Kodi ya majengo Dsm kila mmoja na tozo yake!

Kodi ya majengo Dsm kila mmoja na tozo yake!

Crocozilla

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
469
Reaction score
335
Dar es salaam ndo sehemu pekee hapa Tanzania ambayo kila mtu anatozwa kodi kulingana na utashi wa afisa kodi wa TRA. Hakuna standard ya kutoza kodi ambayo inatoa usawa kwa walipaji.

Si ajabu ukawa na ghorofa ya 800m mbezi au Masaki ukalipa 50,000 kama maelekezo ya bunge yaliyo na mwenzio akawa na nyumba ya kawaida Bunju akalipa 300,000 yaani hakuna usawa kabisa.

Nafikiri ifike mahali kodi ilipwe kulingana Na maelekezo ya bunge ili kuondoa ubaguzi. Sisi wananchi tuko tayari kulipa kodi ila kuwe na usawa na bila ubaguzi au kufahamiana.

Natambua hata rais angependa kuona wananchi tunaishi maisha mazuri maana ndiyo ndoto yake. Tunaomba TRA wazingatie USAWA NA KUONDOA KUFAHAMIANA!
 
Miaka ya nyuma mwamko haukuwa mkubwa.vipi wanatoza ya Mwaka ulioisha julai tu au wanajumlisha na miaka ya nyuma?
 
Miaka ya nyuma mwamko haukuwa mkubwa.vipi wanatoza ya Mwaka ulioisha julai tu au wanajumlisha na miaka ya nyuma?
Waliokuwa kwenye system wanatozwa na malimbikizo ya nyuma, ila kwa sasa serikali imeamua kuongeza tax base ya walipa kodi ndio maana sehemu nyingi wanatoza flat rate ya tsh. 20,000/-ili muingie kwenye system na utambulike kama mlipa kodi,, ndio waanze kuzipandisha sasa na hutakuwa na uwezo wa kukwepa tena kwani system inakutambua.
 
Dar es salaam ndo sehemu pekee hapa Tanzania ambayo kila mtu anatozwa kodi kulingana na utashi wa afisa kodi wa TRA. Hakuna standard ya kutoza kodi ambayo inatoa usawa kwa walipaji. Si ajabu ukawa na ghorofa ya 800m mbezi au Masaki ukalipa 50,000 kama maelekezo ya bunge yaliyo na mwenzio akawa na nyumba ya kawaida Bunju akalipa 300,000 yaani hakuna usawa kabisa.
Nafikiri ifike mahali kodi ilipwe kulingana Na maelekezo ya bunge ili kuondoa ubaguzi. Sisi wananchi tuko tayari kulipa kodi ila kuwe na usawa na bila ubaguzi au kufahamiana. Natambua hata rais angependa kuona wananchi tunaishi maisha mazuri maana ndiyo ndoto yake. Tunaomba TRA wazingatie USAWA NA KUONDOA KUFAHAMIANA!
Viwango vya utozwaji wa kodi za majengo unavigezo viwili kama sijakosea, 1. kuna majengo yaliyofanyiwa uthamini ambapo kodi hutozwa kulingana na thamani ya jengo.
2 majengo yasiyofanyiwa uthamini ambapo wameweka viwango sawa kwa nyumba za kawaida lakini kwa maghorofa ni tsh 50000
 
Nilivyoelewa mimi ni kwamba majengo yote ambayo hayapo katika viwanja vyenye hati miliki yatalipiwa 10,000 nyumba ya kawaida na 50,000 kwa ghorofa kuanzia 01 Julai, 2017 kutoa tofauti zilizopo. Kama nimeelewa vibaya naomba ufafanuzi wakuu
 
Nilivyoelewa mimi ni kwamba majengo yote ambayo hayapo katika viwanja vyenye hati miliki yatalipiwa 10,000 nyumba ya kawaida na 50,000 kwa ghorofa kuanzia 01 Julai, 2017 kutoa tofauti zilizopo. Kama nimeelewa vibaya naomba ufafanuzi wakuu
Me hata cjui...!!
 
Kauli ya Waziri wa fedha kwenye hotuba yake ya bajeti inawahusu watu gani aliposema nyumba za kawaida zitakuwa 10000 na ghorofa 50000, binafsi nilidhani ndiyo standard kwa nchi nzima
 
Hakuna standard ya kutoza kodi ambayo inatoa usawa kwa walipaji. Si ajabu ukawa na ghorofa ya 800m mbezi au Masaki ukalipa 50,000 kama maelekezo ya bunge yaliyo na mwenzio akawa na nyumba ya kawaida Bunju akalipa 300,000 yaani hakuna usawa kabisa.


Kwa mwendo huo usishangae kusikia road license inaendelea kutozwa kwa baadhi ya mikoa
 
utaratibu mbovu sana wa kuregister, wiki iliyopita nilikaa TRA siku kama mbili mara tunakusanya form tukaletewa kama zilivyo, sasa nimeachana nao maana tunapotezeana muda tu
 
Yani kwenyekujenga tuwmakodi kibao tunalipa na nyumba ikiisha nayo wanakulazimisha uilipie kodi
 
Nilivyoelewa mimi ni kwamba majengo yote ambayo hayapo katika viwanja vyenye hati miliki yatalipiwa 10,000 nyumba ya kawaida na 50,000 kwa ghorofa kuanzia 01 Julai, 2017 kutoa tofauti zilizopo. Kama nimeelewa vibaya naomba ufafanuzi wakuu

Hapa kwangu, nyumba ya kawaida tu inasoma, "Mamlaka ya mapato Tanzania ikizingatia Sheria ya kodi ya majengo ya mamlaka ya miji sura ya 289 na sheria ya fedha za serikali za mitaa sura ya 290, inakuarifu kwamba jengo lako tajwa linadaiwa kodi iliyopo katika orodha ya kodi za majengo ya mwaka 2016/2017 ambayo ni kiasi cha Tshs 105,000 bila ya riba".
 
Back
Top Bottom