Mwenekaya Nkulu
Senior Member
- Jul 16, 2014
- 142
- 169
Habari ya leo waungwana, naomba mwenye uelewa juu ya kitu kinachoitwa kodi ya ongezeko la thamani almaarufu VAT, ni kodi inayopaswa kulipwa na nani na kwa utaratibu upi, pia naomba kujulishwa ni biashara ya ukubwa gani ambayo mmiliki wake anapaswa kuwa na namba ya usajili ya VAT yaani VRN, kwa waelewa tafadhali naomba msaada wenu katika hilo na lolote lile ambalo linahusisha tozo za kodi, wasalaam.