani yeye ndiye muumbaji wa ulimwengu na kwamba anaweza kuifanya dunia atakavyo. Ataadhirika zaidi ya ilivyokuwa kwa Saddam Hussein.
Pia lazima ieleweke kwamba wataalam wa NK hawawezi kuwa na akili tulivu kwanza kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa kiduku na pia ulimwengu uko kwenye sala za kuwapofusha na kudumaza akili zao ili kuepusha maafa kwa dunia.
Nasema kamwe kiduku hawezi kuinuka. Ataadhirika.
 
兵者,詭道也。故能而示之不能,用而示之不用,近而示之遠,遠而示之近。
All warfare is based on deception. Hence, when we are able to attack, we must seem unable; when using our forces, we must appear inactive; when we are near, we must make the enemy believe we are far away; when far away, we must make him believe we are near.
 
Hawa jamaa wanajitutumua tu hawana uwezo mkubwa kuliko wanavyojitutumua. Gwaride la mjuzi limebainika kujumuisha silaha za bandia kwa mujibu wataalamu wa mambo ya ujasusi..:D:D.. Yaani uwezo wao ni mdogo kuliko ule wanaotaka dunia ione.
Kwa hyo wanatafuta kikii?
 
知己知彼,百戰不殆。 ( Zhī jǐ zhī bǐ, bǎi zhàn bù dài. )
If you know both yourself and your enemy, you can win numerous (literally, "a hundred") battles without jeopardy.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
故曰:知彼知己,百戰不殆;不知彼而知己,一勝一負;不知彼,不知己,每戰必殆。
So it is said that if you know your enemies and know yourself, you will not be put at risk even in a hundred battles.
If you only know yourself, but not your opponent, you may win or may lose.
If you know neither yourself nor your enemy, you will always endanger yourself.
 
Kwa hyo wanatafuta kikii?
Ni mbinu moja wapo ya kijeshi...Imekuwa inatumika na mataifa mengi sana....Ni njia ya kumfanya adui atafakari mara mbili kwa hiyo kuepusha vita has kwenye mazingira ambayo unaona anayetaka vita na wewe ni powerful zaidi yako kwa hiyo njia ni kumtishia ili ajue kwamba wewe si wa mchezo mchezo..Ilitumika sana toka enz za vita kuu ya pili ya dunia. Mfano ujerumani walikuwa wan vifaru vya bandia ili kuwachanganya marubani wa ndege za kivita
 
Back
Top Bottom