Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,435
- 29,614
Wana JF, tuseme ukweli. Hili suala la mgawanyo wa mapato ya mechi nadhani linapaswa kuangaliwa upya. Klabu zinaonewa sana. Na pia iwe ni changamoto kwa klabu kuanzisha viwanja vyao. Yanga kwa mfano, kwa nini wanashindwa kupata mkopo wa kujenga uwanja wao kwa kutumia makubaliano ya asilimia makato katika kila mechi hadi deni lilipwe?
Hebu angalia kwa mfano mechi ya Yanga na Mbeya City;
Mapatao yaliyoingizwa sh. 175,285,000.
Sasa ukizinatia kwamba vipengele vifuatavyo vinapata mgawao kwa kila mechi (tofauti na klabu inayopata mapato mara moja kwa wiki), sioni kwa nini vipengele hivi vipewe hela za mgao nyingi kiasi hicho;
Mie nadhani kwa kuwa hivi vipengele vinapata mgawo kila mechi, wanastahili kupunguziwa sana asilimia ya mgao wao, ili klabu ziongezewe mapato. Mfano, kwa nini klabu zilipe gharama za mechi na pia Uwanja mamilioni yote hayo? Klabu ndio zinazotoa jasho, na wengine wote wanafaidika kutokana na bidii yao, hivyo klabu zinastahili lion's share.
Ningependa TFF itoe hesabu baada ya ligi kukamilika, tuone kila kipengele cha mgawokilipata kiasi gani kwa mechi zote za ligi zilizochezwa, na hapo ndio utagundua hawa watu wa Bodi sijui nk wanapata fedha nyingi mno kulinganisha na klabu. Huu ni utapeli ulioidhinishwa kwa klabu.
Klabu kama Yanga waangalie hapo juu; ni gharama gani wataokoa kwa kuwa na uwanja wao. Waangalie kama hizo gharama hazitatosha kuwa malipo ya mkopo wa kujenga uwanja wao.

- VAT sh. 26,738,389.83
- Gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200
- Kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50
- Uwanja sh. 21,844,111.53
- Gharama za mechi sh. 13,106,466.92
- Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92
- Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46
- Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36
Sasa ukizinatia kwamba vipengele vifuatavyo vinapata mgawao kwa kila mechi (tofauti na klabu inayopata mapato mara moja kwa wiki), sioni kwa nini vipengele hivi vipewe hela za mgao nyingi kiasi hicho;
- Uwanja
- Bodi ya Ligi
- Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
- Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)