Kodisha shamba kwa ajili ya kilimo!

Mjasiriamali1

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
891
237
Wadau kwa anayehitaji shamba kwa ajili ya kulima nakodisha.Msimu ushafika kwa wilaya ya Handeni tunaanza kulima mwezi ujao.

Iko kuanzia heka 1 mpaka 10 au ukitaka zaidi, liko sehemu moja. kwa ajili ya shughuli za kilimo, shamba lipo wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, kutoka Dar mpaka Handeni ni masaa 5, ivo unaweza kwenda Na kurudi, shamba linalimika kwa trekta, ardhi bado ni mpya inarutuba, kwa uzalishaji wa mahindi ya biashara au mihogo hutajutia.

Mkataba Kati ya mwenye shamba Na mkodishaji utasainiwa mbele ya serikali ya mtaa. Na mashahidi. Hivyo Kama unahitaji kufanya kilimo biashara mwaka huu kwa ajili ya mahindi au mhogo karibu.

Hasa ukizingatia wilaya ya Handeni kuna biashara kubwa mno ya mahindi.

Nicheki 0713297066/0765377506
 
Last edited by a moderator:
Weka bei mkuu mimi nipo kiteto namalizia mashamba yangu nina matractor yangu yatakuja msimu wa Handeni wakimaliza huku.ila bei zake kukodi shamba kwa heka moja ni kuanzia elfu 30 hakuna bei zaidi ya hizo au weka bei zako tuzione
 
Kuna mashamba ya elfu 30, nitakuonyesha ila usije kimbia. Ila Handeni mjini(magungu) mashamba ya elfu 30 hakuna.huko vijijini kwenye nguruwe pori,nyani wa kutosha ole wako upande mahindi,wanakijiji wanasubiri upande tuu wakuibie,hata ya elfu 10 utapata, hata ya bure yasiyofunguliwa utapata, hakuna hata njia za magari.

Ucheze na pori alafu tuone kama utaweza kuingiza trekta lako, yuko Mzee anakodisha mpaka laki 1 kwa heka alafu hata elfu 90 hachukui na watu wanakodisha ardhi ya kule Si mchezo mwenyewe utaikubali.

Kama kweli we mwenyeji nitakuonyesha huko sehemu Kwangu Mimi ni elfu 50 tunaandikiana mkataba. Hakuna punguzo.

Si una tractor?Ukinilimia heka kwa 20,000/= vizuri. Na Mimi nitakufanyia 30000/= kukodi heka. Unasemaje?
 
Last edited:
kilimo cha kutegemea mvua ni upuuzz wa hali ya juu

Sio kila mtu mwenye mtaji wa kufanya irrigation, kwa wilaya ya handeni mahindi hayana upinzani. Wala hayana tatizo, ulizia wenyeji watakupa siri ya mafanikio, irrigation its costly, kwa kila kitu, alafu tunaenda kipindi cha mvua, mvua inanyesha eti na wewe unamwagilia? Itakuwa ni akili au matope?

Wakati wewe ukilalamika na kutoa negative watu tunazidi kufungua mashamba. Nakupiga ela umwagiliaji nenda morogoro huko, nenda ruvu na sijui utamwagilia nini Na mvua zinakuja, utaoneka hujakamilika watu wanapalilia wametulia mvua zinanyesha Na wewe eti unamwagilia tena kwa gharama.

Mahindi Handeni ni kutengeneza pesa tuu. I doubt Kama kweli wewe ni mkulima.
 
Last edited:
Sio kila mtu mwenye mtaji wa kufanya irrigation, kwa wilaya ya handeni mahindi hayana upinzani. Wala hayana tatizo, ulizia wenyeji watakupa siri ya mafanikio, irrigation its costly, kwa kila kitu, alafu tunaenda kipindi cha mvua, mvua inanyesha eti na wewe unamwagilia? Itakuwa ni akili au matope?Wakati wewe ukilalamika na kutoa negative watu tunazidi kufungua mashamba. Nakupiga ela umwagiliaji nenda morogoro huko, nenda ruvu na sijui utamwagilia nini Na mvua zinakuja, utaoneka hujakamilika watu wanapalilia wametulia mvua zinanyesha Na wewe eti unamwagilia tena kwa gharama. Mahindi Handeni ni kutengeneza pesa tuu. I doubt Kama kweli wewe ni mkulima.
Mkuu ni wewe uliyeanzisha uzi unaohusu kuchukua masters na katika moja ya response zako kwa waliokushauri kuhusu kilimo, biashara n.k. ulisema kilimo hakilipi? Nauliza tu.
 
Mkuu ni wewe uliyeanzisha uzi unaohusu kuchukua masters na katika moja ya response zako kwa waliokushauri kuhusu kilimo, biashara n.k. ulisema kilimo hakilipi? Nauliza tu.

Nyama one nakodisha shamba kwa wakulima sio masters. Kuna uhusiano gani Kati ya Mimi kukodisha shamba Na Mimi kwenda kufanya masters? Niulizie kuhusu details za shamba, sio details za masters nayoenda kufanya ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Weka bei mkuu mimi nipo kiteto namalizia mashamba yangu nina matractor yangu yatakuja msimu wa Handeni wakimaliza huku.ila bei zake kukodi shamba kwa heka moja ni kuanzia elfu 30 hakuna bei zaidi ya hizo au weka bei zako tuzione
Mwakajana kiteto watu kilimo kiliwatenda sijui mwaka huu itakuaje
 
Weka bei mkuu mimi nipo kiteto namalizia mashamba yangu nina matractor yangu yatakuja msimu wa Handeni wakimaliza huku.ila bei zake kukodi shamba kwa heka moja ni kuanzia elfu 30 hakuna bei zaidi ya hizo au weka bei zako tuzione
Nakodisha shamba tsh 25000 taslimu kuna heka tano, ila visiki havijang'olewa. Punguzo lipo
 
Mkuu hivi ni wewe uliyemzurumu yule dada aliyeko marekani fedha zake,baada ya kumdanganya atume fedha umlimie??nauliza tu lkn!!
 
Kuna mashamba ya elfu 30, nitakuonyesha ila usije kimbia. Ila Handeni mjini(magungu) mashamba ya elfu 30 hakuna.huko vijijini kwenye nguruwe pori,nyani wa kutosha ole wako upande mahindi,wanakijiji wanasubiri upande tuu wakuibie,hata ya elfu 10 utapata, hata ya bure yasiyofunguliwa utapata, hakuna hata njia za magari.

Ucheze na pori alafu tuone kama utaweza kuingiza trekta lako, yuko Mzee anakodisha mpaka laki 1 kwa heka alafu hata elfu 90 hachukui na watu wanakodisha ardhi ya kule Si mchezo mwenyewe utaikubali.

Kama kweli we mwenyeji nitakuonyesha huko sehemu Kwangu Mimi ni elfu 50 tunaandikiana mkataba. Hakuna punguzo.

Si una tractor?Ukinilimia heka kwa 20,000/= vizuri. Na Mimi nitakufanyia 30000/= kukodi heka. Unasemaje?
mkuu mimi nahitaji heka 20 za kununua zinapatikana
 
Shamba la kununua ngoja nikuulizie kwa Mzee mmoja alikuwa anauza. Kwa upande wa Handeni. ila kwa ifakara ninazo heka 5, nzuri Sana kilimo cha mpunga au cocoa unapiga ela tuu.
 
Back
Top Bottom