Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
INAONEKANA kuna baadhi ya watu wenye dhamira ya kweli katika kuhakikisha mashindano ya soka ya kuwania Kombe la Mapinduzi yanafanyika kila mwaka na yanakuwa yenye hadhi.
Kwa hali ya kusuasua iliyojitokeza mwaka jana, ni dhahiri kwamba matarajio ya wengi ni kwamba mashindano hayo mwaka huu yasingefanyika au yangefanyika kwa hali ile ile.
Tuseme tu kwamba hakuna au kama wapo ni wachache mno waliotarajia kuziona timu za Yanga, Simba, Mtibwa na Azam zikishiriki mashindano hayo mwaka huu.
Hata hivyo katika hali ambayo wengi wetu hatukuitarajia ni kwamba timu hizo zipo Visiwani Zanzibar zikipambana katika kuliwania taji hilo.
Awali fikra za wengi zilikuwa kwamba timu hizo zingeendelea na mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Bara kama ilivyopangwa lakini ghafla mambo yalibadilika na ratiba ya ligi ikafanyiwa marekebisho.
Kinachoonekana ni kwamba hata Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halikutarajia kwa timu shiriki za Ligi Kuu Bara kushiriki mashindano hayo mwaka huu na ndio maana hayakuwapo kwenye kalenda ya shirikisho hilo.
Tuliwahi kuzungumza katika maoni yetu siku zilizopita juu ya umuhimu wa TFF kuongeza mashindano ili wachezaji hasa wa timu za Ligi Kuu wapate fursa ya kushiriki mechi za ushindani.
Mechi 26 ambazo wachezaji hao wanashiriki ni ndogo hasa kutokana na ukweli kwamba ni sehemu ndogo mno ya wachezaji wanaopata nafasi ya kushiriki mechi hizo wengi wao huishia benchi msimu mzima.
Hali hiyo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wachezaji kushiriki mechi za mitaani au Ndondo na kujikuta wakiingia katika migogoro na viongozi.
Kwa mantiki hiyo Kombe la Mapinduzi inaweza kuwa fursa nzuri ya kuongeza mashindano ya soka yenye ushindani na ambayo yana maana kubwa kwa soka la Tanzania.
Kombe la Mapinduzi pia lina maana kubwa kwa soka la Zanzibar ambalo Ligi Kuu yake ipo chini na hivyo wachezaji wanahitaji ushindani kutoka nje ya Zanzibar ili kuinua vipaji vyao na wengine kupata ulaji kwenye timu nyingine zenye maslahi zaidi.
Tangu kufutwa kwa Ligi ya Muungano, timu za Zanzibar zimekuwa hazipati changamoto na wapo wanaoamini kuwa hiyo ni sababu ya timu hizo kutolewa katika hatua za awali kwenye Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ni dhahiri kwamba katika mazingira ya aina hiyo, michuano ya Kombe la Mapinduzi inaweza kuwa na maana kubwa katika soka la Tanzania kwa ujumla kama itaendelea kuwapo.
Hata hivyo tungependa kuona michuano hii ikiboreshwa na kuwa yenye hadhi ambayo Wazanzibari, Watanzania na wapenda soka wangependa iwe.
Hilo litafanikiwa kama kutakuwa na maandalizi ya mapema, kwamba waandaaji waanze maaandalizi ya mashindano ya mwakani mara baada ya mashindano ya mwaka huu.
Timu za nje zinazofikiriwa kualikwa zijulikane na ziarifiwe mapema ili zijipange, TFF nao waarifiwe mapema ili katika kalenda yao watambue uwepo wa Kombe la Mapinduzi.
Wadhamini wa mashindano waanze kutafutwa sasa na si kutegemea serikali au kutafuta wadhamini mwezi au wiki moja kabla ya mashindano.
Hayo yakifanyika ni wazi kwamba Kombe la Mapinduzi litakuwa na hadhi na lenye manufaa katika maendeleo ya soka la Tanzania.
Tahariri MwanaSpoti