Wakati wewe unalia overtime kukatwa kodi ujue kuna walimu wanaolipwa 500k mwezi mzima bila chochote cha ziada.Rais Samia Suluhu Hassan, alipoingia madarakani kwenye hotuba yake ya kwanza, kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi(MEI MOSI), aliahidi kwamba atahakikisha mshahara tu ndiyo utakaokatwa KODI, ili kumpunguzia mfanyakazi makali ya maisha, lakini naona hili bado halijafanyiwa kazi, kwani kukata KODI malipo ya OVERTIME, BONUS na marupurupu mengine ambayo siyo permanent ni kumuongezea mzigo mfanyakazi
Kwa mfano OVERTIME huu ni muda ambao mfanyakazi kaamua kuuza uhuru wake wa kufanya mambo mengine, halafu unakata kodi huu ni uonevu mkubwa sana, unaofanywa na serikali kwa watu wake, TUPAZE SAUTI KWENYE HILI LITEKELEZWE ILI TUPUNGUZE MZIGO KWA WAFANYAKAZI, AMBALO NDILO KUNDI LINALOONGOZA KUONEWA NA SERIKALI.
Kwenye nchi hii lipa Kodi kama huna nafasi ya kukwepa tu, ukiweza kukwepa we kwepa tu.Wakate kodi posho za wabunge na mawaziri au kila mtu asikatwe. Tusihubiri uzalendo kwa wengine tu.
Nasikia hata wale wazalendo wa kaunda suti hawalipi kodi kabisa, huo uzalendo kweli?
Stori za kijiweni hizo.Wakate kodi posho za wabunge na mawaziri au kila mtu asikatwe. Tusihubiri uzalendo kwa wengine tu.
Nasikia hata wale wazalendo wa kaunda suti hawalipi kodi kabisa, huo uzalendo kweli?
Wewe muache .ndio maana William Shakespeare mwandishi Nguli kutoka Uingereza amewahi kusema kuwa aliacha kulia kwa kukosa viatu na kutembea peku pale alipokutana na mtu hana miguu.Wakati unalilia hayo marupurupu yako yasikatwe kodi, kuna wenzako wa kada nyingine hawapati chochote ndani ya mwezi mzima. Kweli dunia haiko fair.
Yaani ni sawa tu na wafanyakazi wanapolilia nyongeza ya mishahara, huku wahitimu wa vyuo vikuu wakitaabika mtaani kwa kukosa ajira. Yaani unakuta baadhi yao wako tayari kuajiriwa hata kwa mshahara wa laki 2 kwa mwezi! Na bado haiwezekani.
Duh mkuu kuwa na huruma, heri yako wewe mara 1000 wakati unalalamikia marupurupu yasikatwe kodi mimi sina hata hayo unayolalamikia ,huoni kuwa itakuwa uonevu mkubwa sana kwa sisi tusio na chochote kukatwa kodi huku wewe ambaye unapokea zaidi ukinufaika.Rais Samia Suluhu Hassan, alipoingia madarakani kwenye hotuba yake ya kwanza, kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi(MEI MOSI), aliahidi kwamba atahakikisha mshahara tu ndiyo utakaokatwa KODI, ili kumpunguzia mfanyakazi makali ya maisha, lakini naona hili bado halijafanyiwa kazi, kwani kukata KODI malipo ya OVERTIME, BONUS na marupurupu mengine ambayo siyo permanent ni kumuongezea mzigo mfanyakazi
Kwa mfano OVERTIME huu ni muda ambao mfanyakazi kaamua kuuza uhuru wake wa kufanya mambo mengine, halafu unakata kodi huu ni uonevu mkubwa sana, unaofanywa na serikali kwa watu wake, TUPAZE SAUTI KWENYE HILI LITEKELEZWE ILI TUPUNGUZE MZIGO KWA WAFANYAKAZI, AMBALO NDILO KUNDI LINALOONGOZA KUONEWA NA SERIKALI.
Serikali ni kikundi cha wahuni. Walimu ndio wanaonewa zaidi na serikali hii ya kifisadi lakini nasikia eti walimu hao hao wameanza mchango wa kumchukulia fomu chifu Hangaya ili aendelee kuwakamua. Hawa walimu ni mbwa sana. Ngoja waendelee kunyanyasika kwa ujinga wao.Rais Samia Suluhu Hassan, alipoingia madarakani kwenye hotuba yake ya kwanza, kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi(MEI MOSI), aliahidi kwamba atahakikisha mshahara tu ndiyo utakaokatwa KODI, ili kumpunguzia mfanyakazi makali ya maisha, lakini naona hili bado halijafanyiwa kazi, kwani kukata KODI malipo ya OVERTIME, BONUS na marupurupu mengine ambayo siyo permanent ni kumuongezea mzigo mfanyakazi
Kwa mfano OVERTIME huu ni muda ambao mfanyakazi kaamua kuuza uhuru wake wa kufanya mambo mengine, halafu unakata kodi huu ni uonevu mkubwa sana, unaofanywa na serikali kwa watu wake, TUPAZE SAUTI KWENYE HILI LITEKELEZWE ILI TUPUNGUZE MZIGO KWA WAFANYAKAZI, AMBALO NDILO KUNDI LINALOONGOZA KUONEWA NA SERIKALI.
Jamaa anayo hoja ya msingi ila kwakuwa wakijani hawahitaji brain, si ajabu kuwaza hivi!Kuna vijana wanatafuta nafasi za malipo hata ya elfu 3 tu kwa siku bila kupewa hata chakula wala nauli lakini bado hawajafanikiwa kupata fursa hizo. Halafu yeye anaongea habari za posho sijuwi na marupurupu gani huko kutaka yasikatwe kodi