Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia suala hili lakini kwa bahati mbaya nimekuwa nikisikia/kusoma habari zinazopingana . Je ni nani aliyefanikiwa kuwapatanisha Rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga? Vyombo vingi vya habari vya Tanzania vimekuwa vikiandika/vikitangaza na kumsifu kwamba Rais Kikwete ndio aliyefanikiwa kuwapatanisha Rais Kibaki na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga mpaka kupelekea kuundwa kwa serikali ya mseto na kumalizika kwa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.
Wakati huo huo ukifuatilia vyombo vya habari vya nje/kimataifa kama CNN, BBC, Sky News n.k. vimekuwa vikitangaza kwenye habari zake kwamba mtu aliyewapatanisha Rais Kibaki na Raila Odinga ni Katibu Mkuu wa zamani wa UN Koffi Annan.
Nakumbuka Rais Kikwete ameshatunukiwa Shahada ya Juu ya Uzamivu (PhD) kwa kutambua juhudi zake katika kuwapatanisha viongozi hawa.
Je ukweli ukoje katika suala hili? Nani alifanikisha kuundwa kwa serikali ya mseto? Kama ni Koffi Annan, je degree aliyopewa Mh. Rais ilikuwa ni ya kutambua mchango wake katika jambo gani?
Mbona Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye naye alishiriki bega kwa bega na Annan hajatunukiwa hiyo shahada?
Naomba mnijuze wanaJF!

Mkuu hata kama Kikwete angelishiriki kikamilifu na kuwaunganisha lkn si unajua tena sikio halizidi kichwa?Koffi Annan ni kichwa na anajulikana zaidi ya kikwete na nakumbuka baada ya yeye kukutanan nao kila kitu kikawa shwari hata kama JK alifanya kila kitu lkn Annan alifagia na kumaliza kila kitu na kazi hiyo sana sana aliifanya kimataifa zaidi ya Kikwete Ki East Africa sijui nimeeleweka jamani....
Hongera kwa kweli kwa Kikwete...na Kuhusu kaka Ben si unajua tena Kikwete ni RAIS alikuwa kiongozi wa something africa sina uhakika..
maoni yangu tu
Aliyepatanisha ni Annan, alikaa Nairobi zaidi ya siku kumi au zaidi, mkapa naye alikwenda pamoja na Obasanjo. Kikwete alihudhuria baada ya kuwa makubaliano yote yameshafikiwa, yeye aliitwa kushuhudia makubalianao hayo wakati huo akiwa ni mwenyekiti wa African Union, hakushiriki hata kidogo katika mazungumzo/muafaka
Kuhusu hiyo shahada waliotoa si wanajulikana?? nadhani watakuwa na jibu ni kwanini alipewa, labda kitendo cha kupeleka majeshi Comoro
Hivi Kikwete anaonekana kama mtu mwenye guts au intelligence ya kuwasomesha watu wawili? Huyo katibu mkuu wake wa CCM Makamba tu anamchachafya, huko Zenj tu hataki hata kutia pua, halafu mnasema Kikwete kapatanisha watu Kenya.
Mugabe alimtukana Kikwete matusi ya nguoni kama mtoto wake hapo Lusaka, na Kikwete hakusema kitu. Kikwete is simply not the gutsy type, hana spine ya kunegotiate na kivuli chake mwenyewe, achilia mbali Mikenya yenye generations za enmity.
Hayo ni maoni yako, lakini yapo mbali sana na ukweli, fuatalia from day one mpaka mwisho wa muafaka
utaelimika zaidi kuliko kutumia maoni yako kama kigezo cha kuwa kikwete alifanya upatanishi huko kenya
Dah!! sasa kama ukweli unaujua kwa nn ulize?Hayo ni maoni yako, lakini yapo mbali sana na ukweli, fuatalia from day one mpaka mwisho wa muafaka
utaelimika zaidi kuliko kutumia maoni yako kama kigezo cha kuwa kikwete alifanya upatanishi huko kenya
Ni kwa mkwara wa GEORGE W BUSH rais wa Marekani wa kipindi hicho ndo maana mazungumzo haya yalifanikiwa.Inaaminika kuwa Bush alimwambia Kikwete waziwazi kuhusiana na mgogoro huu na kumpa ujumbe mzito kwenda kwa Odinga na Kibaki..Kikwete alikuwa mjumbe aliyevaa sura ya usuluhishi.Mara tu baada ya kutoka Marekani,rais wetu mpendwa alitia timu Marekani.