Kansigo
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 2,670
- 2,156
Katika kila tshs 1000 utakayotoa kwenye ATM kuanzia tarehe 1 Julai, 2016 tshs 280 zitachukuliwa na TRA. Hivyo hivyo katika miamala ya M PESA, TIGO PESA nk. (ZITTO KABWE)
My Take;
Kama hili liko sahihi basi Magufuli utatuua masikini wa nchi hii. Huo urafiki wa Magufuli na masikini siuoni.
*UFAFANUZI!*
_Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo_.
_Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako_.
_Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja_'.
_Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki_.
==========
Kwa mujibu wa Hotuba ya Kiswahili
(iv) Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee. Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi.
According to Budget Speech-English Version
iv) To extend the excise duty of 10 percent on charges or fees payable by a person to a telecommunication service provider in respect of money transfers to cover all commission received in the provision of mobile money services. Under the current arrangement, the main component of fees received by any telecommunication service provider in the money-transfer-related service is outside the tax net; as it is contained in money withdraw service;
Kwa mwenye facts na data zaidi ya hizi atuwekee hapa. Ninachoelewa mimi hii kodi itatozwa kwa kampuni iko imposed kwenye kile kiasi inachokata kampuni. Mfano ukitoa Shs.10,000 unakatwa Shs.1200 na MPESA, sasa hapo serikali wanakata Shs.120 kwenye Shs.1200 uliyokatwa na MPESA.