BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Posted Date::11/13/2007
Soka:Kombe la Dunia Afrika Kusini katika hatihati
LONDON, Uingereza
Mwananchi
NDOTO ya Kombe la Dunia kufanyika Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 2010 imeanza kuingia majaribuni baada ya wenyeji Afrika Kusini kueleza kuwa hawawezi kukamilisha kwa muda unaotakiwa ujenzi wa viwanja viwili kati ya saba vinavyohitajika.
Kukiri huko kwa wenyeji, kumezua hofu kwamba huenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) likaangalia uwezekano wa kuhamisha kwingineko fainali hizo.
Afrika Kusini, imeeleza kuwa ujenzi huo utaathiri pia kufanyika kwa michuano ya Kombe la Mashirikisho ya Soka mwaka 2009 katika Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth.
Wenyeji hao, hata hivyo wanaeleza kuwa hakuna sababu ya kuwa na hofu ya kufanyika kwa fainali hizo, ingawa wanakiri ujenzi unasuasua katika Uwanja wa Green Point jijini Cape Town.
"Hakikisho ambalo tuliwapa Fifa limewatosheleza, tunajivuna kwamba Uwanja wa Soccer City ulioko Soweto, utakabidhiwa miezi mitatu kabla ya muda uliowekwa," alisema Tim Modise, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Mwaka 2010.
"Mambo yanakwenda kama yalivyopangwa, ingawa viwanja viwili, ratiba yake ni ngumu, ngumu sana. Uwanja wa Nelson Mandela Bay ndio uliochaguliwa kwa michuano ya mashirikisho mwaka 2009, jambo ambalo linainyima raha kamati ya maandalizi, kiasi kwamba miezi miwili ijayo itajulikana iwapo michuano hiyo itafanyika hapo au la.
Wakuu wa sekta ya utalii wanakadiria kuwa watapokea wageni 450,000, wengi wao wakiwa mashabiki ambao watafika kwa ajili ya kuona fainali hizo na kutumia kiasi cha dola 1.6 bilioni.
Tatizo jingine ambalo linaisumbua nchi hiyo ni kiwango kikubwa cha uhalifu, ingawa Mtendaji Mkuu wa Utalii nchini Afrika Kusini, Moeketsi Mosola anakiri kuwa baadhi yao watazuiwa kuingia nchini huko.
Afrika Kusini inatarajia kutumia askari polisi 140,000 hadi 190,000 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kufanikisha fainali hizo."