Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,812
- 4,409
Kocha Morocco binafsi nakukubali sana, mimi ni katika wale wachache walioamini utaipeleka timu Morocco na nikaposti uzi humu Jf, nimeona wachezaji wanakuelewa sana, tatizo lako kubwa kocha la Afcon ni kuogopa kufungwa kulikopitiliza, timu yetu ya taifa imeimarika, ina uwezo kwanini kila mechi wajilinde tu tangu ushike timu, mbona kwenye Chan walifunguka na kushinda mechi kubwa kama ya Madagascar na Burkina Faso? Mbona tulipofunguka tuliitoa Guinea iliyokuwa na wachezaji world class?
Mechi ya jana na Congo umetuangusha, timu iko mkiani bado unaiogopa? Eti mechi ngumu, hiyo hapana, niliona taifa stars ikicheza kutafuta droo tu kwa kujilinda dkk 90 kupitia possession na bado wakaotewa goli ghafla ukawaamsha wakarudisha goli, yaani kwa mpango wa mechi ya Congo wachezaji wetu hawakuwa na mpango hata mmoja wa kutafuta goli, timu ilicheza chini ya kiwango kama Abajalo au Faru dume, ovyo kabisa, wachezaji walikuwa wazito kama mawe, uvivu uliwajaa, walicheza kama wamelazimishwa au mechi ya kukamilisha ratiba, wote kasoro Mwalimu , walikimbia kimbia tu uwanjani hata hatukujua wanacheza soka au marathon. Iwapo tungefunguka na kuwafunga Congo tuliowazidi uwezo mbali kabisa leo tungekuwa na points 12 tukipata matumaini ya world cup.
Punguza uoga kocha, sisi wabongo kusema ni jadi yetu, tutasema leo kesho na hata milele, tukishinda tunasema,tukifungwa tunasema, usiogope, maandamano na uporaji ni kwa majirani , mashabiki tunaitaka World Cup na tuna kikosi cha dhahabu, fanya mambo sasa ni zamu yetu, mechi zilizobaki tufunguke tu hata tukifungwa hatuna cha kupoteza na ndo tunajifunza.