Kocha Benchikha Abdelhak Simba ni Injini ya FUSO kwenye Bajaj

Mpira wa miguu ni mchezo wa makombe, kama hakuna makombe na medali hakuna mazuri. Mtu akihoji mchakato wa mabadiliko umekwamia wapi, bil 20 ziko wapi, kwanini Rais wa heshima ndio katoa hotuba Simba day badala ya try again au Mangungu, au kwanini waliwasha moto katikati ya uwanja wa Orlando pirates ni kutaka kuivuruga timu?
Nani alikwambia mpira wa miguu ni mchezo wa medali?imekuwa Olympic hiyo?
 
Kaka kuna mambo mangapi yanafanyika Yanga mbona hamuhoji Nina Nani anajua mkataba WA Yanga na Whizmo je Kati yetu Nani anajua wamepewa kiasi gani na mkataba WA mda gani.je Nani anahoji kuhusu fred yupo wapi je Nani anahoji kuhusu kiwango cha konkon je hayo NI mazuri tumekazana na mambo ambayo pengine hayana faida na Sisi hivi unafikili ukimpaka matope jirani yako wewe ndio utakuwa msafi.
Tatizo la Watanzania ni Moja.
Yani akisemwa mmoja mnataka na mwingine asemwe serious!!
Yan Watanzania tupo hivi ukipigwa wewe na baba kwa kosa ambalo mwenzako hakupigwa unaanza kulalamika mbona flani ulimwacha seriouss!!
Yan ukifutwa Mtu kaz kwa kosa ambalo mwenzako aliachwa nalo, unafufua kaburi mbona flani mlimwacha serious!!!

Tujifunze kukubali makosa yetu sisi bila kuangalia ya mwingine.
 
muda wao umeisha we samaki
simba ina tabia ya kushikilia wazee wao (Chama, Bocco, Ndemla, etc) eti wasiende Yanga na ina tabia ya kupokea wazee (Saido, Niyonzima, etc) kutoka Yanga, ila yanga inapokea vijana (Yondani, SMG, Ajib, etc) kutoka Simba
 
Kwa wachezaji wale washikaji zake matola kina Kennedy juma na jimson mwanuke simba ina safari ndefu sana.
 
Kwani mafanikio yaliyofikiwa na Simba hadi sasa yalifikiwa chini ya viongozi malaika?
Kwa nini argument zinakuwa za kitoto namna hii?

Akina Kotei na Zana Coulibaly walioifikisha Simba Robo Fainali ya kwanza baada ya miaka mingi kutofika hapo walikuwa wachezaji chini ya uongozi upi?
Barcelona wanakaribia kumtimua XAVI je, management ya Barca ndiyo mbovu au kocha ndiye mbovu?

Acheni watu wafanye kazi zao wakifeli au wakifaulu tafuta angle ukae uamue kucheka au kulia,ni hayo tu
mkuu ,wee mkomavu
 
Mkuu lazima tuseme ukweli ili tupone, kusifia timu zetu kishabiki hakuwezi kutusaidia sisi, timu zetu na mpira wetu.

Simba mafanikio waliyokuwa wakiyapata kwa miaka 4 mfululizo yalichangiwa na vitu vifuatavyo:
1. usajili mzuri wa wachezaji vijana na benchi zuri la ufundi
2. Uongozi mzuri (Mo, Barbara, Haji Manara)
3. Pesa za mo kwa waamuzi (kununua mechi), hasa pale ambapo simba ilikuwa na mashindano mengi (ligi, caf, FA, mapinduzi) inayoshiriki kwa wakati mmoja kuliko timu nyingine. Bajeti ya kushinda mechi ilitengwa. Tusibishane kwenye hili nina ushahidi nalo.
4. Upendeleo wa TFF katika ratiba. Kuna wakati Simba ilikuwa na vipolo 11 ambavyo hajacheza.
5. KwaMkapa hatoki mtu (ulozi na ?pulizapuliza kwenye vyumba)
 
Uongo mtupu.

Weka ushahidi kayasema wapi hayo ya vibajaji na fuso kama u nkweli.
Benchikha ni kocha mkubwa sana Afrika hiyo haina ubishi, Simba ni miongozi mwa feeder clubs Afrika hasa kwa timu za Kaskazini, haiwezi kugombania wachezaji wazuri sana na timu kubwa. Sio kocha wa kukuza vipaji bali ni kocha wa matokeo ya leoleo.
 
Wacha porojo, nimeandika hivi, jibu nilichoandika:

Weka ushahidi kayasema wapi hayo ya vibajaji na fuso kama u mkweli.
 
Back
Top Bottom