Kombani: Sitegemei kufukuzwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombani: Sitegemei kufukuzwa kazi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,504
  Trophy Points: 280
  Kombani: Sitegemei kufukuzwa kazi Monday, 03 January 2011 20:11

  [​IMG]Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.

  Hussein Issa SIKU moja baada ya CUF, kumshauri Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kwa madai ya kutoa kauli inayowachanganya wananchi kuhusu Katiba, Waziri huyo ameibuka na kusema "Sifikirii kujiuzulu, wala sitegemei kufukuzwa"
  Juzi CUF kilimshauri rais Kikwete kuwapumzisha Waziri Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kwa kile ilichoeleza kuwa wamekuwa wakiropoka kuhusu suala la Katiba na kuwachanganya wananchi.

  Wakati mjadala wa Katiba ukiwa umepamba moto, Waziri Kombani ambaye ndiye waziri mwenye dhamana alisema, "Katiba mpya kwa sasa haiwezekani kabisa kwani sio muhimu na kuwa Serikali haina bajeti ya kushughulikia katiba mpya".

  Waziri huyo aliyepewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo kwa mara ya kwanza, alisema Serikali itaendelea kufanya marekebisho ya sheria hiyo mama wakati wowote inapolazimika.

  “Wachache waje na kitu chenye mashiko na katika maandishi, wakionyesha ni vifungu gani vyenye upungufu, kwa nini vina upungufu na wapendeekeze mbadala wake. Serikali haiwezi kufanyia kazi vitu muhimu kama hivi kwa kupata taarifa kupitia magazetini tu,” alisema Kombani.

  Naye Mwanasheria Mkuu wa Seriakali, Jaji Frederick Werema alisema, "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa.” Jaji Werema alisema hayo Desemba 27 mwaka jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu Mpya, Jaji Mohamed Othman Chande.

  "Suala la kubadilisha ibara zinazoonekana kutokidhi haja na kuingiza mambo mapya kwenye katiba, linakubalika na kwamba hayo yamekuwa yakifanyika," alisisitiza Jaji Werema na kutolea mfano mabadiliko ya katiba yaliyoruhusu kuingizwa kwa haki za binadamu. Lakini alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya CUF jana, Waziri Kombani alisema hafikirii kujiuzulu wala hajui kama atafukuzwa. “Mimi sijui kitu.

  Nimesema sijui chochote na wala sifikirii kujiuzulu hata suala la kufukuzwa silielewi,”alisema Waziri Kombani. Wakati Waziri Kombani akisema hivyo, Jaji Werema jana aliliambia gazeti hili kuwa "Sitaki usumbufu, mimi niko likizoni." Aliendelea ‘Sitaki usumbufu wowote kuhusu hilo na sitaki kusikia habari hizo kabisaaaa.”
  Lakini Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa hawezi kujiuzulu kwa kauli alizotoa kuhusu Katiba na Dowans.

  "Sijiuzulu ng'o," alisema Jaji na Werema na kuongeza: ''Wanaotaka nijiuzulu ni wale wasiofikiria, kwani kila mtu ana nafasi yake ya kuongea kuhusu katiba. Mimi nimetoa mawazo yangu na wengine wakitaka watoe ya kwao."
  Aliendelea, ''Kunitaka nijiuzulu ni fikra za kichanga sana na potofu. Mtu mwenye upeo mpana hawezi kusema Mwanasheria Mkuu ajiuzulu kwa hili,"alisema.

  Juzi, CUF iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa kauli hizo watendaji wakuu wa Serikali kuhusu katiba zinawachanganya wananchi hivyo Rais anapaswa kuwafukuza kazi kwa maslahi ya Serikali yake.

  "Kama Rais Kikwete atakuwa makini, anapaswa sasa kuwapumzisha Kombani na Werema ili wasiendelee kutia doa jeusi Serikali yake ambayo tayari imejaa kila aina ya matatizo," alisema Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,504
  Trophy Points: 280
  Sawa dada yangu lakini unapobebwa bebeka basi..........acha kuongea matope............................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,504
  Trophy Points: 280
  Niliyozungumza kuhusu Katiba, ni maoni yangu binafsi-Werema

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 3rd January 2011 @ 23:47

  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ametetea kauli yake ya hivi karibuni iliyotaka Katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho badala ya kuandikwa upya na kusema, yalikuwa ni maoni yake binafsi.

  Aidha, amejibu hoja iliyoanzishwa na baadhi ya wanasiasa na wadau mbalimbali wa Katiba inayomtaka ajiuzulu kwa kujifananisha na mwanafunzi aliyekuwa wa mwisho darasani ambapo alisema haambiwi aache shule.

  Katika mazungumzo yake na gazeti hili kwa njia ya simu jana Werema alisema, "sikuzungumza kwa kificho na kila mtu alinisikia nikitoa maoni yangu, sielewi ni kwa nini jambo hili linakuzwa, sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?

  "Nafikiri hilo litakupa majibu ya swali lako, kwa sasa nipo likizo, naomba niishie hapo," alisema Werema na kusisitiza kuwa Watanzania hawapaswi kusema tu na kushabikia mambo bila kuyafanyia kazi.

  Mjadala kuhusu kauli ya Werema na Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani kuwa Katiba mpya haihitajiki kwa sasa, ulichukua sura tofauti baada ya Rais Jakaya Kikwete kubariki kuanza kwa mchakato wa kupata Katiba mpya.

  Wachambuzi wa mambo ya siasa na wananchi wenye mitazamo tofauti wameibua maswali mengi ikiwamo yale yaliyohoji uwezo wa kisheria wa Werema na Kombani na kupendekeza Rais awafukuze kazi au wajiuzulu wenyewe, kwa sababu maelezo yao kuhusu Katiba yalipingana na ya tamko la Rais.

  Rais Kikwete alitoa msimamo wake wa kuunga mkono Katiba mpya Desemba 31, mwaka jana wakati akilihutubia Taifa kwa njia ya televisheni, lakini pia aliwataka Watanzania kutoa maoni yao hata yanayopingana kwa staha na kuvumiliana.

  Hata hivyo, maoni ya viongozi hao, pamoja na kuzungumza kuwa ni maoni yao binafsi yalitafsiriwa na wengi kama msimamo wa serikali uliokosolewa na baadhi ya wananchi kwa madai kuwa haukuzingatia maoni ya wengi.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,504
  Trophy Points: 280
  Nchi hii haina utamaduni wa viongozi wanaopwaya kujiuzulu wenyewe mpaka kwa mashinikizo...................Werema tayari hatuna imani naye na nafasi ya AG kwenye mchakato wa katiba mpya anapaswa awe mtu ambaye hana upendeleo wowote ule.........yeye kesha poteza sifa ya kuwa AG

  Sasa mchakato wa kuandika katiba mpya tuna imani gani kuwa mapendkezo yetu hata yachakachua na kudai wengi hawakusema hivi au vile wakati kumbe ndicho tulichosema?
   
Loading...