Kodi ya Majengo bado ni tatizo

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,122
7,707
Kodi ya majengo haswa kwa nyumba ambazo hazijapimwa, hazina hati miliki wala namba za mitaa/namba za nyumba ni vigumu kukusanya kodi mpaka pale utaratibu mzuri utakapo wekwa.

Watu wengi wanao miliki nyumba wapo katika maeneo yasiyo rasmi, nyumba hazina hati, hazina namba lakini baya zaidi makadirio yaliyofanywa na maafisa wa TRA hayajazingatia vigezo hivyo kodi kuwa kubwa au hata kuwa ndogo.

Kodi ya majengo iangaliwe upya ndipo tuanze kutoza.

Kwa sasa hivi bili za madai ya kodi za majengo zimelundikana ktk ofisi za serikali za mitaaa wahusika hawajui lolote.
 
Kodi zingine hizi hazina vichwa wala mguu. Ndiyo maana Nyerere walisema mtabinafsisha hadi magereza!

Kodi za majengo?

Kwani wabunge, makatibu wakuu na mawaziri wanalipa kodi stahiki?
 
TRA pamoja na wizara ya Ardhi wana paswa waweke utaratibu mzuri kwanza haswa kwa nyumba ambazo hazina hati wala namba,

nyumba zenye hati na namba ziendelee kutozwa lkn nyumba ambazo bado hazina hati wala namba ziachwe kwanza mpaka pale utaratibu utakapo wekwa.

unawezaje kumkadiria kodi mtu mwenye nyumba ya kawaida tu ambayo haina hata hati wala haina namba ya nyumba?
tembeleeni ofisi za serikali za mitaaa utakuta lundo la karatasi za madai ya kodi kwa nyumba za aina hiyo nilio itaja, hii inadhihirisha kuwa bado mamlaka husika hazijaweka utaratibu rafiki kwa wahusika.
 
Dr.Mwigulu amepropose Jambo lililo jema kweli Ambalo litarahisisha ukusanyaji wa property tax moja kwa moja, That mean NYUMBA MOJA ~LUKU MOJA.
*NAONA WAPIGA POROJO WANATAKA KUONA MPANGO HUU SIO SAHIHI.
::SEREKALI ICHUKUWE CHAKE KWANZA,WENYE MAJENGO WATABAGAIN NA WATEJA WAO LATERLY.
*HATA KODI ZA LINE ZA SIMU SEREKALI ISIRUDI NYUMA,HIZI ZOTE TUNAITA UNSENSIBLE PAYOUT, BIASHARA ZA KUPOTEZA MUDA HAZINA NAFASI LETS GO FORWARD WABUNGE WAUNGE MKONO HAYA YOTE TUSONGE MBELE...!
::TIME IS MONEY.
 
Dr.Mwigulu amepropose Jambo lililo jema kweli Ambalo litarahisisha ukusanyaji wa property tax moja kwa moja, That mean NYUMBA MOJA ~LUKU MOJA.
*NAONA WAPIGA POROJO WANATAKA KUONA MPANGO HUU SIO SAHIHI.
::SEREKALI ICHUKUWE CHAKE KWANZA,WENYE MAJENGO WATABAGAIN NA WATEJA WAO LATERLY.
hilo la luku linaweza kuwa jawabu lkn bado linahitaji kuboreshwa zaidi, lkn je vipi kuhusu nyumba zisizo na umeme?
 
Ndo maana gharama ya kuweka umeme ni elf. 27 tu ili kila mtu aweke umeme

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
tatizo sio gharama za kuweka umeme tatizo ni uhaba wa vifaa kama vile nguzo, unaweza kukaa mwaka mzima unasubiria nguzo ya umeme!! lazima tuangalia mambo kwa uhalisia wake, usijitazame wewe au watu wanao ishi masaki, tuangalie wakazi wanao ishi pembezoni mwa miji na hata vijijini.
 
Failed state.. Natural resources zilizopo TANZANIA kweli serikali inakuja na njia za hovyo za ukusanyaji wa KODI hadi mm naona aibu SHAME ON THEM.

Hizo kodi za ajabu ajabu zinge baki huko kwenye NCHI ambazo hazina njia yoyote ile ya mapata nimeona KODI ya uzalendo kweli mbuge anainuka na kuchangia vitu kama hivyo tena huyo MP yupo humo Karibu miaka 20yrs hakuona ya kwamba tuna hitaji kodi ya UZALENDO toka hapo awali sijui.
 
makadirio ya kodi hizo zihakikiwe upya, nasema uhakiki ufanyike upya. kila jengo liwe na tozo yake kulingana na thamani ya jengo, eneo lilipo n.k
 
kodi za ajabu ajabu kama vile; kodi za kwato na kodi za kichwa tayari ziliisha futwa kitambo...ila tahadhari zisije zikarudi kwa style mpya.
 
naunga mkono kodi ya majengo kukusanywa kwa kupitia mfumo wa Luku lkn kwanza uboredhwe vizuri kwa kufanya uhakiki upya.
 
Failed state.. Natural resources zilizopo TANZANIA kweli serikali inakuja na njia za hovyo za ukusanyaji wa KODI hadi mm naona aibu SHAME ON THEM.

Hizo kodi za ajabu ajabu zinge baki huko kwenye NCHI ambazo hazina njia yoyote ile ya mapata nimeona KODI ya uzalendo kweli mbuge anainuka na kuchangia vitu kama hivyo tena huyo MP yupo humo Karibu miaka 20yrs hakuona ya kwamba tuna hitaji kodi ya UZALENDO toka hapo awali sijui.
Lawama wanaweza kupewa watangulizi waliopita katika uongozi,Awamu hii ya sita kwa GHAFLA soi rahisi kulisawazisha hilo kwa GHAFLA,Tutalazimika kuyafanya haya kwanza katika Ku sustain TAIFA HUKU RAIS WETU MPENDWA AKITAFUTA NAMNA YA KUZITUMIA KWA UHAKIKA RASILIMALI TULINAZO ITS WRONG TO BLAME MAADAM AT THIS TIME,JIULIZE KWA NINI YULE JAMAA ALIKUWA ANAPORA WATU FEDHA HUKU TAIFA HILI LIKIWA NA RASILIMALI LUKUKI?,
N.B, MAMA ANAFANYA KAZI YAKE TUMPE MUDA YAPO MAMBO YANAWEZA KUWEKWA KWA MUDA LAKINI BAADA YA MUDA FULANI YAKAONDOLEWA, "" INDIRECT HAVING TAX IS A RIGHT WAY FOR NOW"MAANA KUNAKUWA HAKUNA KUKIMBIZANA.
 
makadirio ya kodi hizo zihakikiwe upya, nasema uhakiki ufanyike upya. kila jengo liwe na tozo yake kulingana na thamani ya jengo, eneo lilipo n.k
Hapana, huo ndio utakuwa utaratibu wa hovyo "sisemi wa kipumbavu" kuliko wote, TRA walianza kukadiria watu, nyumba moja eti kwa kuwa Ina marumaru na bati la "m south" Kodi 250,000 kwa mwaka, ndio maana rais Magufuri aliingilia Kati kuweka flat rate, Kodi kwenda ku bargain na TRA ni vyanzo vya rushwa na uonevu mkubwa, makadirio yao yanaanzia 170,000 kwenda juu, ilikuwa hailipiki
 
sasa unapendekeza iweje? au makadirio ya kodi ya majengo haswa kwa nyumba/majengo ambayo hayana hati miliki au hata namba, nyumba zilizopo ktk maeneo ya pembezoni mwa miji.
toa mapendekezo.
 
Tuendeleze mawazo ya Magufuri, nyumba isiyo ya ghorofa 10,000, ghorofa moja 50,000 n.k wazee wenye nyumba zisizo na wapangaji bure, nyumba za nyasi bure
 
tatizo sio gharama za kuweka umeme tatizo ni uhaba wa vifaa kama vile nguzo, unaweza kukaa mwaka mzima unasubiria nguzo ya umeme!! lazima tuangalia mambo kwa uhalisia wake, usijitazame wewe au watu wanao ishi masaki, tuangalie wakazi wanao ishi pembezoni mwa miji na hata vijijini.
Uhaba wa nguzo na vifaa ni changamoto kwa serikali, kwa sababu ina malengo ya kukusanya kodi kupitia LUKU naamini changamoto hii wataifanyia kazi ili wapate Kodi zao.
 
Back
Top Bottom