Koboko(black mamba) aua mtoto Songwe

R.I.P mtoto. Hakuna Reptiles siwapendi kama nyoka. Kuna siku nilikuwa naanika nguo nyumbani kwangu para paap akadondoka mbele yangu nyoka wa kijani hawa wa Dar. Niliogopa. Baadae niliambiwa hawa nyoka wa Dar wa kijani sio hatari. Hatari ni wale weusi.
 
Huyu ni aina gani ya nyoka? Mana nimekutana nae mahali nikafanikiwa kumuua
IMG_20190522_082527.jpg
 
Mkuu niliendaga Porini huko Jimboni kwa Hayati Spika wa Bunge la Nne Samweli Sitta kwa siku moja unakoswakoswa na nyoka sio chini ya 5 mpaka nilivyorudi Dar sikuamini kama nimerudi salama
 
Alitokea msela mmoja tu tu akawambia wanakijiji wamuachie uwanja, akapambana nae Massa mawili hadi akamuua asee koboko ni hatari.
Wanaume wa mkoani Nyie si magangwe Hebu kabiliana nae huyo
Koboko....tunawaminia

Ova
 
Halafu kuna mada niliiona humu kuna mtu kachangia anasema ati nyoka hawaoni. Hawaonii na wakati wanakwepa fimbo balaa.
 
R.I.P mtoto. Hakuna Reptiles siwapendi kama nyoka. Kuna siku nilikuwa naanika nguo nyumbani kwangu para paap akadondoka mbele yangu nyoka wa kijani hawa wa Dar. Niliogopa. Baadae niliambiwa hawa nyoka wa Dar wa kijani sio hatari. Hatari ni wale weusi.
Ni kweli kuna nyoka wa kijani hawana lakini ujue kuna koboko wa kijani Anaitwa green mamba unachotakiwa kufanya waogope nyoka wote sababu nyoka wapo katika makundi mawili tukitumia kigezo cha sumu wapo wasio na sumu na wenye sumu

Changamoto ni kuwatofautisha kwa sababu huwa wanafanana (mimicry) sana kwa baadhi ya species nadhani huu ni mpango wa Mungu kuwafanya waogopeke kwa maadui zao
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom