Klabu ya Simba yathibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Habibu Kyombo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Klabu ya Simba yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi Jijini Dar es salaam, leo Julai 9, 2022 imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Habibu Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyu msimu uliopita (mzunguko wa pili) alicheza kwenye Klabu ya Mbeya Kwanza FC ambapo alifanikiwa kufunga mabao 6 na Assist 3 katika michezo 15 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Mchezaji mzawa mwenye hadhi ya kucheza timu kubwa Afrika, Habibu Kyombo ni Mnyama". imeeleza taarifa hiyo kwa ufupi ya Simba SC kwa katika ukurasa wake wa Twitter

Kyombo amekuwa mchezaji wa pili kusajiliwa ndani ya Simba SC kuelekea msimu mpya baada ya Mzambia Moses Phiri.

Screenshot_20220709-131210~2.jpg
 
Wachezaji wa ndani wana wajibu mkubwa wa kuprove wrong hawa mashabiki maandazi. Kila zikisemwa tetesi za kina Habibu, Kichuya, Mhilu, Kapama utaona mashabiki mandazi wakilaumu. Ukiwaukiza kwa hiyo asajiliwe nani,hawana jibu wao wanataka kusikia wachezaji toka nje,wanataka kusikia Ki Aziz, Okrah, Akpan, Manzok nk

Hatimaye mmepewa fursa ya kuonekana. You have to show your fucking talent and make them mute and puzzled.

Imagine mchezaji kafunga goli 6 kwenye ligi na bado mashabiki maandazi hawamtaki. Hawafikirii akipewa nafasi timu nzuri anaweza kufanya poa
 
Ipo siku Ahmedy Ally atapigwa mawe na mashabiki wa Simba, yaani usajili huu ndo wa kusimamisha Afrika.? Amewaweka mashabiki kwenye tension kubwa sana, kumbe ni mchezaji ambaye wameenda kugombaniana na Singida.? Wonders shall never end😂😂😂😂😂
 
Wachezaji wa ndani wana wajibu mkubwa wa kuprove wrong hawa mashabiki maandazi. Kila zikisemwa tetesi za kina Habibu, Kichuya, Mhilu, Kapama utaona mashabiki mandazi wakilaumu. Ukiwaukiza kwa hiyo asajiliwe nani,hawana jibu wao wanataka kusikia wachezaji toka nje,wanataka kusikia Ki Aziz, Okrah, Akpan, Manzok nk

Hatimaye mmepewa fursa ya kuonekana. You have to show your fucking takent and make them mute and puzzled.

Imagine mchezaji kafunga goli 6 kwenye ligi na bado mashabiki maandazi hawamtaki. Hawafikirii akipewa nafasi timu nzuri anaweza kufanya poa
Teh teh teh kweli Simba akikosa nyama hata majani yenye mbigili atakula. By the way kwani msimu uliopita hamkuwa na wachezaji wa ndani?
 
Ndo yale ya Yanga na yule muangola wao kale keupe kembamba..endeleeni kuwasajili hao wa kutoka ulaya tuacheni sisi tupambane na wa ndani tutaona mwisho wa ligi
Yule dogo ni bonge la mchezaji ni vile mmejaa ushamba hamjui hata ubora wa mtu.
Sijawahi kuona mchezaji ambaye mipira yake ya adhabu au kona ina hatari kama Calinhos hapa nchini.
 
Wachezaji wa ndani wana wajibu mkubwa wa kuprove wrong hawa mashabiki maandazi. Kila zikisemwa tetesi za kina Habibu, Kichuya, Mhilu, Kapama utaona mashabiki mandazi wakilaumu. Ukiwaukiza kwa hiyo asajiliwe nani,hawana jibu wao wanataka kusikia wachezaji toka nje,wanataka kusikia Ki Aziz, Okrah, Akpan, Manzok nk

Hatimaye mmepewa fursa ya kuonekana. You have to show your fucking takent and make them mute and puzzled.

Imagine mchezaji kafunga goli 6 kwenye ligi na bado mashabiki maandazi hawamtaki. Hawafikirii akipewa nafasi timu nzuri anaweza kufanya poa
Umenena vema sana kiongozi. Yani sisi wabongo ni washobokaji sana nalazimika kutumia hilo neno japo linawezekana lisionekane ni zuri lakini haina namna inabidi nilitumie hilohilo tu. Hivi hapa bongo kuna mvhezaji gani mzawa ambaye timu za Simba na Yanga zitamsajili washabiki walipuke kwa shangwe? Naamini wapo wachezaji wetu wengi wazuri kushinda hata hao wa nje tunaowaabudu lakini ni hopeless tu. Hivi mchezaji zaji kama Chiko anamzidi nini Kichuya au Nado wetu? Mugalu ana nini cha zaidi kumzidi Lusajo au Mpole? Ni vile tumeshakuwa washobokaji tu. Naamini kuna mashabiki wanatamani hata timu ziwe zinasajili wachezaji wote wa nje wakiamini ni bora kuliko wazawa, tuthamini na kuviheshimisha vya kwetu kwanza kabla ya kuwaabudu hao wa 'kimataifa'
 
Ndo yale ya Yanga na yule muangola wao kale keupe kembamba..endeleeni kuwasajili hao wa kutoka ulaya tuacheni sisi tupambane na wa ndani tutaona mwisho wa ligi
Naona unamtafuta Madam Sepetu kwa kipenzi chake #calinho#
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Habib Kiyombo wa Mbao Fc na huyu aliyesajiliwa simba. Mwenyezi Mungu amsaidie kurejea kwenye kiwango chake cha awali.

Kiukweli huyu wa sasa, ni wa kawaida sana.

By the way, na Kichuya naye mnamtambulisha lini?
Kwa Simba ya sasa Kichuya ni wa muhimu sana kwani hakuna winga wa kushoto natural na hilo limeicost timu msimu mzima. Tangu mikisoni aondoke hakuna winga alieweza kukaribia hata robo ya kuweza kuziba hilo gap lililoachwa. Kwangu kama Kichuya akisajiliwa utakuwa usajili mzuri
 
Umenena vema sana kiongozi. Yani sisi wabongo ni washobokaji sana nalazimika kutumia hilo neno japo linawezekana lisionekane ni zuri lakini haina namna inabidi nilitumie hilohilo tu. Hivi hapa bongo kuna mvhezaji gani mzawa ambaye timu za Simba na Yanga zitamsajili washabiki walipuke kwa shangwe? Naamini wapo wachezaji wetu wengi wazuri kushinda hata hao wa nje tunaowaabudu lakini ni hopeless tu. Hivi mchezaji zaji kama Chiko anamzidi nini Kichuya au Nado wetu? Mugalu ana nini cha zaidi kumzidi Lusajo au Mpole? Ni vile tumeshakuwa washobokaji tu. Naamini kuna mashabiki wanatamani hata timu ziwe zinasajili wachezaji wote wa nje wakiamini ni bora kuliko wazawa, tuthamini na kuviheshimisha vya kwetu kwanza kabla ya kuwaabudu hao wa 'kimataifa'
umenigusa ulipotoa mifano..hawa kina Mugalu, Chiko, Makambo wanawazidi nini domestic players. Huko Azam ndio usiseme kuna rundo la wachezaji wa nje lakini hata majina hatuwajui
 
Kwa Simba ya sasa Kichuya ni wa muhimu sana kwani hakuna winga wa kushoto natural na hilo limeicost timu msimu mzima. Tangu mikisoni aondoke hakuna winga alieweza kukaribia hata robo ya kuweza kuziba hilo gap lililoachwa. Kwangu kama Kichuya akisajiliwa utakuwa usajili mzuri
Ndiyo hivyo sasa. Ameshakula mkataba. Bado tu kutambulishwa rasmi. Hivyo msimu ujao atachezea timu yake pendwa ya simba.
 
Back
Top Bottom