Kocha atimuliwa baada ya timu yake kushinda 25-0

Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,341
2,000
youth_football.jpg

Kocha wa klabu ya Serranos B ya vijana wenye umri chini ya miaka 11 ya Hispania ametimuliwa baada ya timu yake kuwapa kichapo wenzao wa Valencia Benicalap C mabao 25-0 mnamo Juni 3, kwa sababu uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa idadi ya mabao ilikwenda kinyume na ari ya mchezo.

"Tunaamini katika kuwatia moyo wapinzani wako. Baada ya matokeo hayo, tuliamua kuwa kocha huyo aondolewe katika timu," alisema Pablo Alcaide anayesaidia kuiendesha timu hiyo.

Hata hivyo, Gazeti la El Pais la Hispania nalo pia lilichapicha habari kutoka kwa mwanasheria wa kocha huyo, ambaye alisisitiza kuwa mteja wake hakuwahimiza wachezaji kufunga magoli mengi kama walivyoweza.

Gazeti hilo liliripoti kuwa uchezaji huo wa upande mmoja hauungwi mkono katika soka la vijana Hispania, ambapo klabu nyingi hazihesabu mabao endapo watafunga zaidi ya 10.
 

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,737
2,000
Aje simba
Ili iwe mwiko yanga kuchukua kikombe kwa ushindi wa Magoli nasio pointi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom