Kocha wa Simba SC uwezo wake Mdogo

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Watanzania na Wanasimba toka aajiriwe kuinoa Simba, kocha Omog ameonesha uwezo mdogo sana. Hana mbinu mpya wala kuwazidi Kibadeni na Julio. Ni wa kawaida sana. Labda kwa kuwa haongei lugha ya kiswahili ndio maana waliomuajiri wanamwona ni wa maana.

Lakini kwa mpira hana uwezo wa kuipa mbinu Simba. Mwaka jana mbinu zake dhaifu ziliikosesha Simba Ubingwa. Na mwaka huu itakuwa hivyohivyo. Ili Simba iweze kufanikiwa inabidi iachane na Kocha huyu na kutafuta kocha mwenye mbinu.

Hilo ndio suluhisho.
Napendekeza.
 
Sasa hao unaowataja wote walisha ifundisha simba sasa sijui ww unataka kuwabeba vipi tena ....makocha ambao hata experience ya afcon hawana kocha ana mechi nne tu hajapoteza ata mchezo mmoja we unamlalamikia
 
Hii ni baada ya kutoka sare leo ila kabla ya mechi ilikuwa 'Simba rarua hao, mara Okwi ana magoli mengi kuliko Yanga' mara leo tuwapige ngapi hawa Mbao? Saa hizi wanyongeeee eti uwezo wa kocha mdogo. Wakati simba anashinda zile za Ruvu kocha alikuwa nani vile?
 
Nimesema toka aajiriwe hajaonesha uwezo. Sasa wewe naona unatunga thread yako. Muwe mnasoma na kuelewa mada za wenzenu. Acheni kukurupuka. Mimi sijataja Ruvu wala Mbao kwenye thread yangu......!
 
Mbona hukuanzisha thread yako kabla matokeo ya Mbao hayajajulikana?
Kabla ya matokeo ya leo ningetoa thread yangu ungesema mechi ya Mwadui. Na ningesema kabla ya mechi ya Mwadui ungesema mechi ya Azam......Hivyohivyo ungenirudisha nyuma mpaka mwaka 1985.
Kwa hiyo usitake kuleta hadithi ya Mbwa Mwitu na Mwanakondoo.
 
Hii ni baada ya kutoka sare leo ila kabla ya mechi ilikuwa 'Simba rarua hao, mara Okwi ana magoli mengi kuliko Yanga' mara leo tuwapige ngapi hawa Mbao? Saa hizi wanyongeeee eti uwezo wa kocha mdogo. Wakati simba anashinda zile za Ruvu kocha alikuwa nani vile?
Okwi.
 
Kumbe kilio cha Lwandamina na huku kipo!? Basi tuendelee Ku share ukongwe wetu! Japo nyinyi huwa inateremka 1.3 billion dimbani
 
Watanzania na Wanasimba toka aajiriwe kuinoa Simba, kocha Omog ameonesha uwezo mdogo sana. Hana mbinu mpya wala kuwazidi Kibadeni na Julio. Ni wa kawaida sana. Labda kwa kuwa haongei lugha ya kiswahili ndio maana waliomuajiri wanamwona ni wa maana.

Lakini kwa mpira hana uwezo wa kuipa mbinu Simba. Mwaka jana mbinu zake dhaifu ziliikosesha Simba Ubingwa. Na mwaka huu itakuwa hivyohivyo. Ili Simba iweze kufanikiwa inabidi iachane na Kocha huyu na kutafuta kocha mwenye mbinu.

Hilo ndio suluhisho.
Napendekeza.
Haya basi tumekusikia, Tangu leo wewe ndiyo kocha. Nadhani umeridhika
 
Back
Top Bottom